Agnes Gerald ‘Masogange
HUKU
skendo ya kunaswa akiwa na madawa ya kulevya ikiendelea kumtesa kwenye
mitandao mbalimbali ya kijamii, Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald
‘Masogange’ anatarajiwa kupandishwa kortini nchini Afrika Kusini leo
kujibu shitaka ambalo mwenyewe hajaliweka wazi, Ijumaa linakupasha.
Dawa za kulevya lakini siyo walizokamatwa nazo akina Agnes na Melisa.
AWALI YA YOTE
Mwishoni mwa wiki iliyopita, habari ya mjini ilikuwa Masogange kanaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini.
Habari
zilisambaa kwamba sanjari na Masogange, mwingine aliyenaswa naye ni
mdogo wake (mtoto wa mama yake mdogo Agnes) aitwaye Melisa Edward.
Melisa Edward aliyekamatwa na Agnes.
IJUMAA LAANZA KUSAKA UKWELI
Baada
ya kunasa habari hiyo, Ijumaa liliingia mzigoni kuusaka ukweli ambapo
hata hivyo, madai hayo yalikuwa yakijifungafunga sana.
Mtu mmoja wa karibu na Masogange alipoulizwa kuhusu ukweli au uongo wa habari hiyo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni
kweli Agnes amekamatwa akiwa na madawa ya kulevya kule Sauzi. Lakini si
yenye thamani hiyo ya bilioni sita bali ni milioni arobaini tu. Hata
hivyo, ameachiwa kwa dhamana ila paspoti yake imezuiliwa.
“Nadhani kuna mambo yanawekwa sawa ikiwezekana atarudi nyumbani.”
JIJINI DAR, KAMANDA WA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA ANENA
Jumatatu
iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya
Tanzania, Godfrey Nzowa aliviambia vyombo vya habari kuwa, Watanzania
wawili walikamatwa nchini Afrika Kusini na mamlaka ya mapato wakiwa na
madawa ya kulevya kutoka Tanzania yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Kamanda
Nzowa aliwataja Watanzania hao kuwa ni Agnes Gerald ambaye ana miaka 25
na Melisa Edward mwenye miaka 24. Alisema wawili hao baada ya kukamatwa
na chombo hicho walikabidhiwa kwa polisi ambapo mahojiano yanaendelea.
IJUMAA LAMWIBUKIA KAMANDA NZOWA
Baada
ya Kamanda Nzowa kuwataja kwa majina wawili hao Jumatatu iliyopita,
siku iliyofuata, Ijumaa lilipiga hodi kwenye ofisi za kamanda huyo kwa
lengo la kutaka kujua kama Agnes Gerald aliyemtaja jana yake ni Masogage
au majina yanafanana tu.
Kamanda
huyo hakuwepo ofisini kwake asubuhi hiyo na kwa mujibu wa wasaidizi
wake, alikuwa kwenye kikao cha dharura kwenye Ofisi za Polisi wa
Kimataifa ‘Interpol’.
APIGIWA SIMU
Ilibidi
Ijumaa limsake kwa njia ya simu ya kiganjani kwa mara kadhaa.
Alipopokea akaulizwa kuhusu Agnes Gerald aliyemtaja kama ni Masogange
yule staa.
Kamanda
Nzowa: “Eee, mimi siwezi kusema ni huyo, ninachojua ni Agnes Gerald tu
basi. Sasa kama ni Masogange mimi sifahamu lolote.”
JUMANNE USIKU SIMU KUTOKA SAUZI
Mpaka
hapo, timu nzima iliyokuwa ikifuatilia habari hiyo haikuona ukweli wa
Agnes Gerald kuwa ni Masogange na kwa vile siku zote Global Publishers
inasimamia utafiti kabla ya kuandika habari iliamua kuiweka pembeni
kwanza ili kuendelea kuichimba.
Saa
2:14 usiku wa siku hiyo, Ijumaa lilipokea simu yenye kuashiria wito
(code number) ni ya nje na kabla haijapokelewa, ilibainika ni ya Afrika
Kusini.
Ijumaa: Haloo.
Sauti: Haloo, mimi Masogange.
Ijumaa: Mambo Agnes, pole sana na mkasa uliokupata bwana, pole sana.
Agnes:
Kwanza naumizwa sana na maneno ambayo watu wanazidi kuyaeneza sehemu
mbalimbali bila kuwa na uhakika wowote, mimi sikukamatwa kwa sababu ya
madawa ya kulevya.
“Mkasa nilioupata siyo ambao watu wanaueneza kwenye mitandao mbalimbali na katika vyombo ya habari.”
Ijumaa: Kwa hiyo madai ya kukutwa na madawa ya kulevya si ya kweli?
Agnes: Kweli nilikamatwa huku kwa matatizo f’lan ila siyo ishu ya madawa kama watu wanavyosambaza.
Ijumaa: Ni tatizo gani sasa?
Agnes:
Unajua sipendi tena kuwapa watu faida ila lilikuwa ni tatizo la
kawaida, nilikamatwa na baada ya hapo nilitoka na niko huru. Nasubiri tu
kwenda mahakamani Ijumaa (leo) mara moja kisha n’tarudi Bongo.
Ijumaa: Mh! Sasa Egg, mbona huku mpaka viongozi wa polisi wamesema ni madawa?
Agnes: Hapana, siyo, ipo ishu ndogo tu.
Ijumaa: Haya pole sana kwa misukosuko.
Agnes: Asante sana, nitakuja huko siku si nyingi.
CHANZO GLOBAL PUBLISHER
No comments:
Post a Comment