Wednesday, November 06, 2013

LULU AFUNGUKA KUHUSU YEYE KUCHUMBIWA...!!!

 
Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu amekanusha fununu zilizoandikwa kwenye gazeti la udaku liitwalo ‘Filamu’ kwamba amechumbiwa na muda mchache ataolewa.
 
Akizunguza jana  kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muigizaji huyo wa Foolish Age, alisema hajachumbiwa na mtu yeyote ila ni magazeti ya udaku tu ndio yamekuwa yakiandika kile yanachojisikia.
 
“Mimi sijachumbiwa na hakuna mtu yeyote aliyenichumbia na kama itatokea siku nikachumbiwa kila mtu atajua, na ni mimi mwenyewe ndiye nitakaesema,” alisema mrembo huyo.
  “Lakini sasa sijajua wao wamepata hiyo habari kutoka kwenye chanzo gani, by the way kwaajili kumekuwa na habari kila kukicha kila mtu anayejisikia kuandika anaandika ,anaamka anaandika, anaamka anandika. 

 "Kwa hiyo leo wameandika nimechumbiwa, kesho wataandika nimeolewa, kwa hiyo inategemea na mood ambayo wao waliamka nayo, kwamba ‘leo Lulu tumchumbie, tumuozeshe, tumuachishe’, I don’t know.
 
“Kuchumbiwa, kuolewa,kuwa mke ni vitu ambavyo tumeumbiwa binadamu, vipo kama ukiwa mpango wa mwenyezi Mungu nitachumbiwa na nitaolewa.” Lulu

ANGALIA PICHA ZA JUX KING OF PAMBA KWA WASANII WA BONGO

http://distilleryimage8.ak.instagram.com/d08bd338f3c411e289bf22000a1fa4a9_7.jpg

http://distilleryimage2.ak.instagram.com/ddfe26f6ef9611e2a63622000a9e28ec_7.jpg


http://distilleryimage11.ak.instagram.com/cbffd894453311e3984822000a1f9707_7.jpg 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

UJUMBE MZITO WA LULU KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameliomba Bunge kurekebisha sheria za Magereza katika vikao vyao vinavyoendelea mjini Dodoma.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam juzi, Lulu alisema kutokana na kukaa huko kwa mwaka mmoja, ameona mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho.
“Unaweza ukamkuta mfungwa ana miaka zaidi ya 20 lakini hajawahi kufikishwa mahakamani wala kuulizwa chochote kutokana na kitu ambacho kimempeleka hapo, kiukweli hata kama ana makosa haiwezekani kumkalisha miaka yote hiyo pasipo kusikilizwa,” alisema.
Alisema yeye amekaa huko kwa muda mfupi lakini amepata shida sana kuyazoea mazingira hayo, kwani huwezi kuishi kama nyumbani, hivyo ni vizuri ukiwekwa utaratibu mtu anasomewa kesi yake kwa muda gani.
Lulu alilazimika kukaa gerezani kwa muda huo kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa nguli wa filamu nchini, Steven Kanumba, aliyefariki dunia nyumbani kwake Sinza Vatican Aprili 7, mwaka jana

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 06, 2013

.
.
.

MAELEZO BINAFSI YA MH. ESTER BULAYA KUHUSU WAHARIFU WA DAWA ZA KULEVYA.....!!!


 bulaya
Haya ni maelezo binafsi ya Mheshimiwa Ester Amos Bulaya bungeni Dodoma November 4 2013 kuitaka serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya dawa za kulevya na kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia wahalifu wa dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 28(8) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2013, napenda kutoa maelezo binafsi ya juu ya tatizo sugu la uagizaji, uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya linaloongezeka kwa kasi kubwa nchini, lengo likiwa ni kuitaka serikali ifanye mabadiliko/marekebisho ya sheria ya Dawa za kulevya na kuanzisha Mahakama Maalum kushughulikia wahalifu wanaojihusisha na usafirishaji na biashara ya dawa za kulevya.
chinese
Mheshimiwa Spika,
Nimeona ni wakati muafaka kutoa maelezo haya, ili Bunge lako tukufu na Serikali ipate fursa ya kuona uzito wa tatizo hili kutokana na ukweli kwamba katika miaka ya karibuni tatizo la dawa za kulevya katika nchi yetu limeongezeka kwa kasi ya ajabu hali inayopelekea athari kubwa za kiuchumi, kijamii na kiafya. Na mbaya zaidi kundi kubwa linaloathirika ni kundi la vijana, ambao ndio nguvu kazi ya Taifa letu.

