Monday, July 20, 2015

NCHIMBI AENGULIWA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE...!!!

Dr. Emmanuel Nchimbi

KAMATI ya Siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Songea Mjini imetupilia mbali fomu ya mgombea UBUNGE Dr. Emmanuel Nchimbi kwa madai kuwa fomu hiyo haikuwa na vigezo na kusababisha kushindwa kuijadili baada ya mgombea kutokuwepo kwenye kikao hicho.

Akizungumza asubuhi ya leo ofisini kwake katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Juma Mpeli alisema kuwa mpaka jana majira ya saa kumi jioni fomu za kugombea ubunge jimbo la Songea Mjini zilipokelewa tisa (9) lakini fomu moja ya Dr. Nchimbi ilikuwa imechukuliwa na mmoja wa wakazi wa Songea na ikalejeshwa siku hiyo hiyo ikiwa imejazwa.

Alisema kuwa fomu hiyo ya mgombea ilishindikana kujadiliwa kwa kuwa mgombea mwenyewe Dr. Nchimbi hakuwepo kwenye kikao ambacho wagombea wote waliitwa kujadiliwa kadri ya maelezo waliyoyatoa kwenye fomu ya kugombea ubunge kwenye jimbo hilo.

MAN U KUTOONGEZA WASHAMBULIAJI

Kocha Mkuu wa Manchester United Louis Van Gaa

 Kocha mkuu wa Manchester United Louis Van Gaal ametamba kuwa hatanunua mwingine kwani alio nao kwa sasa wanatosha wakiongozwa na Wayne Rooney.

Pamoja na Wayne Rooney washambuliaji wengine waliobaki ni Javier Hernandes Chicharito, na James Wilson baada ya mshambuliaji mpachika magoli Robin Van Persie kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki hivi karibuni na Radamel Falcao mkopo wake kumalizika.

Van Gaal anatarajia kumtumia Rooney kama mshambuliaji pekee pale mbele ambapo atasaidiwa na Mephis Depay aliyesajiliwa wakati wa majira ya joto kutoka PSV Eindhovenya Uholanzi. Van Gaal anatamba kuwa Depay anaweza kuwa mshambuliaji wa katikati tofauti na alivyokuwa akitumika wakati alipokuwa PSV.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...