Saturday, November 01, 2014

MTANGAZAJI BEN KIKO AFARIKI DUNIA



Ben Kiko enzi za uhai wake.
ALIYEKUWA mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania, Ben Kiko, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana Oktoba 31, 2014 akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.
Kiko amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya figo kwa muda mrefu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 01, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

JEN TRAORE AJITANGAZA RAIS BURKINA FASO

Jenerali Honore Traore mkuu wa jeshi la Burkina Faso aliyejitangaza rais mpya wa nchi hiyo
Mkuu wa Jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore sasa amejitangaza kuwa rais baada ya aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Compaore kutangaza kujiuzulu.
Jenerali Traore ameshinikizwa na waandamanaji ambao walikuwa wanamtaka kuchukua usukani baada ya kuondoka kwa Bwana Compaore.
Bwana Compaore amesema kuwa amekubali kuondoka madarakani ili kutii matakwa ya waandamanaji ambao hawamtaki kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya kutawala kwa miaka 27.
Bwana Compaore sasa ametaka uchaguzi mpya wa urais ufanyike baada ya siku 90.
Awali msemaji wa jeshi alikuwa amewaambia waandamanaji kuwa bwana Compaore hayuko tena madarakani huko Ouagadougou.
Maelfu ya waandamanji walikuwa wamerejea mabarabarani kwa siku ya pili
Hata hivyo hakubaini ikiwa afisa huyo wa kijeshi alikuwa akizungumza kwa niaba ya jeshi lote.
Jeshi lilisema kuwa litafanya mkutano na waandishi habari.
Siku ya Alhamisi waandamanaji waliokuwa wamekasirishwa na jitihada za rais za kuongeza muda wa uongozi wake baada ya kutawala kwa miaka 27 waliteketeza jengo la bunge na kuvamia kituo cha televisheni ya taifa.
Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa angebaki madarakani kwa mwaka moja zaidi. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

WATAKA KIWANGO CHA KALORI KATIKA POMBE KITAJWE

Wataka pombe ionyeshe kiwango cha kalori kupunguza vitambi na unene wa kupitiliza
Pombe inatakiwa kuwa na nembo inayoonyesha kiwango cha kalori au kipimo cha joto litolewalo na chakula ili kupunguza vitambi au unene wa kupita kiasi.
Madaktari wa afya ya umma, wameonya kuwa glasi kubwa ya mvinyo inaweza kuwa na kiasi cha kalori 200- sawa na donati, aina ya maandazi.
Hata hivyo idadi kubwa ya watu hawajui madhara ya kula kiwango kikubwa cha kalori.
Waziri wa Afya Jane Ellison amesema "hatua kubwa" imefanyika kwa kuviwekea nembo vyakula, na kwa suala hilo serikali italiangalia.
Sekta ya vinywaji imesema imesema iko tayari kwa wazo hilo la kuweka nembo zenye kuonyesha kiasi cha kalori, lakini kuweka nembo zinazonyesha kiwango cha kilevi katika kinywaji ni muhimu zaidi.
Uingereza ni moja ya mataifa yenye watu wenye unene wa kupita kiasi duniani kwa kuwa na idadi ya karibu robo ya watu wazima kuwekwa katika kundi la wenye unene wa kupitiliza.
Vyakula tayari vinakuwa na taarifa za kiasi cha kalori kilichomo ndani yake, lakini pombe haimo katika sheria za Umoja wa Ulaya zinazotaka vyakula viwekewe nembo.
Mvinyo nao watakiwa kuonyesha kiwango cha kalori
Na Tume ya Ulaya inaangaliwa iwapo vinywaji viwekewe nembo yenye kuonyesha kiasi cha kalori kilichomo.
Utafiti uliofanywa na Chama cha Masuala ya Afya ya Jamii nchini Uingereza, umesema hatua hii itaungwa mkono na wanywaji nchini Uingereza.
Mkuu wa chama hicho cha RSPH, Shirley Cramer, ameiambia BBC: "Ni jambo la kushtusha kweli - asilimia 80% ya watu wazima hawana wazo la kujua kiasi cha kalori kilichomo katika kinywaji chochote na kama wanafikiri wana wazo hilo kwa ujumla wanakadiria kiasi cha chini mno."
"Itasaidia taifa kupunguza watu wenye unene wa kupitiliza na huenda kupunguza kupunguza unywaji wa pombe."

Kiasi cha kalori:

Glasi kubwa ya 250ml ya mvinyo wenye kileo cha asilimia 8% ni kalori 170 Kiasi hicho hicho cha glasi ya 250ml ya mvinyo wenye kileo cha asilimia 14% ni kalori 230 Painti moja yenye asilimia 4% ya bia ni zaidi ya kalori 180. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...