Friday, March 21, 2014

RAIS KIKWETE KUZINDUA SHUGHULI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO

Bunge la Tanzania mjini Dodoma
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kuzindua rasmi shughuli za bunge la kitaifa kuhusu marekebisho ya katiba mjini Dodoma katika hatua itakayoanzisha rasmi mjadala wa kitaifa kuhusu marekebisho hayo.
Bunge hilo maalum la katiba limepewa kati ya siku 70 hadi 90 kujadili rasimu ya katiba na kisha kuifanyia marekebisho kabla ya kura ya maamuzi.
Kuna ripoti kwamba baadhi ya wajumbe kutoka upinzani na mashirika ya kiraia yanapanga kuvuruga shughuli hiyo ya uzinduzi.
Suala la hotuba ya Rais Kikwete limekuwa sehemu ya mjadala katika Bunge hilo kutokana na baadhi ya wajumbe kuhoji sababu za Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu kabla ya Rais kuzindua Bunge kwa mujibu wa kanuni.
Mjadala huo uliwafanya baadhi ya wajumbe kumzuia Jaji Warioba Jumatatu iliyopita kuwasilisha rasimu hiyo kama ilivyokuwa imepangwa.
Kikao cha maridhiano kilifanyika siku hiyohiyo usiku na kufikia mwafaka kwamba Mwenyekiti huyo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba awasilishe Rasimu ndiposa Rais aweze kuzindua shughuli ya kujadili rasimu hiyo kabla ya kura ya maoni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

SHUGHULI ZA KUISAKA NDEGE YA MALAYSIA ZAENDELEA

Picha za kinachodhaniwa kuwa mabaki ya ndege ya Malaysia nchini Australia
Ndege na meli kutoka nchi mbali mbali zinaendelea kuitafuta mabaki ambayo huenda yanatokana na ndege ya Malaysia iliyopotea takriban wiki mbili zilizopita ikiwa imebeba takriban watu 240.
Matumaini ya kutatua kitendawili hicho yaliongezeka baada ya Australia kutoa picha za Satelaiti za vitu viwili vilivyoonekana baharini vuikidhaniwa kuwa vifusi vya ndege hiyo.
Hata hivyo hadi kufikia sasa hakuna cha maana kilichopatikana.
Afisa mmoja mkuu wa New Zealand amesema operesheni hiyo ilitatizwa na kuchafuka kwa bahari na kutoona vizuri.
Meli ya mizigo ya Norway ilitumia taa kuyatafuta mabaki hayo pasina kufanikiwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

WARUSI ZAIDI WAWEKEWA VIKWAZO NA EU

Viongozi kutoka mataifa ya Jumuiya ya Ulaya wanaokutana mjini Brussels kuimarisha vikwazo wanavyowekea Urusi,wameamua kuongeza idadi ya Warusi wanaopaswa kuwekewa vikwazo kibinafsi.
Orodha ya awali ya 21 sasa imeongezewa watu wengine 12.
Viongozi hao wa Jumuiya ya Ulaya pia wametoa wito kwa Tume inayosimamia jumuiya hiyo iwe tayari kuimarisha vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya Urusi iwapo hali hiyo ya sintofahamu itaendelea.
Kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema kuwa wale ambao majina yao yameongezwa kwa orodha ya hapo awali hawataruhusiwa kutembelea Ulaya na mali yao itapigwa tanji kama ilivyofanyika kwa maafisa 21 wa Urusi na Ukraine mapema juma hili.
Bi Merkel pia alisema kuwa Jumuiya ya Ulaya iko tayari kuunga mkono Serikali mpya ya Ukraine kifedha, bora tu iafikiane na Hazina ya Fedha duniani (IMF). 
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema hatua muhimu zimechukuliwa kufikia sasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 21, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

SAUDI ARABIA YAPIGA MARUFKU KUWAPA WATOTO MAJINA HAYA......!!!

Screen Shot 2014-03-21 at 5.23.39 AM
Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia imepiga marufuku majina hamsini ambayo yapo kinyume na tamaduni pamoja na dini ambapo kuanzia sasa, wazazi kutoka falme hiyo hawataruhusiwa tena kuwapa watoto wao.
Majina hayo ni kama Linda, Alice, Elaine au Binyamin (jina lenye maana Benjamin) ambapo jina la Benjamin (Binyamin) kwa dini ya kiislamu linaaminika kuwa jina la mtoto wa mtume Jacob, yaani Yacoub kwa dini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 
Mengine katika orodha hiyo ambayo hayatoruhusiwa ni kwa sababu yanaaminika kuwa yenye kufuru, yasiyo ya kiarabu na yasio ya kiislamu au yenye kupingana na tamaduni na dini ya falme hiyo.
Sababu nyingine ni ya kigeni ama ya ughaibuni yakiwemo yenye maana ya ufalme au ukubwa, cheo flani kama Sumuw (mtukufu), Malek (mfalme) na Malika (Malkia).
Screen Shot 2014-03-21 at 5.23.23 AM
Majina mengine hayapo katika jamii hizi hivyo hakuna sababu zilizotolewa juu yake, hii ni sehemu nyingine ya orodha yenyewe ambapo ni Malaak (angel), Abdul Aati, Abdul Naser, Abdul Musleh, Binyamin (Arabic for Benjamin) Naris, Yara, Sitav.
Mengine ni Loland, Tilaj, Barrah, Abdul Nabi, Abdul Rasool, Sumuw (highness), Al Mamlaka (the kingdom), Malika (queen), Mamlaka (kingdom), Tabarak (blessed), Nardeen, Sandy, Rama (Hindu god), Maline, Elaine, Inar, Maliktina
Maya. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...