Wednesday, July 10, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 10, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.

MWANAMUZIKI MARIAH CAREY ADONDOSHWA CHINI NA VIATU VIREFU...!!!

Mariah Carey
Mariah Carey
MUIMBAJI mwenye sauti yenye mvuto nchini Marekani Mariah Carey ajikuta katika wakati mgumu na aibu ya aina yake baada ya viatu virefu maarufu kwa jina la 'high heels' kumdodosha wakati akicheza shoo ya video ya nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Beautiful'
Viatu virefu ni moja ya vitu ambavyo muimbaji huyo huvipenda lakini huenda hatotaka tena kuvisikia kutokana na hali iliyompata kudondoshwa na viatu hivyo na kumsababishia maumivu makali na hatimaye kukimbizwa hospitali .

Mtu wakaribu wa mwanamuziki huyo aliiambiwa chanzo kimoja cha habari kuwa ajali hiyo ilitokea wakati wa utengenezaji wa video ya remix ya 'Beautiful' iliyokuwa ikiongozwa na muwewake Nick Canno, ndipo muimbaji huyo alidondoka na kusababisha maumivu ya bega. 

Wakati huo huo chanzo kingine kiliuambia mtandao wa New York Post kuwa ajali hiyo ilitokana na viatu virefu alivyokuwa amevaa wakati anacheza video hiyo. 

HII NDIO TWEET YA AGNES MASOGANGE BAADA YA TAARIFA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Katika picha agnes masogange anaonekana akihesabu mihela yake na akatweet kuwa " Anatafuta hela sio umbeya watu wasile bata mnazusha"

KAMATI KUU YA CHADEMA YABARIKI FUJO MIKUTANONI .... WAANDAA "RED BRIGADE"

MUHTASARI
Ili kukabiliana na vitendo vya fujo vinavyofanywa na vijana wa CCM dhidi ya wagombea, Wanachama na viongozi wa CHADEMA, Kamati Kuu imeagiza kwamba kitengo cha ulinzi cha Chama “Red Brigade” kiimarishwe zaidi kwa kuhakikisha kuwa vijana wote wa Red Brigade Nchi nzima wanapewa mafunzo maalum ya UKAKAMAVU yatakayoandaliwa katika Makambi maalum katika mikoa yote.
RIPOTI KAMILI
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA KILICHOFANYIKA TAREHE 06-07/07/2013 KATIKA HOTEL YA BLUE PEARL, DAR ES SALAAM.

Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ilikutana katika Kikao cha dharura kuanzia tarehe 06-07/07/2013 katika Hotel ya Blue Pearl Dar es salaam kujadili pamoja na mambo mengine Rasimu ya Katiba mpya na hali ya Siasa nchini.

Kamati kuu imejadili na kuyatolea maamuzi mambo mbalimbali kama ifuatavyo:

1:0. Hali ya Siasa Nchini.

Kamati kuu imepokea taarifa ya hali ya siasa nchini na kuzingatia mambo yafuatayo:

a) Shambulio la Bomu Arusha.

 Kamati Kuu imesikitishwa na kulaani kwa nguvu zote tukio la Bomu Arusha lililosababisha watu wanne kuuwawa na zaidi ya watu 70 wengine kujeruhiwa vibaya.

KASEJA ANAWINDWA KILA KONA, USIKU NA MCHANA



KLABU za APR ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya zipo katika harakarti za kumwania aliyekuwa kipa namba moja wa timu ya Simba, Juma Kaseja, imefahamika.
Habari za uhakika ambazo Sports Lady Blog imezinyaka zinasema viongozi wa timu hizo wameshaanza mazungumzo na Kaseja ili kumsajili kwa msimu ujao katika nchi hizo.
 
Mdau mmoja wa soka ambaye yupo karibu na uongozi wa timu hizo, alidokeza jana kwamba, kwa nyakati viongozi wa timu hizo mbili, wamekuwa kwenye harakati za kumsaka Kaseja, wakiamini bado ni kipa mwenye uwezo mkubwa langoni.
 
