Friday, July 17, 2015

WANAJESHI WANNE WANAMAJI WAUAWA MAREKANI

Rais wa Marekani Barack Obama

Mtu mwenye silaha amewaua askari wanne wa jeshi la wanamajiwa Marekani katika shambulio lililofanywa kwenye majengo mawili ya jeshi hilo katika mji wa Chattanooga, Tennessee.

Wanajeshi hao wote waliuawa katika jengo moja. Maafisa nchini humo wameyaita mauaji hayo kuwa ni Shambulio la ndani. 

Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linalochunguza mauaji hayo, limesema halijajua bado kilichosababisha shambulio hilo.

Kufuatia tukio hilo maeneo kadhaa yamefungwa zikiwamo hospitali na shule ili kuchukua tahadhari. "Ni mazingira ya kusikitisha kwa watu ambao wametumikia taifa kwa moyo wote,kuuawa katika mfumo huu inasikitisha.

Wakati maandalizi ya mawasiliano na familia za wanajeshi hawa yakifanyika, naomba wafahamu kuwa nazungumza kwa niaba ya raia wote wa Marakani kuelezea masikitiko yangu na kuwahakikishia kuwa tupo nao katika mazingira haya magumu".

Naye Meya wa jiji la Chattanooga Andy Berke alisema muuaji aliuawa na polisi. Pia ofisa wa polisi pamoja na watu wengine wamejeruhiwa. "tunafahamu kuwa kuna watu wanne waliouawa.

Tunafahamu kuwa muuaji pia aliuawa katika eneo la tukio na pia afisa wa polisi mmoja wa Chattanooga amepigwa risasi kwenye kifundo cha mguu na anatibiwa vilevile pale Arlanga, pia kulikuwa na watu wengine waliopigwa risasi na wametibiwa Mwanasheria mkuu wa jimbo la Tennessee, Bill Kilden, ameyaelezea mauaji hayo kama ugaidi wa ndani.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...