Friday, July 12, 2013

NATASHA WA BONGO MOVIE.... "NAOLEWA KWA AJILI YA STAREHE ZA MAPENZI NA SI KWA AJILI YA KUZAA"


MWIGIZAJI mkongwe wa maigizo na filamu Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ ambaye pia ni mtangazaji wa Radio Times FM, anayetarajia kufunga ndoa kesho, amefunguka kuwa anaoelewa kwa ajili ya kustarehe na siyo kwenda kuzaa kama wengine wanavyofanya.


Akizungumza na mwandishi wetu, Natasha alisema kuwa katika maisha yake hakuna kitu anachokichukia kama kubeba mimba na umri alionao ndiyo kabisa hawezi kufanya hivyo bali atalea wajukuu tu.
 

“Kuolewa si lazima kuzaa, mimi nimeolewa kwa ajili ya ‘ku-relax’ na kufurahi maisha kwa mume wangu na si vinginevyo, wakati wa kuzaa umeshapita, namwachia Monalisa (mwanaye) sasa aendelee kuijaza dunia,” alisema Natasha.


Mwanamama huyo ambaye hivi karibuni alifanyiwa bonge la pati katika sherehe ya kuagwa ‘send-off’ katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar alisema kuwa anaiombea ndoa yake idumu miaka mingi, wafe wazikane.

IRENE UWOYA AFUNGUKA BAADA YA DIAMOND KUMLIPUA JANA ....!!!


Kuna saa najiuliza kwanin ukimwamin mtu ndio anageuka...kwanin ukiwa muwaz watu wanakuchukulia vbaya? Leo nimeumia sanaaa kuliko skuzote...sijaamini mtu niliye mwamini kumuona kama rafiki yangu anaweza kuongea shit kuhusu mim...au najiuliza siruhusiwi kuwa na rafik wa kiume? Lakin sa nyingine nakaa chin nasema God ...u know me better” alifunguka Uwoya.
Sababu kubwa iliyodaiwa kumfanya Diamond atembee na Uwoya ni kitendo cha muigizaji huyo kudaiwa kumponda mara kwa mara na alikuwa hampendi Diamond ambaye alikuwa anafikishiwa habari hizo na marafiki zake Irine.



Kama hukufanikiwa kusoma habari hiyo iliyoripotiwa na Globalpublishers basi isome hapa  
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
SIRI nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.
KISA KAMILI
Huku akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni mke wa ndoa wa mtu, kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa kilichomfanya kujiweka kwa muda kwa Uwoya.

TANZANIA YAMJIBU RAIS KAGAME....YADAI IPO TAYARI KWA LOLOTE NA AKITHUBUTU ITAMCHAPA KAMA MTOTO...!!!


SERIKALI ya Tanzania imeipa onyo kali nchi ya Rwanda ikiitaka isijaribu kuota ndoto za kuishambulia kijeshi, vinginevyo itajibu mapigo kwa nguvu zote na kuhakikisha kuwa imeichakaza.

Kauli hiyo ya kwanza nzito imetolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa kufuatia taarifa ya matamshi makali yanayodaiwa kutolewa na Rais Paul Kagame wa Rwanda, dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na kutishia kuishambulia Tanzania.


Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally, alisema ingawa Serikali ya Tanzania hadi sasa inajua haina ugomvi wowote na Rwanda, lakini amekiri kuwapo kwa kile alichokiita ‘kupishana lugha’ kwa Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame.


Mkumbwa alikiri Serikali ya Tanzania kunasa matamshi yanayodaiwa kutolewa na Rais Kagame katika moja ya hotuba zake aliyoitoa Juni 30, nchini kwake wakati akihutubia katika hafla moja ya vijana.

WAZIRI WA FEDHA AMESISITIZA TENA KUWA KILA MTANZANIA NI LAZIMA ALIPIE SH. 1000 KWA AJILI YA KADI YA SIMU YAKE


SERIKALI imesisitiza kuwa itatoza Sh 1,000 kwa kila kadi ya simu inayotumika lakini pia inaangalia utaratibu wa kufanya makato hayo kwa njia ambayo haitamuumiza mtumiaji wa simu.
Akizungumza jana jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa alisema kuwa kupitia tozo hizo wanatarajia kukusanya Sh bilioni 160 kwa mwaka.
“Kupitia wawakilishi wenu na sisi serikali kuwa sikivu, tulishauriwa na ikaonekana kwamba kuna uwezekano wa kupata chanzo kingine cha mapato kupitia kadi za simu”alisema.
Alisema katika mapendekezo yaliyokuwa yametolewa serikali ilishauriwa kutoza Sh 1,450 katika kila kadi ya simu lakini baada ya kukaa na kushauriana serikali iliona ni vyema ikatoza Sh 1,000 ili kila mwananchi aweze kumudu gharama ambapo kwa mwaka kila mmiliki wa kadi ya simu atatozwa sh 12,000.

