Thursday, April 19, 2018

BABU SEYA NA WANAE WATINGA BUNGENI LEO

Mwanamuziki nguli wa dansi, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na watoto wake ambao ni Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ na Francis Nguza, leo Aprili 19, 2018 wametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma baada ya kualikwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mariam Ditopile.

Babu Seya na familia yake, walishangiliwa na Bunge zima baada ya kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika bungeni humo.

Wanamuziki hao walikuwa ni miongoni mwa wafungwa 8,157 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanganyika, Desemba 9, 2017 zilizofanyika mjini Dodoma.

MSUKUMA 'LEMA SASA HIVI KIDOGO AMEKUWA BINADAMU'

Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma, amemuomba Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, kupeleka bungeni muswada  kubadilisha sheria ili makosa ambayo hayastahili mtu kufungwa apewe adhabu ndogo ili kuondoa msongamano katika magereza.

Pia mbunge huyo aliwataka baadhi ya wabunge waache kupiga kelele bungeni juu ya matukio ya watu kupotea na kutekwa, badala yake waviache vyombo vya sheria na vya usalama vifanye kazi yake.

Hayo ameyasema Bungeni wakati akichangia hoja katika Wizara ya Katiba na Sheria jana, Aprili 18, 2018.

PICHA ZA HARUSI YA ALIKIBA ILIYOFANYIKA MOMBASA



 Baada ya ukimya na usiri wa muda mrefu kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi hatimae leo April 19, 2018 Ali kiba amefunga ndoa katika msikiti wa Ummul Kulthum Mombasa nchini Kenya akiwa ameozeshwa na sheikh Mohammed Kagera.


Alikiba  amemuoa Amina Khalef Ahmed mkazi wa Mombasa ambapo ndipo sherehe za harusi hiyo zinafanyika hii leo huku sherehe nyingine kubwa ikitarajiwa kufanyika April 29, 2018 jijini Dar es Salaam.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...