Saturday, June 07, 2014

MADEREVA WA UMMA WAGOMA BRAZIL

Mgomo wa wafanyakazi hao umesababisha uhaba wa magari ya usafiri
Maafisa wa polisi nchini Brazil wametumia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji katika siku ya pili ya mgomo wa wafanyikazi wa sekta ya uchukuzi ambao umesababisha uhaba mkubwa wa usafiri wa uma katika mji wa Sao Paulo.
Takriban nusu ya vituo vya treni vilifungwa na kusababisha msongamano mkubwa wa watu katika barabara za mji huo mkubwa ambao unatarajiwa kuandaa michuano ya kombe la dunia kuanzia alhamisi ijayo.
Wafanyakazi hao wa treni wanataka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia kumi.
Awamu nyengine ya majadiliano imefeli na wafanyikazi hao wanasema kuwa mgomo huo utaendelea kwa mda usiojulikana. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...