Thursday, August 21, 2014

ANGALIA PICHA ZA NYUMBA YA JUSTIN BIEBER YENYE NIGHT CLUB, GYM NA MOVIE THEATER

Hivi sasa Justin Bieber anaweza kujiachia kwenye club bila kupigwa picha na mapaparazi kwa sababu nyumba yake mpya ina night club na bar tatu ndani yake.
Japokuwa pesa alizolipa Bieber kumiliki nyumba hii haijawekwa wazi, sifa zake ni kuwa na ukubwa wa square meter 16,000, vyumba vya kulala 10, gym kubwa, bwawa la kuogelea, movie theater yenye screen ya inch 160 na vitu vingine.
Justin Bieber ameshahama kwenye nyumba aliyokuwa amepanga na kuhamia kwenye nyumba hii mpya aliyonunua. Hizi ni picha 10 zikionyesha nyumba hiyo

0 1
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

HII NDIO STORY MPYA KUHUSU NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA

mala
Mwanamke mmoja mwenye cheo cha juu katika bank kubwa iliyopo Kuala Lumpur Malaysia pamoja na mumewe wameshtakiwa kwa kuiba pesa kutoka katika account za abiria na wafanyakazi wa ndege ya Malaysia iliyopotea kwenye bahari ya Hindi.
Pamoja na kushtakiwa huko mtu na mkewe hao waliepuka makosa mengine 16 kati ya makosa hayo yamo wizi,kukaidi amri ya mahakama na makosa mengineyo.
Ofisa huyo Nur Shila Kanan anatuhumiwa kutumia cheo chake vibaya katika benki ya HSBC nchini Malaysia kwa kuiba pesa za abiria walipotea na ndege.
Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama moja mjini Kuala Lumpur,Malaysia kwamba wawili hao walifanikiwa kukwapua dola za kimarekani elfu thelathini kutoka katika account tatu tofauti za abiria waliopotea na account moja ni ya mfanyakazi wa shirika hilo la Malaysia airline. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS AGOSTI 21, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MWINYI: SERIKALI HAIKUFUTA AZIMIO LA ARUSHA

Rais wa mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi
Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi amesema serikali haijawahi kufuta Azimio la Arusha kama inavyodaiwa na baadhi ya wananchi, bali ilizimua azimio hilo kuwapatia viongozi wa kati uwezo wa kumudu makali ya maisha.
"Serikali haikufuta Azimio la Arusha. Ililizimua azimio hilo kuwapatia viongozi wa kati kumudu makali ya maisha, lakini baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia vibaya nafasi hiyo kuvunja sheria ya maadili ya viongozi," amesema.
Alhaji Mwinyi ameeleza hayo leo jijini Dar es Salaam katika semina ya siku moja ya maandalizi ya sheria ya kudhibiti mgongano wa maslai miongoni mwa viongozi na watumishi wa umma iliyoandaliwa na Sekretarieti ya Maadili ya viongozi.
"Baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vibaya nafasi hiyo kuvunja maadili ya viongozi wa umma kwa kutumia raslimali za umma kujinufaisha. Tabia hii imewafanya wananchi kutokuwa na imani na viongozi wao," amesema.
Kwa mujibu wa Alhaji Mwinyi, mgongano wa maslai ini tatizo kubwa nchini linalotakiwa kuangaliwa kwa umakini vinginevyo baadhi ya viongozi wataendelea kujinufaisha kwa kutumia nafasi zao kazini.
Kwa upande wake Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi Jaji Salome Kaganda amesema lengo na makusudi ya mapendekezo ya sheria hii ni kuleta amani na utulivu wan chi.
Jaji Kaganda amesema, "mapendekezo ya sheria hii hayalengi kuwafanya viongozi kuwa maskini, bali kasi yao ya ukwasi iendane na halii halisi ya kipato chao."
"Sheria hii itakapopitishwa na ngazi husika, itapunguza ubinafsi wa viongozi walioko madarakani kujipendelea wenyewe na maeneo wanayotoka," amesema na kuongeza kuwa, "Lazima kuwepo na hatua uya serikali kurejesha maadili ya maadili. Kama itazingatiwa na kuheshuimiwa, taifa litafikia maendeleoo ya haraka yaliyokusudiwa." Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WAANDAMANAJI WAMTAKA NAWAZ SHARIF AJIUZULU

Waandamanaji wanaotaka waziri mkuu Nawaz Sharif ajiuzulu. Islamabad, Pakistan Aug. 19, 2014.
Waandamanaji wanopinga serikali nje ya bunge la Pakistan, hawaonyeshi ishara yoyote ya kuondoka,hadi pale waziri mkuu Nawaz Sharif atakapojiuzulu, dai ambalo serikali imekataa kwa misingi ya kuwai kinyume na katiba. Wakati huo, huo jeshi lenye nguvu la Pakistan limeonya pande zote kutatua mzozo wao kupitia majadiliano.
Maelfu ya waandamanaji wanopinga serikali wamekuwa katikati ya mji mkuu wa Pakistan kwa karibu wiki moja, katika juhudi za kumshinikiza waziri mkuu Nawaz sharif kujiuzulu.
Wote serikali na viongozi wa maandamano hayo hawaelekei kurudi nyuma, na hivyo kuongeza hofu ya mapambano baina ya polisi na waandamanaji hao kila kuchao.
Mwanasiasa wa upinzani Imran Khan na kiongozi mashuhuri wa kidini Tahir-ul Qadri, wameaanda maandamano ya umma, ingawa si kwa ushirikiano lakini wanamtaka waziri mkuu Sharif kuachia madaraka.
Maandamano hayo dhidi ya serikali yamelazimisha sehemu kubwa ya mji huo kufungwa na kuvuruga maisha ya kila siku pamoja na shughuli za kibiashara. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
CHANZO:VOA

RATIBA LIGI KUU BARA 2014/2015 YAANIKWA HADHARANI, MAXIMO KUANZA NA MTIBWA, PHIRI NA WAGOSI WA KAYA


Kocha mkuu wa Yanga akiongea na msaidizi wake
RATIBA ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 utakaoanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu umeanikwa hadharani na Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF.
Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo katika taarifa yake amesema ratiba hiyo imezingatia michuano ya Chalenji itakayochezwa Novemba, usajili wa dirisha dogo Nov 15- Des 15, ushiriki wa klabu za Azam na Yanga kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa (CL) na Kombe la Shirikisho (CC).
Wambura alisema mechi zitachezwa wikiendi ili kuongeza msisimko/kuwapa fursa washabiki wengi zaidi kuhudhuria, na katikati ya wiki imeachwa wazi kwa ajili ya mechi za Kombe la FA (Federation Cup).
DSC_0007-546x291
Kocha mkuu wa Simba sc Patrick Phiri akiongea na wachezaji wake  
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAREKANI YALAANI MAUAJI YA MWANDISHI

James Foley
Rais Barack Obama wa Marekani amesema mauaji ya mwandishi wa habari James Foley raia wa Marekani aliyeuawa na wapiganaji wa kundi la Kiislam yameishtua dunia.
Obama amesema kitendo hicho ni cha kikatili na kisichokubalika mbele za Mungu na kwamba ni matokeo ya mawazo duni yasiyoendana na karne ya sasa.
Kauli hiyo ya Rais Obama inakuja huku wazazi wa mwandishi huyo wakielezea kutoridhishwa kwao na hatua zinazochukuliwa na Marekani kutokana na mauaji ya mtoto wao.
Wazazi hao wamesema wakati mwingine waandishi wa habari huru hawathaminiwi katika aki zao hata pale wanapojitolea maisha yao kwa ujira mdogo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...