Thursday, January 30, 2014

MKUU WA WILAYA AFUNGA KIWANDA CHA SUKARI

miwa e4424
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka amekifungia kwa muda usiojulika shughuli za uzalishaji, Kiwanada cha Sukari cha Mtibwa mpaka kiwanda hicho kitakapolipa madeni ya wafanyakazi na wakulima wa miwa.
Akitoa msimamo wa Serikali ya wilaya hiyo juu ya kukifungia kiwanda hicho mbele ya wafanyakzi na wakulima hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi za mtendaji wa kata ya Mtibwa wilayani hapa, Mtaka alisema, wamechukua uamuzi huo baada ya mabishano ya muda mrefu baina ya pande mbili kutofikia muafaka.
Mkuu huyo wa wilaya katika mabishano hayo ya muda mrefu juu ya madai ya wakulima na wafanyakazi alisema wanakidai Kiwanda cha Mtibwa zaidi ya Sh1.9 bilioni ambazo ni za mauzo ya miwa na mishahara ya wafanyakazi.
Mtaka alisema shughuli nyingine kiwandani hapo zitaendelea kama huduma ya afya, ulinzi na idara ya fedha ili kuwezesha makundi hayo kupata mafao yao mwishoni mwa wiki hii kama ilivyoahidiwa na uongozi wa kiwanda hicho.
Meneja mkuu Hamad Juma alisema, kiwanda hicho kilikwama kulipa madeni hayo kutokana na uingizwaji mwingi wa sukari nchini uliosababisha wao kukosa soko ingawa waliahidi kuanza kulipa mwezi huu. Chanzo: mwananchi

MAN UNITED YAKATAA MABILIONI KWA JANUZAJ

JANU eb4eb
HATUTAKI, na tena hatutaki hata kusikia. Na ikiwezekana msirudi tena. Ndivyo ambavyo mapovu yamewatoka mdomoni watu wa Manchester United baada ya PSG kurudi mezani juzi Jumapili na ofa ya kumtaka kinda wao mahiri, Adnan Januzaj.
PSG wamekuwa wakitokwa udenda kwa kinda huyo mwenye asili ya Albania aliyezaliwa Ubelgiji miaka 18 iliyopita na hawajali kama aliingia mkataba mpya wa kuichezea Man United mwishoni mwa msimu uliopita.
Hata hivyo, kocha David Moyes amekataa ofa hiyo ya PSG inayodhaniwa kuanzia Pauni 25 milioni na kuendelea huku wakisisitiza kwamba hawana mpango hata wa kukaa chini na kuzungumza na matajiri hao wa mafuta kutoka Paris.
Man United imempatia mkataba mrefu wa miaka mitano Januzaj Oktoba mwaka jana baada ya kugundulika kuwa huenda mchezaji huyo angekuwa huru na kuondoka Mei mwaka huu mara baada ya msimu kumalizika.

RAIS KIKWETE AMPIGA KIJEMBE RAGE

rage1 1d2f4
RAIS Jakaya Kikwete amemshangaa Mwenyekiti wa Simba SC ya jijini Dar es Salaam, Ismail Aden Rage kwa kuitisha mkutano wenye ajenda moja kwa ajili ya wanachama wa klabu hiyo. Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Simba Rage, alitangaza kuwepo kwa mkutano wa klabu hiyo Machi 23 na kueleza wazi kuwa kutakuwa na ajenda moja ya kujadili mapungufu ya Katiba.
Akizungumza mbele ya umati wa watu waliohudhuria mazishi ya Mbunge wa Chalinze, Saidi Bwanamdogo mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Kikwete ambaye alifika katika eneo la makaburi, alimuuliza Mwenyekiti huyo wa Simba kuhusiana na maandalizi ya mkutano huo.
"Ndugu yangu Rage mimi Mwenyekiti mwenzio, lakini sijawahi kuona mkutano wenye ajenda moja ndio kwanza huo wa kwako, yaani wewe kiboko, pamoja na makelele yote lakini umeweza kutuliza hali ya mambo mpaka leo umedumu kuwa mwenyekiti," alisikika Rais Kikwete akisema huku mamia ya waombolezaji wakicheka.
Akizungumzia kauli hiyo ya Rais Kikwete, Rage alisema ili kuwa kiongozi imara ndani ya klabu za Simba na Yanga, inakupasa kuwa na roho ngumu, kwani bila ya kufanya hivyo wanachama watakuwa wakikuchezea kila kukicha.
"Mheshimiwa Rais kuwa kiongozi ndani ya klabu hizi mbili kunahitaji umakini sana, kwani bila ya kufanya hivyo wewe utakuwa ni kiongozi wa kupelekwa kila siku na hatimaye unamaliza muda hakuna ulichokifanya ndani ya uongozi wako," alisema Rage. Chanzo: mtanzania

