KAMATI KUU YA CHADEMA YABARIKI FUJO MIKUTANONI .... WAANDAA "RED BRIGADE"
MUHTASARI
Ili kukabiliana
na vitendo vya fujo vinavyofanywa na vijana wa CCM dhidi ya wagombea, Wanachama
na viongozi wa CHADEMA, Kamati Kuu imeagiza kwamba kitengo cha ulinzi cha Chama
“Red Brigade” kiimarishwe zaidi kwa
kuhakikisha kuwa vijana wote wa Red Brigade Nchi nzima wanapewa mafunzo maalum
ya UKAKAMAVU yatakayoandaliwa katika Makambi maalum katika mikoa
yote.
RIPOTI
KAMILI
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA KILICHOFANYIKA TAREHE
06-07/07/2013 KATIKA HOTEL YA BLUE PEARL, DAR ES SALAAM.
Kamati kuu ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo ilikutana katika Kikao cha dharura kuanzia
tarehe 06-07/07/2013 katika Hotel ya Blue Pearl Dar es salaam kujadili pamoja na
mambo mengine Rasimu ya Katiba mpya na hali ya Siasa nchini.
Kamati kuu
imejadili na kuyatolea maamuzi mambo mbalimbali kama ifuatavyo:
1:0. Hali
ya Siasa Nchini.
Kamati kuu imepokea taarifa ya hali ya siasa nchini na
kuzingatia mambo yafuatayo:
a) Shambulio la Bomu Arusha.
Kamati
Kuu imesikitishwa na kulaani kwa nguvu zote tukio la Bomu Arusha lililosababisha
watu wanne kuuwawa na zaidi ya watu 70 wengine kujeruhiwa vibaya.
No comments:
Post a Comment