Thursday, April 04, 2013

PICHA ZA RAMANI YA UJENZI WA UWANJA WA YANGA, HIVI NDIVYO UTAVYOKUA


Ramani ya uwanja mpya wa klabu ya Yanga - Kaunda Stadium unavyoekana kwa ndani
 

 Kampuni ya Beinjing Construction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi akinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) leo imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya eneo la Jangwani.
Kaimu meneja wa kampuni ya BCEG Zhang Chengwei David amesema upembuzi akinifu umekamilika kuhusiana na suala la ujenzi wa uwanja wa mpya wa klabu ya Yanga eneo la jangwani ambapo taratibu za makadirio na michoro imekamilika tayari na leo kuwasilishwa kwa uongozi wa klabu ya Yanga.

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE YATOA UFAFANUZI KUHUSU UWANJA WA SONGWE KUITWA JAKAYA KIKWETE

MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI BW. SULEIMAN SULEIMAN AKIZUNGUMZIA UGUMU WA KUBADILISHA JINA LA SONGWE KUITWA JAKAYA KIKWETE




MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE BW.SULEIMAN SULEIMAN AKIFAFANUA KWA WAANDISHI WA HABARI JUU YA UTARATIBU WA JINA LA VIWANJA VYA NDEGE VYA KIMATAIFA ULIVYO





CHEK PICHA ZA NDOA YA COMEDIAN KUPA ILIYOFANYIKA WEEKEND ILIYOPITA

13
 Weekend iliyopita comedian maarufu “Kupa” alifunga ndoa na mke wake ambapo sherehe yao ilihudhuriwa na wasanii wenzake kibao kutoka bongomovie unit. Cheki mpango mzima ulivyokuwa siku ya siku na wasanii walivyopendeza kwenye party hiyo. Short list ya wasanii waliofika kwenye party hiyo ambayo MC alikuwa Dr Cheni ni Ray,JB,Nisha,Irene Uwoya,Wolper na wengine wengi.

WEMA SEPETU AMSUPRISE MARTIN KADINDA KWA BOOOOOOONGE LA KEKI NA MSHIKO WA MAANA

ahahahhha a this woman is something Else.. baada ya kukurukakala zangu Wema sepetu  aliniita nyumbani kwake.... as soon as i got there nitwishwa boooooonge la keki... You i was like whaaat?


hakuishia hapo.... mkononi kashika nini hapo?? usisonye sasa... hahha

SHILOLE, Q-CHILLAH WAFUMWA LAIVU WAKIWA KATIKA MAHABA

Aibu hiyo ilitokea Machi 29, mwaka huu ambayo ilikuwa Ijumaa Kuu ambapo wasanii hao walikuwa wakitoka Dar kwenda Mwanza kwa ajili ya kufanya shoo siku ya Pasaka.
Akilisimulia gazeti hili, shuhuda wetu aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo (jina tunalo) alisema aliwaona Shilole na Q-Chillah wakiwa katika ‘malovee’ ambapo mara kwa mara walikuwa wakipigana mabusu kitendo kilichowafanya abiria wengine kuwakodolea macho yenye kuwashangaa.


Airtel, Samsung wakubaliana kukuza soka la vijana: Airtel Rising Stars Awamu ya tatu kuanza mwishoni mwa mwezi huu

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayofanya kazi pamoja na kampuni ya Samsung zimesaini makubaliano ya kushirikiana kudhamini mashindano makubwa Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17. 

Katika mkataba huo wa mamilioni ya dola, Samsung pia itakuwa mtoaji rasmi wa vifaa vya mawasiliano kwenye mpango huo wa mashindano maarufu kama Airtel Raising Star (ARS) unaoendeshwa na Airtel. 

Airtel inatoa huduma za mawasiliano kwa simu za mkononi kwenye nchi 20 barani Asia na Africa huku Samsung ikiwa ni miongoni mwa makampuni makubwa ya vifaa vya kisasa vya elektoniki.

Chadema wamtuhumu Mwakyembe kutoa zabuni kinyume cha sheria

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtuhumu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kwamba alitoa zabuni ya ujenzi wa bandari ya nchikavu kwa kampuni inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinyume cha sheria za ununuzi. Chadema walisema jana kwamba, kampuni hiyo ni Jitegemee Trading Company ambayo ilipewa zabuni ya ujenzi wa bandari katika Viwanja vya Sukita pasipokuwa na mchakato wa kushindanisha kampuni nyingine. 
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema: “Mwakyembe aseme alitoa zabuni hiyo kwa Jitegemee kwa kuzingatia vigezo gani? Kampuni ngapi zilishindanishwa katika mchakato huo na asipofanya hivyo hastahili kukaa wizarani hapo bali alipelekwa Segerea gerezani kwani ni kosa kubwa kutoa zabuni kinyemela.”
Hata hivyo, Dk Mwakyembe, ambaye yuko jimboni kwake Kyela mkoani Mbeya alipoulizwa kuhusu madai hayo alijibu na kukata simu; “Mimi nina kazi ya kuongoza wizara na wao Chadema wana kazi ya kuchonga mdomo, hivyo waache mimi niongoze Serikali.

