Saturday, November 15, 2014

BUTIKU AMKINGIA KIFUA WARIOBA

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Mwalimu Nyerere , Joseph Butiku 

Taasisi ya Mwalimu Nyerere imesema kuwa wanaotaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akae kimya kuhusu Katiba Inayopendekezwa hawana hoja.
Imesema kuwa wanaosema hivyo hasa wale wa chama tawala (CCM) wanatakiwa kujiuliza kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita wamefanya nini kuhusu Katiba, ikisisitiza kuwa itaendelea kufanya midahalo ya kuwaelimisha Watanzania kuhusu mchakato wa Katiba ili utakapofika wakati wa kura ya maoni waelewe kipi wanatakiwa kukifanya kwa mustakabali wa taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Joseph Butiku alisema hayo jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu na gazeti hili kuhusu kazi na majukumu ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere tangu ilipoanzishwa hadi sasa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

G20 YAMUONYA PUTIN AONDOKE UKRAINE

Viongozi wa mataiifa ya magharibi wanaohudhuria mkutano wa mataifa tajiri, G-20 mjini Brisbane, Australia, wameionya Urusi ifuate makubaliano ya kusitisha mapigano Ukraine, ama sivyo itakabili vikwazo zaidi.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alimwambia Rais Putin kuwa uhusiano baina ya Ulaya na Urusi utabadilika iwapo wanajeshi wa Urusi watabaki Ukraine.
Rais Obama alisema hatua za Urusi zinachusha.
Urusi inakanusha kuwa ina wanajeshi wake ndani ya Ukraine.
Msemaji wa Bwana Putin alitoa maanani ripoti kuwa kiongozi wa Urusi anapanga kuondoka mapema kwenye mkutano. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

EBOLA YAISHA DRC, YAONGEZEKA S-LEONE

Jamhuri ya Demokrasi ya Congo imejitangaza kuwa haina tena virusi vya ebola baada ya virusi kuambukiza watu kwa miezi mitatu na kuuwa wagonjwa karibu 50.
Virusi vya Ebola vilivyoathiri Congo ni tofauti na vile vya Afrika Magharibi.
Lakini Waziri wa Afya, Felix Kabange Numbi, amewasihi watu bado kuwa macho - kwamba kumalizika kwa ugonjwa, haimaanishi kuwa nchi haiko kabisa hatarini.
Na Daktari wa Sierra Leone ambaye ameambukizwa Ebola amepelekwa Marekani kwa matibabu.
Martin Salia, ambaye ana kibali cha makaazi Marekani na ambaye ameoa Mmarekani, atatibiwa wakati ametengwa kwenye kitengo maalumu katika jimbo la Nebraska.
Haijulikani iwapo Dr Salia, daktari wa upasuaji, aliuguza wagonjwa wa Ebola Sierra Leone.
Hospitali alikofanya kazi haina kituo cha kuuguza wagonjwa kama hao.
Dakta Salia atakuwa mgonjwa wa 10 wa Ebola kuuguzwa Marekani.
Hadi sasa watu zaidi ya 5,000 wamekufa kutokana na Ebola Afrika Magharibi.
Juma hili iliripotiwa kwamba wakati idadi ya maambukizi ya Ebola yanapungua Liberia na Guinea, bado yanaongezeka nchini Sierra Leone.
Na katika tukio jengine, Ufaransa imewashauri raia wake wasiende katika sehemu fulani za Mali baada ya watu watatu kufariki huko kwa sababu ya Ebola.
Raia wa Ufaransa walioko Mali wameambiwa wafuate ushauri wa serikali ya Mali. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 15, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

GUINEA IKWETA KUANDAA AFCON 2015


Guinea ya Ikweta inaandaa michuano ya AFCON mwakani

Shirikisho la soka la Afrika CAF limeichagua na kuipatia nafasi Guinea ya Ikweta kuandaa fainali za kombe la Afrika 2015 kuchukua nafasi ya Moroko iliyojitoa wiki iliyopita. Awali Rais wa CAF Issa Hayatou alikuwa na majadiliano yenye manufaa na Rais wa nchi hiyo tajiri ya mafuta Teodoro Obiang Nguema mjini Malabo kabla ya kufikia hatua ya kuikabidhi nchi yake dhamana hiyo.
Taarifa ya CAF imethibitisha leo ijumaa kuwa Guinea ya Ikweta mojawapo ya nchi ndogo barani Afrika imepewa jukumu hilo kubwa la kuokoa jahazi la michuano hiyo na itashiriki fainali hizo kama ilivyo kawaida ya mwenyeji. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...