Saturday, June 07, 2014

MWEGANE YEYA WA MBEYA CITY AAHIDI MAKUBWA TAIFA STARS, AMSHUKURU MUNGU KWA KUITWA NA MART NOOIJ


Mwagane-Yeya.pngnnnnnnnnnnnnnnNa Baraka Mpenja, Dar es salaam
MSHAMBULIAJI hatari wa Mbeya City fc, Mwegane Yeya amefurahishwa na kitendo cha kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij.
Akizungumza na mtandao huu, Mwegane amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kupata nafasi hiyo kwasababu Tanzania ina wachezaji wengi wenye viwango vya hali ya juu, lakini amechaguliwa yeye.
“Hii ni nafasi nyingine muhimu kwangu. Niliwahi kuitwa katika kikosi cha Young Future Taifa Stars na Kim Poulsen, lakini sikufanya vizuri kwasababu nilikuwa majeruhi. Naamini kwasasa nitaitumia vizuri nafasi hii”. Alisema Mwegane ambaye ni hatari kwa kufunga magoli ya kichwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz


Mwegane aliongeza kuwa kuitwa na Nooij ni ishara ya kukubali kazi yake, hivyo anajiona mwenye wajibu mkubwa wa kuisadia Stars kuelekea mchezo muhimu dhidi ya Msumbiji.
Nyota huyu wa Wagonga Nyundo wa Mbeya ni miongoni wa wachezaji wa Kikosi cha Taifa Stars kinachotarajia kuingia tena kambini Jumatano (Juni 11 mwaka huu) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura Mgoyo, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku tatu jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka huu.
Wachezaji wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Haruna Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...