MAUNO YA WOLPER YAWACHENGUA WATU UKUMBINI

  VIUNO alivyokatika  staa maarufu wa filamu, Jacqueline Wolper viliwachengua ile mbaya watu waliohudhuria harusi ya wasanii maarufu wa Bongo Movies, Jimmy Mafufu na Idrissa Makupa ‘Kupa’.Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Ukumbi wa Urafiki uliopo Ubungo, jijini Dar baada ya  wasanii kwenda mbele ya ukumbi kwa zamu na kuonyesha uhodari wa kuyarudi mangoma ambapo ilipofika zamu ya Wolper, alionekana kuwazidi wenzake kwa utundu wa kucheza.
Baada ya kuonesha vitu adimu ambavyo havikuoneshwa na staa yeyote kati ya waliomtangulia, wageni waalikwa walishangilia na kupiga makofi hadi aliporejea sehemu aliyokaa awali.

RAY ASALIMU AMRI JUU YA FILAMU YAKE INAYO SHUTUMIWA KUUDHALILISHA UKATOLIKI

 
Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.
HATIMA ya filamu ya mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’, Sister Mary iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji huyo amesalimu amri ya viongozi wa kanisa hilo.Kanisa Katoliki nchini linaloongozwa na Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa namna ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi.

Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu hiyo.
Akipiga stori na paparazi wetu, Ray amebainisha kuwa baada ya kuambiwa achomoe vipande vingi kwenye filamu hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani hata akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya wakati mwingine. “Asilimia 85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo walivyosema niviondoe, sina ujanja kwa sasa nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda nije kuirudia upya hapo baadaye,” alisema Ray.

WAJUE WASANII SITA (6) WA BONGO FLEVA WENYE KUHESHIMIKA SANA TANZANIA.

1.LADY JAY DEE
Mwanadada JIDE ama binti machozi ameweza kuongelewa sana kama msanii anayeheshimika sana tanzania kutokana na idadi kubwa ya watu walio hojiwa kumtaja yeye kama ndo mwana muziki mwenye kuheshimika sana tanzania kwa upande wa muziki wa kizazi kipya

2.PROF J
Prof J naye hakuwa nyuma katika kutajwa na idadi kubwa,Prof j kama muhasisi mkubwa wa huu muziki wa kizazi kipya anaheshimika sana kutokana na mchango wake mkubwa katika hii gemu bila ya kuwa na sifa mbaya zinazo weza kumchafulia heshima yake
3.FID, Q

Polisi Wavamia Nyumba Ya Diddy

Diddy

Polisi na Helikopta mbili za polisi walivamia Nyumba ya Diddy iliyopo Los Angelos Marekani Usiku wakuakia Leo . Lakini habari zilizotoka kwenye vyomba vya usalama viliimbia TMZ kuwa tukio hilo lilikuwa la bahati mbaya
Habari zilizotoka polisi ziliwaambia TMZ kuwa Kuna Mtu alipiga simu polisi kuwa ndani nyumba ya Diddy kuna mtu anarusha risasi.
Baadae polisi na wakubwa wengine walipojua kuwa ni mchezo mwingine unaofanyiwa wasani wakubwa marekani waliamukuondoka katika tuukio hilo.

TMZ wanasema kuwa waliambiwa kuwa Tukio hilo lilikuwa limepangiwa kufanyiwa kwa muigizajiSteve Carell ambapo nyumba yake ilikuwa imezungukwa na Polisi wengi kwasababu ilikuwa karibu na nyumba ya Diddy.
Hapa ndio nje kwa Diddy

Inasemekana Diddy sio staa wa kwanza kufanyiwa tukio hilo, kuna baadhi ya mastaa walishawahi kufanyiwa hivyo kama vile nyumbani kwa wazazi wa Miley Cyrus mwaka jana Walifanyiwa kitendo hicho hicho.
Polisi wamesema kuwa matukio hayo yakutishia ya mekuwa ya kudumu na sugu sasa wamesema watamshitaki kwa sheria kali kwa yeyote atakayefanya tena tukio kama hilo.

Mauaji ya Padri: DPP, Polisi wakorogana



Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, ametupilia mbali uchunguzi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na kusema mtuhumiwa hana kesi ya kujibu mahakamani.

Padri Mushi ambaye alikuwa Paroko wa Kanisa Katoliki Minara Miwili aliuawa kwa kupigwa risasi Febuari 17, mwaka huu katika eneo la Beitrasi mjini hapa akiwa ndani ya gari alipokuwa akielekea kuongoza misa ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Theresia, mjini Zanzibar.
Baada ya mauaji hayo, Rais Jakaya Kikwete alitoa kibali cha kukaribisha maafisa wa FBI kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa mauaji hayo na Machi 17, mwaka huu Jeshi la Polisi lilimkamata Omar Mussa Makame kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE APRIL 04, 2013

.
.
.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...