Monday, June 10, 2013

TCRA IMEITAKA STAR TV IRUDISHWE KWENYE STAR TIMES KABLA YA SAA KUMI JIONI LEO.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma akitoa maamuzi kuhusu kujitoa kwa StarTV kwenye Star Times.

TCRA imeagiza Chaneli ya Star Tv irudishwe mara moja kwenye Star Times kabla ya saa kumi jioni leo.

Aidha Star Times na Star TV wameelezwa kuwa wote wamevunja sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010 na Kanuni zake na kutakuwa kujitetea tarehe 17 Juni 2013.

Agizo la kurudishwa kwa Chaneli ya Star TV linatakiwa kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa wananchi hawanyimwi haki ya kupata habari.

Vile vile wote wametakiwa kufuata Sheria inapotokea kutokuafikiana badala ya kutoa maamuzi bila kumshirikisha Mdhibiti (TCRA)

MSANII WA BONGO MOVIE KASH AFARIKI DUNIA LEO

Marehemu Jaji Khamisi (Kashi)

Habari iliyotufikia hivi punde ni kwamba msanii wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi)aliyewahi kutamba na michezo ya ITV enzi zile akiwa na wasanii kama mzee Masinde,Samson na wengine katika mchezo wa Tamu chungu na mingine mingi Amefariki dunia mchana huu katika hosptali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa,akizungumza na rais wa shirikisho la wasanii amesema kuwa tasnia yake bado inaendelea kukumbwa na majanga  lakini amedai yote ni kazi ya mungu
Nae mzee Masinde ambaye alikuwa nae katika kundi moja akiwa kama kiongozi wake amesema kashi ni msanii ambaye alikuwa mpiganaji na kwa hakika ni pigo kubwa katika tasnia yetu
Mungu ailaze roho ya marehemu Jaji Khamis (Kashi) mahali pema pepponi Amini.

Source:thesuperstarstz

HII NDIO VITA KATI YA STAR TIMES NA STAR TV


 Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki Kituo cha Televisheni cha Star, imeingia katika mgogoro na Kampuni ya Ving’amuzi ya Startimes na kufikia uamuzi wa kuitoa kurusha matangazo ya televisheni ya kituo hicho.

Hatua hiyo ya Kampuni ya Startimes kuondoa Star Tv kwenye orodha ya vituo vinavyopatikana kwenye king’amuzi chake ilianza juzi.


Startimes ilianza kutoa taarifa kuwa kutokana na matakwa ya Star Tv, wameamua kuitoa kwenye orodha ya chaneli zao bila ya ufafanuzi wa kina kuhusu uamuzi huo.
Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, alipotafutwa kutolea ufafanuzi wa kitendo hicho, alisema hafahamu lolote.
“Sifahamu kwani niko Pemba lakini labda watafute Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (Mkurugenzi wa TCRA) watakuwa wanajua,” alisema Profesa Mbarawa.

Taifa Stars yawasili leo ikitokea Morocco, Poulsen asema Refa aliuharibu mchezo wetu.

IMG_5878
 Wachezaji wa Taifa Stars wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Jumatatu alfajiri wakitokea Morocco.
IMG_5874
IMG_5825
-Asema adhabu ya kadi nyekundu haikuwa na ulazima
-Asema wangecheza 11 ushindi ulikuwa wazi
Kocha wa Timu bali matokeo ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema refa wa mechi ya Taifa Stars na Morocco iliyopigwa Marrakech Jumamosi kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la  Dunia Brazil mwakani aliuwa mchezo kwa kutoa kadi nyekundu kwa mchezaji Aggrey Morris.

MJUE MSANII WA BONGO MOVIE ALIEANZA KUCHEZA FILAMU ULAYA


Lucy Francis Komba (amezaliwa tar. 24 Oktoba, 1980) ni mwigizaji wa filamu, mwongozaji na mtayarishaji kutoka nchini Tanzania. Huenda akawa anafahamika zaidi kwa kutayarisha filamu ya Yolanda 1-2 na Utata. Lucy pia ni mmoja kati ya waliokuwa waigizaji wa kundi la sanaa la Kaole Sanaa Group.

Maisha ya awali


Lucy Francis Komba alizaliwa mnamo tarehe 24 Oktoba ya mwaka wa 1980, katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Alipata elimu yake ya awali (chekechea) katika shule ya St. Peters Nusery School na msingi alisoma katika shule ya Oysterbay Primary School. Elimu ya sekondari alisoma Moshi katika mkoa wa Kilimanjaro, kwa kidato cha 1 - 4 na 5 - 6 alisoma katika shule ya Kibosho Secondary School.
Kwa elimu ya vyuo, alisoma katika Chuo cha Utumishi wa Serikali na alisomea maswala ya IT (Information Technology) na alipata Diploma katika elimu hiyo.
Sanaa ya awali
Lucy Komba alianza maswala ya sanaa katika kundi la sanaa la Fukuto Arts Professional. Akiwa huko alishiriki katika baadhi ya mifululizo ya vipindi vya televisheni kama vile "Valentine Day" na "Rangi ya Chungwa".
Baada ya hapo akaelekea zake katika kikundi cha Dar Talent, akiwa huko alipata kushiriki katika filamu moja ya vichekesho. Baada ya hapo alilekea zake katika kikundi cha sanaa cha Kaole Sanaa Group, akiwa huko alipata kushiriki katika mifululizo minne ya vipindi vya televisheni (tamthilia).
[hariri]Kazi binafsi

JK kuteta na Wabunge, Mawaziri Dodoma.

Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili mjini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine atakutana na Kamati ya Bunge ya Bajeti ikiwa siku chache kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali itakayoainisha Mapato na Matumizi yake kwa mwaka wa fedha 2013/14, Juni 13.


Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge imekuwa na vikao karibu kila siku, wakati mwingine vikimalizika usiku ili ikijiweka sawa kabla ya


 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na vyombo vya habari siku za hivi karibuni
kuwasilishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa Rais Kikwete akiwa mjini Dodoma atakutana na baraza lake la mawaziri na Kamati ya Bajeti ili kupata picha ya mwelekeo wa bajeti, ambayo sehemu kubwa imeelezwa kubanwa na upatikanaji wa fedha za kutosha kwa ajili ya kuziwezesha wizara na taasisi zake kwa shughuli za kawaida na maendeleo.
Hata hivyo, habari zinadai kuwa ugumu uliopo ni namna ya kupata fedha kwa asilimia 100 kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo na matumizi ya kawaida kwa wizara na Idara za Serikali.

Chanzo chetu kilieleza kuwa pamoja na 'kukuna kichwa' jinsi ya kupata fedha hizo, hata utekelezaji wa bajeti ya 2011/12 na 2012/13, ulikuwa mgumu kwa kuwa baadhi ya wizara na
taasisi zake zilipata nusu ya bajeti iliyopitishwa au asilimia 30 ya bajeti nzima.

Upatikanaji wa fedha hizo chini ya asilimia unatarajiwa kwa wizara na taasisi zake huku ikielezwa kuwa ni kutokana na kumegwa kwa asilimia za mafungu kulikosababishwa na kuongezeka kwa matumizi ya Serikali zikiwemo dharura.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AANZA KUTEKELEZA AHADI ZAKE KWA VITENDO

1
Na Gladness Muushi wa Fullshangwe-Meru
Chama cha mapinduzi Wilaya ya Meru kimefanikiwa kutoa   Kiasi cha
Shilingi Milioni sita  pamoja na ahadi ya Milioni nane ikiwa ni ahadi
ya Katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman  Kinana aliyotoa mwaka jana
kwa ajili ya maendeleo ya vijana na wanawake wa Wilaya hiyo ingawaje
inatawaliwa na wapinzani
 Akikabidhi fedha hizo  mapema jana  katika uzinduzi  wa mashina ya
wakereketwa wa ccm   mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa arusha John
Pallangyo alisema kuwa fedha hizo ni moja ya ahadi zilizotolewa na
katibu mkuu wa ccm taifa Abdulrhaman Kinana mara alipofanya ziara ya
kujitambulisha mwaka  jana
Alisema kuwa mara baada ya katibu huyo kufanya ziara wilayani humo
aliamua kuwaunga mkono  vijana wa bodaboda  na wanawake wajasiramali
wa wilaya hiyo mkono ili waweze kujiendeleza kiuchumi ili waweze
kujikwamua katika hali ngumu ya kimaisha.
Aliongeza kuwa kwa kuwa ajira ni sehemu ya ilani ya chama cha
mapinduzi wameamua kutekeleza ahadi hiyo ili kuhakikisha kuwa vikundi
hivyo vinajiendeleza na kuachana na hali ya kuwa tegemezi  kwa kuwa
kupitia fedha hizo wataweza kujipatia mitaji ya kujienedeleza.
“Katika kutekeleza ilani ya chama chetu cha mapinduzi ni lazima
kuhakikiasha kuwa ajira inakuwepo hasa kwa vijana hivyo naombeni fedha
hizi mzitumie kwa uangalifu ili ziweze kuwasaidia kujiajiri wenyewe na
pia zitawasaidia kuachana na makundi ya upotoshaji”alisema Pallangyo

Kwa upande wake katibu wa chama hicho wilaya ya meru Langaeli Akyoo
alitoa wito kwa vijana wote na wanawake wa uwt wilayani humo kutumia
vizuri mitaji waliyopewa na chama hicho na kuhakikisha kuwa fedha hizo
zinawabadilishia hali zao za maisha pamoja na familia zao.
Aidha akyoo akielezea kuhusiana na uzinduzi wa mashina ya wakereketwa
alisema kuwa ni mkakati wa wa chama hicho wa kuhamasisha wananchi wote
katika harakati zake za kurudisha jimbo lililoko chadema na
kulirudisha mikononi mwao
Hata hivyo katika uzinduzi huo  mashina   yaliyozinduliwa ni pamoja na
kilala,usa madukani,sabato,imbaseny madukani,mji mpya,njia ng’ombe
,kimandafu pamoja na Arudeco.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 10, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


1 8a11b

2 bd675

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...