Thursday, September 18, 2014

SCOTLAND YAAMUA KUHUSU MUUNGANO

Wascochi wanapiga kura kuamua ikiwa wataendelea kuwa sehemu ya Uingereza au watajitawala
Wapiga kura wamekuwa wakielekea kwa vituo vya kupigia kura katika maeneo mbali mbali nchini Scotland, ambapo watu wanaamua leo ikiwa wataendela kuwa sehemu ya uingereza au wawe taifa huru kwa mara ya kwanza kabisa tangu zaidi ya miaka 300 iliyopita.
Mwandisi wa bbbc anasema kuwa siku ya leo inatarajiwa kuwa ya shughuli nyingi katika historia ya kupiga kura eneo la Scotland ikiwa asilimai 97 ya watu wamejisajili kupiga kura.
Kumekuwa na kampeni kali katika saa 24 zilizopita huku ikidhihirika matokeo yanaweza kwenda upande wowote.
Kiongozi wa chama cha Scotish National Party, Alex Salmond, ametaja kampeni ya kuitisha Uhuru wa Scotland kutoka kwa Uingereza kama tukio muhimu zaidi la kidemokrasia kuwahi kutendeka nchini humo.
Kadhalika amesema tayari limebadilisha mfumo wa maisha eneo la Scotland.
Idadi kubwa ya wapiga kura wamesajiliwa na kwa mara ya kwanza vijana wenye umri wa miaka 16 na 17 wataruhusiwa kupiga kura. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

POLISI WADAIWA KUTESA RAIA NIGERIA

Serikali ya Nigeria bado haijasema chochote kuhusu madai ya Amnesty International
Polisi nchini Nigeria wamedaiwa kuwatesa wanaume na wanawake pamoja na watoto. Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International.
Shirika hilo limechapisha ripoti yake ambayo inadai kwa watu huzuiliwa kinyume na sheria Kaskazini Mashariki mwa Nigeria ambako jeshi la serikali linapambana na wanamgambo wa Boko Haram.
Serikali ingali kujibu tuhuma hizo.
Shirika hilo linasema kuwa jeshi la Nigeria pamoja na polisi hutumia mbinu tofauti kuwatesa watu ikiwemo kuwapiga, kuwadunga misumari na kuwang'oa meno, ubakaji na dhuluma nyinginezo za kingono.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo wanajeshi huwatesa watu zaidi katika eneo la Mashariki ambako vita dhidi ya Boko Haram ni vikali zaidi.
Shirika hilo linasema kuwa kati ya watu efu tano na elfu 10 wamekamatwa tangu mwaka 2009 na kunyongwa katika kambi za wafungwa.
Ripoti hiyo yenye mada, "Welcome to hell fire", inatoa taswira mbaya sana kuhusu haki za binadamu kote nchini Nigeria, na inasema kuwa vituo vingi vya polisi vina afisaa wa polisi anayesimamia mateso na kutaka watu kulipa hongo ili kukwepa mateso hayo.
Licha ya kuharamisha mateso, shirika la Amnesty linasema kuwa wanasiasa nchini humo bado hawajapitisha sheria inayowachukulia hatua wale wanaohusika na mateso dhidi ya raia wasio na hatia. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...