Sunday, October 20, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 20, 2013

.

.

KENYATTA ARUHUSIWA KUTOHUDHURIA BAADHI YA VIKAO VYA KESI


017113680_35400_1b04e.jpg
Mahakama ya ICC jana Ijumaa(18.10.2013)ilimruhusu kwa kiasi fulani Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi dhidi yake, ili kumpa muda wa kushughulikia majukumu ya kisiasa.
Kenyatta , ambaye alichaguliwa kuwa rais mwezi Machi mwaka huu, amekuwa akidai kwa muda mrefu sasa kuwa kesi hiyo mjini The Hague itazuwia uwezo wake wa kuiongoza nchi.
"Mahakama hiyo kimsingi inamuondolea Uhuru Kenyatta ulazima wa kuwapo wakati wote katika kesi dhidi yake inayoanza Novemba 12, imesema mahakama hiyo ya ICC katika taarifa, lakini ikasisitiza kuwa ni lazima afike kwa ajili ya ufunguzi wa kesi hiyo.
Majaji wamesema kuwa ruhusa ya Kenyatta inatolewa kwa misingi kwamba anaweze kutimiza majukumu aliyonayo kama rais wa Kenya, na sio kwasababu ya kutoa hadhi kwa kazi yake kama rais.
Atakuwapo wakati wa kutoa ushahidi
Mahakama hiyo iliyoko nchini Uholanzi pia inasisitiza kuwa Kenyatta anapaswa kuwapo wakati pande zote zitakapokuwa zinatoa taarifa zao za mwisho katika kesi hiyo, wakati wahanga wanatoa ushahidi wao na pia,iwapo kutakuwa na haja wakati wa kikao cha kutoa hukumu.

MSHAHARA WA RAIS KAA LA MOTO


jk 17ab9
Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe kutaja hadharani mishahara ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, serikali imekataa kuizungumzia mishahara hiyo.
Msimamo wa Serikali kutotaja mishahara ya viongozi wakuu unatofautiana na utamaduni wa nchi nyingine kama Marekani, Afrika Kusini, Ufaransa na Kenya ambazo mishahara ya wakuu wake huwekwa wazi kwa umma.
Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema akiwa wilayani Igunga Mkoani Tabora, alisema Rais Kikwete anapokea zaidi ya Sh30 milioni kwa mwezi (sawa na Sh360 milioni kwa mwaka) ikiwa ni marupuru na mshahara kwa mwezi bila kodi, huku Pinda akipokea Sh 26 milioni kwa mwezi.
Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema kiongozi yeyote haruhusiwi kutaja mshahara wa mtu mwingine kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya utumishi wa umma.
"Kuutaja mshahara wa mtu mwingine ni kinyume cha sheria na kosa, siyo utaratibu. Kwani wewe upo tayari watu waujue mshahara wako?" alihoji.

MATOKEO YA LIGI KUU YA UINGEREZA

2816039_orig_51785.jpg
Source: bongostaz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...