HILI NDILO JUMBA LA KIFAHARI LENYE UWANJA WA NDEGE HAPO HAPO NYUMBANI

article-2486741-1923386700000578-170_634x475Nyumba hii ipo huko Las Vegas Marekani na ina heka 40 na indoor car parking kubwa sana kuingiza magari zaidi ya kumi kwa wakati mmoja na upande wa mwingine ina zoo humohumo ndani, jet inayopark kwenye airport yako binafsi hapo mjengoni haina haja ya kwenda kwenye public airport na ukitaka kumiliki hii nyumba inabidi zikutoke $ 48 millioni.
article-2486741-1923389000000578-571_634x475
Vyumba vya kulala vipo vingi kiasi kwamba wakati mwingine inabidi kuwasiliana kwa simu chumba hadi chumba kwasababu ya umbali wa kufikia vyumba vingine pia kuna ofisi binafsi kiasi kwamba unaweza usiende sehemu yoyote kazi zako zote zikafanyika ndani ya hizi heka 40.
Upande wa michezo kuna uwanja wa kucheza golf, basketball, swimming pool kubwa likiunganishwa na water falls na pia kuna eneo kubwa sana la wazi na humo ndani kumewekwa nakshi na material ya gharama kuanzia dinning, jikoni hadi vyumbani.

article-2486741-1923388400000578-459_634x475

RAIS KIKWETE KULIHUTUBIA BUNGE KESHO....!!!

jk_d71ab.jpg
Rais Jakaya Kikwete, kesho anatarajiwa kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Habari zilizopatikana Mjini Dodoma jana na kuthibitishwa na uongozi wa Bunge pamoja na Ikulu, Dar es Salaam zinasema atahutubia mchana.
Kutokana na ujio huo, Serikali imewaelekeza Mawaziri na Manaibu Waziri kutotoka nje ya Dodoma hadi hapo Rais atakapokuwa amehutubia Bunge. 
Kadhalika safari zote za Kamati za Bunge ambazo zilikuwa katika mchakato wa kutekelezwa zimeahirishwa hadi baada ya kesho, ili kutoa fursa kwa wabunge wote kuwapo wakati wa hotuba hiyo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema jana kuwa hata yeye amesikia taarifa kuwa Rais atazungumza bungeni lakini hajui atazungumza kitu gani... "Hata mimi nimesikia kuwa atazungumza lakini sijui atazungumza jambo gani kwa kuwa siyo miongoni mwa watu wanaomwandalia hotuba," alisema Balozi Sefue.
Kadhalika, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alithibitisha kuwa Rais Kikwete atalihutubia Bunge, Alhamisi... "Nathibitisha ni kweli, ila kwa taarifa nyingine watafuteni watendaji wa Bunge, kama Katibu wa Bunge nadhani wana taarifa zaidi."

M23 'WAMALIZA UASI' BAADA YA KIPIGO

130913125600_m23_congo_304x171_afp_nocredit_ab833.jpg
Waasi wa M23 katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametangaza kumaliza uasi wao ndani ya nchi hiyo muda mfupi baada ya kupigwa katika ngome yao ya mwisho na majeshi ya serikali ya Congo yakishirikiana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupigana na waasi hao.
Katika taarifa walioitoa waasi hao wamesema badala ya kufanya uasi sasa wataendesha harakati zao kutumia njia ya kisiasa.
Muda mfupi uliopita Kiongozi wa waasi hao Bertrand Bisimwa ametangaza kuwaamuru mkuu wa wapiganaji wa M23 na makamanda wa vikosi vyote muhimu wa kundi hilo kuwaandaa wapiganaji wao kusalimisha silaha, kutawanyika kuondoka katika eneo la mapigano na kukubaliana na matakwa yatakayowekwa na serikali ya Congo
Awali Msemaji wa Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Lambert Mende aliambia BBC kuwa majeshi ya nchi yameishambulia ngome ya mwisho ya waasi na wamekimbia na wengine huenda wakawa wamejisalimisha.
Majeshi ya serikali ya Kongo yakishirikana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupambana na waasi hao walianza mapambano dhidi ya M23 Octoba mwaka huu na kufanikiwa kuwaondoa katika eneo la Bunagana kwenye mpaka wa Uganda ambayo ni ngome yao muhimu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...