Saturday, September 06, 2014

MORSI ASHTAKIWA KWA KUTOA SIRI ZA MISRI

Mohammed Morsi akiwa Kizimbani

Kiongozi mkuu wa mashtaka nchini Misri amemfungulia mashtaka aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi kwa kupeleka stakhabadhi za siri kutoka idara ya usalama nchini Qatar.
Bwana Morsi amekuwa akizuiliwa jela tangu jeshi limuondoe madarakani mwaka uliopita wakati wa maandamano ya kumtaka ajiuzulu.
Tayari kiongozi huyo anakabiliwa na hukumu ya kifo katika mahakama nyengine tofauti.
Kundi la Muslim Brotherhood ambalo ni mwanachama wa maisha limepigwa marufuku na viongozi wake wengi huku wengine wakihukumiwa kifo.
Qatar imekuwa ikimuunga mkono Bwana Morsi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

DAMU YA WALIOPONA EBOLA KUTIBU UGONJWA HUO

Mkutano wa WHO kuhusu Ebola mjini Geneva.

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa damu ya watu ambao wameponea ugonjwa wa Ebola inaweza kutumiwa kuwauguza wagonjwa wengine.
Katika mkutano mjini Geneva, wataalam wa shirika hilo walikubaliana kwamba hii itakuwa njia ya haraka na ilio salama dhidi ya ugonjwa wa Ebola,sababu kuu ikiwa kwamba kinga ya mwili katika damu ya mtu aliyepona inaweza kukabiliana na virusi hivyo.
Wataalam hao pia wanataka matibabu mengine kuharakishwa ikiwemo dawa ya Zmapp pamoja na chanjo zengine mbili.
Idadi ya watu wanaodaiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola imepita elfu mbili.
Zaidi ya watu elfu nne wameambukizwa ugonjwa huo huku tiba yake ikiwa bado haijajulikana. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...