IKULU YAVUNJA UKIMYA KUHUSU "MAWAZIRI MIZIGO" ...!!!


kawambwa_2846f.jpg
SHUKURU KAWAMBWA
Dar es Salaam. Ikulu imetaka kufungwa kwa mjadala wa kuhusu kurudishwa kwa mawaziri wanaodaiwa kuwa ni mizigo kwenye Baraza la Mawaziri na badala imetaka waachwe wafanye kazi.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema kuendeleza mjadala huo ni kupoteza muda, kwani Rais Jakaya Kikwete alishamaliza kazi yake.

Rweyemamu alisema Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua mawaziri ambao wana wajibu wa kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake, hivyo si sahihi wateule hao kuitwa 'mizigo' kwani yeye (Rais) ameona wanafaa.
"Rais anapoteua watu anaangalia wanaofaa kumsaidia na si vinginevyo. Kwani lengo lake ni kuona nchi ina 'move forward' (inasonga mbele) kimaendeleo," alisema Rweyemamu. Alisema watu wanapaswa kukumbuka kuwa mtu anapoteuliwa kwenye uwaziri kuna suala la uwajibikaji: "Anatakiwa kutekeleza uwajibikaji wa pamoja. Sasa kumshambulia mtu binafsi na kumwita mzigo siyo sahihi."

Rweyemamu alisema mjadala huo kwa sasa umepitwa na wakati na kuwataka wananchi na wachambuzi kuwaacha mawaziri hao kuchapa kazi.
"Ni vizuri wananchi wakawapa nafasi mawaziri hawa ya kufanya kazi na baadaye kuwapima na kuwachambua kutokana na utendaji wao," alisema.
Chimbuko la majadala
Mjadala kuhusu suala hilo unatokana na Rais Kikwete kuwarejesha katika Baraza la Mawaziri baadhi ya mawaziri ambao walidaiwa kuwa ni mizigo kutokana na udhaifu katika utendaji wao.

NEC "DAFTARI LA WAPIGA KURA LITABORESHWA"

 
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva.PICHA|MAKTABA 
**********
Pamoja na kushindwa kutaja tarehe rasmi ya kuanza kuboresha daftari la kudumu la wapigakura, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema daftari hilo litaboreshwa kabla ya kuanza kwa upigaji wa kura ya maoni kwa ajili ya kupata Katiba Mpya. Upigaji wa kura hiyo utafanyika ndani ya siku 70 baada ya kumalizika kwa Bunge Maalumu la Katiba linalotarajiwa kuanza katikati ya mwezi ujao mjini Dodoma. Litafanyika kwa kati ya siku 70 na 90.

Nec imetoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa na wananchi kwamba tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, daftari hilo halijawahi kuboreshwa, jambo ambalo litasababisha upigaji wa kura kwa ajili ya kupata Katiba Mpya kutawaliwa na vurugu. Malalamiko hayo yanatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu waliotimiza umri wa kupiga kura lakini hawamo katika daftari hilo.
Pia waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura na wenye kasoro mbalimbali zinazowafanya wapoteze sifa.

HAYA HAPA MATOKEO YA MECHI ZA LIGI KUU YA UINGEREZA, USIKU WA JUMATANO

MAGAZETI YA LEO JANUARI 30, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...