Friday, July 19, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA PROFESA LIPUMBA KWA MAZUNGUMZO IKULU DAR


  
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alikutana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba na kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam.
 
 Mazungumzo hayo yalihusu masuala mbalimbali ya siasa na uchumi nchini.Pichani Rais Kikwete akiwa na Professa Lipumba katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana. 
 
Rais Kikwete, akiagana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba baada ya mazungumzo yao jana. Picha na Fredy Maro

MNYIKA AANIKA NAMBA ZA MAWAZIRI KWA UMMA...!!!

  Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.

Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba kwamba; “Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili”, naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:

Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo.

Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

WEMA SEPETU KUOZEA JELA, ALICHOKIFANYA SAFARI HII....!!!


KUNA kila dalili kwamba mrembo anayetamba kwenye filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au Madam jela inamwita na anatakiwa kufanya maombi ili kukwepa kifungo maishani mwake.

Hali hiyo inafuatia staa huyo kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena Jumatano iliyopita, pale alipopanda katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar kwa kosa la kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni meneja wa hoteli moja iliyopo Kawe Beach jijini Dar, Godluck Kayumbu.


Kabla ya  kupandishwa  kwa ‘pilato’,  staa huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame alikuwa akisakwa na askari kwa siku kadhaa na kufanikiwa kuwapiga chenga za hapa na pale.

ANASWA AKIFUTURU
Hata hivyo, mbio zake ziliishia ukingoni Julai 16, mwaka huu, alipokamatwa saa mbili usiku akiwa anafuturu na wageni wake nyumbani kwake, Kijitonyama Dar.

MTITI KIDOGO
Askari saba walifika nyumbani kwake wakiwa ndani ya Land Rover ‘difenda’ kwa ajili ya kumkamata, hata hivyo walipata upinzani kidogo kutoka kwa mlinzi wa staa huyo ambaye alikuwa akizuia bosi wake asikamatwe ambapo ilibidi askari hao wakaze msuli na kutuliza mtiti uliokuwa ukitaka kutokea.

MZEE WA MIAKA 63 ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMBAKA MSICHANA WA MIAKA 16 NDANI YA MSIKITI...!!!


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma, imemhukumu Ahamad Fadhil (63), kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16 ndani ya Msikiti wa ni Mwembe Mmoja, mjini hapa.

Hukumu hiyo ilitolewa na jana na Hakimu wa mahakama hiyo, Obadiah Bwegoge, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa.


Hakimu Bwegoge alisema mahakama hiyo inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili liwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia ya kikatili kama yake.


  Alisema upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani hapo mashahidi watano ambao bila kuacha shaka, walithibitisha kuwa mshtakiwa huyo alimbaka msichana huyo (jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.


Alisema shahidi wa kwanza upande wa Jamhuri ambaye ni mlalamikaji, alidai kuwa siku ya tukio, saa nane 8:00 mchana, alikwenda msikitini hapo kuomba msaada kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kifafa.

SERIKALI YASISITIZA KUWA "KODI YA LINE ZA SIMU" IKO PALE PALE...!!!


Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesisitiza uamuzi wa Serikali kuendelea kutoza Sh 1,000 kwa kila mwezi kwa laini ya simu, licha ya kampuni za simu na wanasiasa kupinga.

Akizungumza na mwandishi juzi, Mgimwa alikumbusha wanaolalamikia kodi hiyo, kwamba suala la ulipaji kodi kwa taasisi au watu binafsi, ni la kisheria kulingana na mapato yao na hali halisi iliyopo.

Pia alieleza kushangazwa na matangazo ya baadhi ya kampuni kuhusu utozwaji kodi wananchi akisema wananchi ndio wanataka barabara, maji na umeme vijijini na kodi hizo zinakwenda kutumika huko.

Kwa mujibu wa Mgimwa, kodi ya laini za simu na ya intaneti, imetengwa ikatumike kusaidia maji na uwezo wa Serikali kupeleka elimu vijijini jambo ambalo ni la maendeleo.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 19, 2013

MASISTER BANDIA WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA ...!!!

Wanawake watatu wamekamatwa kwa madai ya kujaribu kusafirisha dawa za kulevya kupitia uwanja wa ndege wakiwa wamevalia kama masista.
 
Wasafirishaji hao walisimamishwa wakati wakiwasili kwenye kituo maarufu cha mapumziko nchini Colombia, sababu polisi walifikiri kwamba mavazi yao hayakuwa yakionekana halisia.
Maofisa waligundua kwamba kila mwanamke kati yao alikuwa na zaidi ya kilo 4 za cocaine zikiwa zimefungwa katika miguu yake.

Wakiwaongezea fedheha katika mashitaka, wasafirishaji hao walipangwa mstari mbele ya waandishi wakiwa bado wamevalia mavazi yao ya kituko kuficha ukweli.

LOWASSA AMCHAMBUA RAIS KIKWETE...!!!


Na Swahili TV
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa  Edward Lowassa, amemsifia Rais  Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata heshima  katika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Swahili TV jijini Washington DC.

“Ni hivi karibuni  tu  Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani  George W.Bush  walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa” alisema Mheshimiwa Lowassa.

TAARIFA MAALUM YA TFDA KWA UMMA KUHUSU UTHABITII WA DAWA AINA YA 'DICLOFENAC' ILIYODAIWA KUWA NA MDHARA MWILINI..!

1.Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ina jukumu la kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kuhakiki ubora, usalama na ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

2. Hivi karibuni, TFDA imepokea taarifa ya kuwepo kwa hofu juu ya usalama wa dawa aina ya Diclofenac kupitia mitandao ya simu na vyombo vya habari. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:
a. Diclofenac ni dawa iliyoko kwenye kundi la dawa zinazojulikana kitaalam kama “Non – Steroidal Anti-inflammatory Drugs”(NSAIDs). Dawa hizi hutumika kutuliza maumivu na kuondoa uvimbe unaosababishwa na



magonjwa mbalimbali. Magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya viungo, mifupa, uvimbe wa fizi na maumivu ya kichwa.

b. Mamlaka imesajili dawa ya Diclofenac kutoka makampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi baada ya kutathmini ubora, usalama na ufanisi wake. Hata hivyo Diclofenac, kama ilivyo kwa dawa nyingine, ina madhara yanayofahamika. Kwa baadhi ya wagonjwa Diclofenac inaweza kusababisha vidonda vya tumbo, kuumwa kichwa, kuharisha, kutapika na kuwashwa mwili.



c. Pamoja na madhara yaliyoainishwa hapo juu, hivi karibuni imetolewa taarifa na Mamlaka ya udhibiti wa dawa ya nchi za Umoja wa Ulaya (European Medicines Agency) kwamba watu wenye matatizo ya moyo na shinikizo la damu, kisukari, waliowahi kupata kiharusi, wenye lehemu (cholesterol) nyingi kwenye damu, mshituko wa moyo na wanaovuta sigara wanaweza kupata matatizo kwenye moyo na mfumo wa damu ikiwa watatumia Diclofenac kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...