Wednesday, November 26, 2014

UKAWA WASAMBARATIKA SERENGETI


Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara, umesambaratika baada ya Chadema kuamua kusimamisha wagombea vitongoji na vijiji vyote ikiwa ni kinyume na makubaliano ya vyama hivyo.

Novemba 4, viongozi wakuu wa vyama vya Nation League for Democracy (NLD), NCCR Mageuzi, CUF na Chadema walitiliana saini ushirikiano wa kusimamisha mgombea mmoja kila ngazi ya uchaguzi kuanzia serikali za mitaa, vijiji na vitongoji. Kusambaratika kwa umoja huo kulitokana na viongozi wa vyama vya CUF, NCCR Mageuzi na Chadema kukaa vikao vitatu kupanga jinsi ya kuachiana vijiji, vitongoji na mitaa kushindikana kufuatia viongozi wa Chadema kuvitaka vyama vingine kuwaachia vitongoji 24 vya Mamlaka ya Mji Mdogo Mugumu. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

HALIMA MDEE AMKANA MKONO


Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee. PICHA|MAKTABA 

Siku moja baada ya Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kusema amelishwa sumu akiwa London, Uingereza, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amemtaka kusema ukweli na si kulihadaa Taifa kwa uongo.

Mkono akizungumza na waandishi wa habari juzi kuelezea mwenendo wa afya yake, alisema lengo la kulishwa sumu ilikuwa ni kutaka kuharibu figo zake ndani ya saa 72 kitendo kilichoshindikana.

Mdee aliyekuwa na Mkono katika ziara hiyo alisema: “Hakuna ukweli wowote kwamba alilishwa sumu, nilikuwa naye kule na mazingira aliyoanza kuumwa hadi kupona kwake ni utata... awaeleze Watanzania anaumwa nini na si kusema alilishwa sumu.

“Nilikaa kimya baada ya kuripotiwa na gazeti moja (The Citizen) kwamba Mkono kalishwa sumu, sasa amezungumza tena nikaona si busara kukaa kimya wakati alilidanganya Taifa. Mkono waeleze ukweli watu mbona unawadanganya.” Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 26, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MKOSAMALI APANDISHWA KIZIMBANI

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Felix Mkosamali. PICHA|MAKTABA 

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Felix Mkosamali amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kibondo akikabiliwa na shtaka la kumzuia karani mwandikishaji kufanya kazi yake.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Peter Makala alidai jana mahakamani hapo kuwa mbunge huyo alitenda kosa hilo juzi, baada ya kufika Kituo cha Kitongoji cha Nduta, Kijiji cha Kumhasha, Kata ya Murungu, wilayani Kibondo na kumzuia karani kuendelea kuandikisha wakazi kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Makala alidai kuwa kitendo cha kumzuia karani huyo kuendelea kufanya kazi yake ni kinyume na ukiukwaji wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Pia, alidai kuwa kitendo cha kuwazuia wakazi hao kujiandikisha ni kuwanyima haki yao ya msingi, kwani baada ya kuzuiwa waliendelea kudai kutaka kujiandikisha lakini mshtakiwa hakusikiliza kilio chao.
Mshtakiwa alikana shtaka na Hakimu Erick Marley alisema dhamana iko wazi kwa mdhamini kusaini bondi ya Sh4 milioni. Mbunge huyo alitimiza masharti na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 29.
Mkosamali alikamatwa juzi jioni baada ya kudaiwa kumnyang’nya karani vitabu na madodoso na kuyapeleka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BOKO HARAM WAFANYA MAUAJI TENA

Shambulio la bomu lililofanywa kariibu na soko.
 
Watu 78 wameuawa katika mashambulio mawili ya kujitoa mhanga yaliyofanywa sokoni, katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema mlipuko wa kwanza ulitokea wakati washambuliaji hao walipomuwekea mlipuko mwanamke mmoja mwenye matatizo ya akili.
Wakati umati wa watu wakienda kutoa msaada, mwanamke mwingine alijitoa mhanga.
Kundi la kiislamu la wapiganaji la Boko Haram ambalo linadhibiti maeneo mengine ya miji ya kaskazini mwa nchi hiyo na vijiji, linadhaniwa kuhusika na shambulio hilo.
Mwandishi wa BBC anasema Wanaigeria wamekosa Imani na jaribio la serikali ya nchi yao kufanya mazungumzo na Boko Haram, kutokana an kuongezeka kwa ghasia hizo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ZAIDI YA WATU 60 WAUAWA SYRIA

Majeshi ya Syria yafanya mashambulizi.
 
Zaidi ya watu 60 wameuwawa, katika mashambulio kadhaa ya angani yaliyofanywa na Jeshi la serikali ya Syria.
Raia wengi waliuwawa katika mashambulio tisa yaliyolenga ngome kuu za kundi la wapiganaji wa Islamic State.
Wakereketwa wameiambia BBC kuwa Hospitali kuu ya Raqqa imesalia bila huduma kwani HAKUNA chakula na umeme. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KLABU BINGWA BARANI ULAYA

 Timu ya Chelsea 
 
Usiku wa kuamkia leo kindumbwe ndumbwe cha michuano ya Klabu Bigwa barani Ulaya kiliendelea na kushuhudia Chelsea ikitoa kipigo cha mbwa mwizi mbele ya mashabiki wa Schalke 04 ya Ujuremani pale ilipoishindilia magoli 5 bila majibu.
Manchester City ya England nao wakawabamiza wababe wengine wa Ujerumani Bayern Munich kwa kwa kuwafunga magoli 3 - 2 na kufufua matumaini ya kusonga mbele katika michuano hiyo huku magoli yote matatu ya Man City yakitiwa kimiani Sergio Aguero.
Katika mechi nyingine Paris St. Germain ya Ufaransa waliwashikisha adabu Ajax ya Uholanzi kwa kuifunga magoli 3 - 1 huku Becelona kwa upande mwingine wakiisasambua Apoel Nicosia ya Syprus kwa kuishushia kichapo cha magoli 4 kwa yai.
CSKA Moscow ya Urusi na AC Roma zikatoka suluhu ya goli moja 1 - 1
Burudani hiyo itaendelea leo ambapo Liverpool ya England baada ya kufanya vibaya katika mechi zilizotangulia leo wanajaribu bahati yao wakiwa ugenini dhidi Ludogorets ya Bulgaria.
Arsenal nao watawakaribisha Borusia Dortmud ya Ujerumani huku vita vingine vikiwa ni kati ya FC Basel ya Uswis watakaopopepetana na Real Madrid. Malmo FF ya Sweden watakuwa wenyeji wa Juventus ya Italia. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...