Sunday, February 18, 2018

MTULIA, DR. MOLLEL WAREJEA BUNGENI UPYA

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni amemtangaza mgombea wa CCM, Mtulia Maulid kuwa Mbunge mteule wa jimbo hilo.

Mgombea huyo ameongoza kwa kura 30, 247 akifuatiwa na Mwalimu Salum wa CHADEMA kwa kura 12,353, Rajab Salum wa CUF kwa kura 1,943 na Ally Abdallah wa ADA-Tapea mwenye kura 97.
“Nashukuru waliojitokeza kufanya haki yao ya kidemokrasia, pia nawashukuru Tume ya Uchaguzi kwa umakini waliouonesha kuhakikisha tumefanya uchaguzi na kumaliza salama, kushindwa ndio kawaida ya ushindani.” Mtulia Maulid

Mkoani Kilimanjaro, NEC imemtangaza rasmi Dk Mollel kuwa mshindi wa uchaguzi katika jimbo la Siha baada ya kupata kura 25,611 huku akiwaacha mbali wapinzani wake, Elvis Mosi wa Chadema, Elvis Mosi aliyepata kura 5,905 na mgombea wa CUF, Tumsifueli Mwanri aliyepata kura 274 huku Mdoe Azaria wa Sau akiambulia kura 170.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARY 18, 2018 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS




Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz tu-follow instagram @jambotz. YouTube channel @jambotz.

WAZIRI NCHEMBA AAGIZA WAKIMBIZI WA BURUNDI 32,000 KURUDISHWA KWAO

Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba amewaagiza UNHCR kuwaondoa wakimbizi 32,000 ambao wameomba kwa hiari yao kurudi katika nchi yao ya Burundi haraka tofauti na wanavyofanya sasa.

Waziri Dr Mwigulu ameyasema hayo wilayani Ngara alipotembelea kituo cha mapokezi ya wakimbizi cha Lumasi kujionea shughuli zinazoendela katika vituo vya mapokezi ya wakimbizi ambavyo serikaki ikishaagiza vifungwe mala moja.

Dr Mwigulu amesema shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR wao wanafanya kazi masaa 24 katika kuwapokea wakimbizi kuingia nchini lakini wanakuwa wazito pale wakimbizi wenyewe wanapotaka kwa hiari yao kurudi kwao baada ya kujiridhisha kuwa kuna amani nchini kwao.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...