AGNESS MASOGANGE AKILI KUKAMATWA AFRIKA KUSINI...!!!

Agnes Gerald ‘Masogange
HUKU skendo ya kunaswa akiwa na madawa ya kulevya ikiendelea kumtesa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ anatarajiwa kupandishwa kortini nchini Afrika Kusini leo kujibu shitaka ambalo mwenyewe hajaliweka wazi, Ijumaa linakupasha.


 
Dawa za kulevya lakini siyo walizokamatwa nazo akina Agnes na Melisa.
AWALI YA YOTE
Mwishoni mwa wiki iliyopita, habari ya mjini ilikuwa Masogange kanaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini.
Habari zilisambaa kwamba sanjari na Masogange, mwingine aliyenaswa naye ni mdogo wake (mtoto wa mama yake mdogo Agnes) aitwaye Melisa Edward.
Kwa mujibu wa habari hiyo ya mjini, wawili hao walinaswa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oriver Tambo uliopo Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania wakiwa na ‘mzigo’ wa kilo nyingi aina ya ‘crystal methamphetamine’ wenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 6.8!.

SERIKALI YATANGAZA KIMA CHA CHINI MISHAHARA YA KISEKTA

 
Serikali imetangaza viwango vipya vya chini vya mishahara kisekta ambavyo vinatofautiana kati ya sekta moja na nyingine ambavyo ni kuanzia Sh40,000 hadi Sh400,000 kwa mwezi kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema, watakaolipwa kima kidogo zaidi cha Sh40,000 ni wafanyakazi wa nyumbani ambao wameajiriwa na watu wa kawaida huku wakiishi kwenye nyumba za waajiri wao.

 Kwa upande mwingine, katika viwango hivyo, kima kikubwa katika viwango hivyo cha Sh400,000 kitalipwa kwa wafanyakazi wa sekta za mawasiliano zikiwamo kampuni za simu, kampuni za kimataifa za nishati, madini na taasisi za fedha. 

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 12, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

LWAKATARE WA CHADEMA ALAZWA MUHIMBILI....!!!




Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, jana, kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya Shingo
*********
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na matatizo ya shingo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwenye wodi ya uchunguzi ya Sewahaji, Lwakatare alisema kuwa anakabiliwa na matatizo ya pingili za shingo na jopo la madaktari linakutana leo kuamua kama afanyiwe upasuaji ama la.
“Nilifanyiwa uchunguzi kwa x-ray na madaktari walisema hakuna jinsi zaidi ya upasuaji na kesho (leo) jopo la madaktari linasoma picha za x-ray kuamua aina ya upasuaji...nimegundulika kuharibika pingili ya sita na saba.

POLISI YA TZ YAKIRI KUWA WASICHANA WALIO KAMATWA SOUTH AFRICA NA MADAWA YAKULEVYA WALIPITA JULIAS NYERERE AIRPORT

JK-Airport 

Ni takribani siku sita sasa toka wasichana wawili raia wa Tanzania Agnes Gerald na Melisa Edward kukamatwa katika uwanja wa ndege wa OR Tambo Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya zaidi ya billion 6 za Tanzania.

Swala linalozua maswali mengi ni jinsi gani wasichana hao waliweza kupita katika uwanja wa ndege Julius Nyerere na karibia kilo 150 za dawa hizo za kulevya, kiasi ambacho Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini imesema ndio mzigo mkubwa zaidi wa dawa za kulevya kuwahi kukamatwa katika mipaka yote ya nchi hiyo kama mzigo mmoja (kwa lugha nyingine imevunja rekodi).

Idara ya polisi nchini Tanzania imekiri kuwa Agnes na Melisa walipitia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, na walisafiri na ndege ya shirika la ndege la South African Airways inayomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...