Sunday, July 26, 2015

MLIPUKO WAUA WATU 10 SOMALIA


Takriban watu 10 wameuawa katika mlipuko huo

Takriban watu 10 wameuawa kufuatia mlipuko mkubwa uliotokea katika hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Mwandishi wa BBC katika mji huo anasema kuwa lori moja lilitumiwa kushambulia hoteli ya Jazeera karibu na uwanja wa ndege wa taifa hilo. Wajumbe wa kimataifa wamekuwa wakiishi katika hoteli hiyo ambayo imelengwa katika siku za nyuma.

Ripota wetu anasema kuwa ni moja ya mashambulizi mabaya kuwahi kushuhudiwa mjini Mogadishu. Anasema kuwa magari ya ambulansi yameanza kuokota miili.

14 WAFA KATIKA SHAMBULIO CAMEROON


Watu 14 wameuawa jana usiku katika shambulizi la bomu lililotekelezwa na Boko Haram

Watu 14 wameuawa jana usiku katika shambulizi la bomu lililofanyika kwenye jumba moja la starehe katika mji wa Maroua Kaskazini mwa Cameroon.

Siku chache baada ya kutokea kwa mashambulizi mawili ya bomu katika mji mkuu wa eneo hilo kulingana na habari kutoka kwa maafisa wa usalama. Afisa mmoja wa jeshi lililopelekwa katika eneo hilo kupambana na Boko Haram ndiye aliyetoa habari hiyo kwa siri.

Shambulizi hilo lilifanyika saa mbili kasorobo jana usiku saa za Afrika Mashariki wakati mwanaume mmoja alirusha bomu ndani ya baa katika wilaya ya Ponre kulingana na afisa huyo wa jeshi ambaye hakutaka kutajwa. Wakazi walijaribu kumfuata lakini aliwarushia grunedi kuwafukuza.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...