Licha ya kutemwa kwenye kikosi cha Simba kwa msimu ujao, Kaseja bado kipa namba moja wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha wake Kim Poulsen, raia wa Denmark.
Habari zaidi zinasema, klabu ya APR iliyofika fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashabiki na Kati-Kagame Cup na kufungwa na Vital’o wiki moja iliyopira nchini Sudan, inapewa nafasi kubwa ya kumpata kipa huyo.
 
Hayo yanatokea huku Kaseja akiwa kwenye kambi ya timu ya Stars inayojiandaa na mechi ya kuwania tiketi ya Fainali za Afrika kwa Nyota wa Ndani –CHAN dhidi ya Uganda itakayopigwa Julai 13, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
“Ujue baada ya Simba kutangaza kuachana na Kaseja, kuna timu nyingi hasa za nje zimeonesha nia ya kutaka kumsajili lakini mpaka sasa ni APR na Gor Mahia ndio wako makini zaidi na mchakato huo,” kilisema chanzo hicho.

HUYU NDIE MWIGIZAJI WA HOLLYWOOD ALIYEMTUKANA OBAMA NA MKE WAKE

amanda bynes obama ugly tweet

 
 
Anaitwa Amanda Bynes ni mwigizaji maarufu HoolyWood. Wiki chache zilizopita alikua katika vita ya maneno na msanii Rihana kupitia mtandao wa twitter, sasa vita hiyo kaihamishia kwa Raisi wa nchi yake Obama pamoja na mke wake.

Katika tweet aliyoandika jana alisema “Barack Obama and Michelle Obama are Ugly” na mda mchache tu baada ya kuandika hivyo watu walianza kumshambulia kwa kumwambia kua alichofanya si kitu kizuri kabisa. Pia katika kuonyesha kua watu hawamungi mkono wengi wa followers wake walimunfollow.


Hii si mara yake ya kwanza kuwaita watu weusi ugly kwani alishawahi kumuita na Drake jina hilo

MWANAMKE APEWA MIMBA NA MAITI, ALIJIFANYISHA MAPENZI WAKATI ANAMUOGESHA.


Mwanamke mmoja mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti ameushangaza ulimwengu kwa kitendo chake cha Kujilazimishia mapenzi kutoka kwa mwanaume ambaye amekufa hadi kufikia kupata Ujauzito.
Felicity Marmaduke (38), Mkazi wa Lexington Missouri, alikumbwa na mkasa huo baada ya kumtamani marehemu huyo wakati wa kumuosha na ndipo alipoamua kujiweka juu yake na kuanza kufanya naye mapenzi, cha kushangaza ni kwamba maiti hiyo iliweza kutoa mbegu za kiume.

Baada ya wiki mbili, mwanamke huyo alienda kujipima ujauzito baada ya kujihisi tofauti na ndipo alipogundua ya kwamba ameshika mimba.
Ilimbidi atoe taarifa kwa familia husika ambayo ilimfungulia mashataka kwa kitendo chake hata hivyo naye amefungua mashtaka akidai iuzwe moja ya nyumba ya marehemu huyo ili alipwe gharama za matunzo.

MCHUNGAJI AKAMATWA KWA KOSA LA KUUPINGA USHOGA NA USAGAJI.



Tonny Miano ni Mchungaji kutoka nchini mMarekani ambaye alikwenda Nchini Uingereza katika Kufanya Mahubiri Huko. Kilichomkuta kilisababishwa na yeye kusema ya kwamba tabia za kishoga na kisagaji ni Dhambi na hazimvutii Mungu,.


Polisi walipigiwa simu na mwanamke mmoja aliyekuwa eneo la tukio akilalamika ya kwamba hajafurahishwa na maneno anayoongea Tonny, ambaye ni askari mstaafu wa jeshi la polisi nchini Marekani.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...