Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel inayofanya kazi pamoja na kampuni ya
Samsung zimesaini makubaliano ya kushirikiana kudhamini mashindano
makubwa Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17.
Katika
mkataba huo wa mamilioni ya dola, Samsung pia itakuwa mtoaji rasmi wa
vifaa vya mawasiliano kwenye mpango huo wa mashindano maarufu kama
Airtel Raising Star (ARS) unaoendeshwa na Airtel.
Airtel
inatoa huduma za mawasiliano kwa simu za mkononi kwenye nchi 20 barani
Asia na Africa huku Samsung ikiwa ni miongoni mwa makampuni makubwa ya
vifaa vya kisasa vya elektoniki.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam leo, Airtel imefanya
kazi kwa karibu sana na taasisi za elimu kwenye nchi 17 zinazozungumza
Kiingereza na Kifaransa ambapo kwa kupitia mashindano hayo ya soka ya
Airtel Rising Stars yamefanikiwa kushirikisha zaidi ya timu 18,000.
ambapo vijana wa kike na wa kiume wapatao 400,000 barani Afrika
walishiriki katika mashindano hayo ya Airtel Rising Star.
Mwaka
jana mashindano haya ya Airtel Rising Stars yalionekana kukua kwa
asiliamia 65 na kuna kila dalili kwa mwaka huu kukua zaidi,” inasomeka
sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Airtel Makao Makuu.
Mkakati
huo wa kukuza soka barani Afrika unaungwa mkono kwa dhati na klabu
kubwa za England; Arsenal FC na Manchester United ukiwa na lengo la
kuibua na kukuza vipaji vipya vya vijana wa Kiafrika. “ARS imefikia
kuwa chanzo kizuri cha wachezaji wapya wa timu za mataifa mbalimbali
huku pia wengine wakijiunga na klabu zinazoshiriki ligi kuu barani humu.
Afrika ina vijana wengi zaidi duniani.
Uwiano
wa vijana barani humu ni mkubwa kuliko mabara yote kwani takwimu
zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya Waafrika zaidi ya bilioni moja ni
vijana,” alisema George Ferreira, Makamu wa Rais wa Samsung Electronics,
Africa.
Akizungumzia
ushirikiano huo, Andre Beyers, Ofisa Masoko Mkuu wa Airtel Africa
alisema: "Ushirikiano huu utapanua wigo wa biashara na kuyawezesha
mashindano ya ARS kufikia malengo yake.”
Msimu
ujao wa Airtel Rising Stars ukiwa ni wa tatu tangu kuanzishwa kwake
utaanza mwishoni mwa mwezi huu. Moja kati ya matunda ya mashindano haya
ya Airtel ni Priscilla Okyere, binti aliyeibuka kutoka ARS na sasa ni
nahodha wa timu ya taifa ya wasichana chini ya miaka 17 ya Ghana.
Aliiongoza timu hiyo kunyakua medali ya fedha kwenye mashindano ya Dunia
ya FIFA Under-17 kwa wanawake mwaka jana huko Azerbaijan.
No comments:
Post a Comment