Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya dare s Salaam limewafukuza kazi askari watano kutokana na makosa mbalimbali ya kinidhamu yanayotokana na wizi wa fedha shilingi milioni 150 uliotokea eneo la Kariakoo lililofanyika tarehe 14/12/2012.
Katika tukio hilo askari hao walihusika katika ukamataji wa watuhumiwa na vielelezo na ndipo ilipodaiwa kielelezo (pesa) kilipotea na askari hao kuhusishwa na upotevu huo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova amewataja askari hao kuwa ni SSGT Dancan, CPL Rajab, CPL Cavin, CPL Geofrey na CPL Kawanami.