Ni takribani siku sita sasa toka wasichana wawili raia wa Tanzania
Agnes Gerald na Melisa Edward kukamatwa katika uwanja wa ndege wa OR
Tambo Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakituhumiwa kusafirisha dawa za
kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya zaidi ya
billion 6 za Tanzania.
Aliendelea kusema Dawa hizo zilisafirishwa kama mizigo mingine inayokaa sehemu za mizigo ndani ya ndege kwani uzoefu unaonyesha kwamba kwa namna yoyote ile abiria hawezi kuruhusiwa kwenda kukaa na mzigo wake ndani ya ndege unaofikia kilo 150.
Swala
linalozua maswali mengi ni jinsi gani wasichana hao waliweza kupita
katika uwanja wa ndege Julius Nyerere na karibia kilo 150 za dawa hizo
za kulevya, kiasi ambacho Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini imesema
ndio mzigo mkubwa zaidi wa dawa za kulevya kuwahi kukamatwa katika
mipaka yote ya nchi hiyo kama mzigo mmoja (kwa lugha nyingine imevunja
rekodi).
Idara ya polisi nchini Tanzania imekiri kuwa Agnes na Melisa walipitia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, na walisafiri na ndege ya shirika la ndege la South African Airways inayomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini.
Idara ya polisi nchini Tanzania imekiri kuwa Agnes na Melisa walipitia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, na walisafiri na ndege ya shirika la ndege la South African Airways inayomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini.
Kamanda
wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey
Nzowa akiongea na NIPASHE jana (June 10) waliotaka kujua wasichana hao
walipitia uwanja gani wa ndege na kama walikaguliwa. Alikiri kuwa
wasichana hao walikaguliwa kama abiria wengine, lakini akadai kwamba si
jukumu la Jeshi la Polisi kufanya ukaguzi kwenye viwanja vya ndege, na
kuongeza kuwa ni jambo la kawaida mtu kukamatwa nchi nyingine na dawa
za kulevya wakati katika nchi aliyoanzia safari hajakamatwa kwani
inategemea utalaamu wa watu wenyewe wanaokagua.
“Kila
mtu anapopita uwanja wa ndege anakaguliwa na kama ana kitu ambacho ni
kibaya ndipo anakamatwa, hawa wasichana walikaguliwa maana huwezi
kupita uwanja wa ndege bila kukaguliwa,” Alisema.
Kamanda
Nzowa aliongeza kuwa watu wa uwanja wa ndege ni lazima wawe na mtu au
mkaguzi ambaye ni mtaalamu sana wa kutambua dawa za kulevya kwa kuwa
ziko za aina nyingi na mbinu nyingi zinatumika kuzisafirisha.
“Utakumbuka
Juni 23 mwaka 2010 nilikamata mabalozi wawili, hawa watu walitoka
Brazil wakaenda Afrika Kusini, lakini tukawakamatia hapa Tanzania,”
alisema Nzowa
Kamanda Nzowa alisema uchunguzi unaendelea kumbaini mmiliki wa dawa hizo na kuna dalili za kuwabaini wahusika hao.
Aliendelea kusema Dawa hizo zilisafirishwa kama mizigo mingine inayokaa sehemu za mizigo ndani ya ndege kwani uzoefu unaonyesha kwamba kwa namna yoyote ile abiria hawezi kuruhusiwa kwenda kukaa na mzigo wake ndani ya ndege unaofikia kilo 150.
Aliongeza
kuwa Katika hali ya kawaida, hata kama wasichana hao wangeamua
kugawana dawa hizo kwa usawa, kila mmoja angebeba kilo 75, kiasi
ambacho hata hivyo abiria haruhusiwi kupanda nacho kama mzigo wa
mkononi, wala mzigo ambao haulipiwi.
Taarifa
kuhusiana na kukamatwa kwa wasichana Agnes Gerald (25) na Melisa (24)
wakiwa na mzigo mkubwa wa dawa za kulevya wenye thamani ya zaidi ya
billion 6 kumezua maswali mengi ikiwa ni pamoja na hofu kubwa kutokana
na ongezeko kubwa la watanzania wanaozidi kukamatwa wakitaka
kusafirisha au kuingiza dawa hizo nchini.
Hivi
karibuni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika taarifa yake ilisomwa kwa
niaba yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Bunge), William Lukuvi, mjini Dodoma, katika maadhimisho ya kitaifa ya
‘Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani’ alisema tatizo la dawa
hizo ni janga la kitaifa hivi sasa nchini.
Alisema
kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara
haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita Watanzania 240 walikamatwa katika
nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, kuharibu taswira ya nchi na
kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu
wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.
Mwezi huu (July) pekee watanzania watano wamekamatwa wakisafirisha dawa za kulevya zenye thamani ya shilingi billion 9.
Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa Agnes Gerald na Melisa Edward wameshafunguliwa mashitaka nchini Afrika Kusini.
SOURCE: NIPASHE
No comments:
Post a Comment