Sunday, March 17, 2013

LOWASSA, MENGI KUFANYIWA UMAFIA KAMA ABSALOM KIBANDA.

 EDWARD LOWASSA.
Reginald Mengi.

AFISA IKULU AHUSISHWA NA MKAKATI HUO, AFYA YA LWAKATARE YAZIDI KUDOROLA
 WAKATI sakata la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare anayetuhumiwa kupanga mikakati ya uhalifu na kurekodiwa kwa video likizidi kuibua maswali, vigogo wengine wanadaiwa kuandaliwa mpango wa kurekodiwa kwenye video ili kuwachafua na kuwanyamazisha, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Vigogo hao ni pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.

Taarifa za mkakati huo zilisambazwa jana kwenye mtandao maarufu wa Jamii Forum, huku ukihusisha mawasilino ya ofisa mmoja wa Ikulu ya Rais Kikwete akieleza kufurahishwa kwake na kuwapongeza waliofanikisha mpango wa kuandaa video ya Lwakatare ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

AZAM FC YAMJIBU SHAFFIH DAUDA


UONGOZI WA SSB na Azam FC umesikitishwa na makala iliyotolewa na Blogu ya Shaffihdauda eti, klabu zimekuwa zikidhulumiwa na SSB na Azam FC kwa mechi zao kurushwa Live na Star TV. 

Tungependa ieleweke kuwa Azam FC ingependa kuona mashabiki wake nchini na nje ya nchi wakiiona mechi live na ndiyo maana tumekuwa tukilipia matangazo hayo, pia tunadhani hili ni jambo jema la kuungwa mkono na wadau.

Pia tungependa ifahamike kuwa kwenye kipengele cha mkataba kati ya SSB na Star TV, kuna kipengele kinachoilazimisha Star TV kutoa sehemu ya pato lake na kuvilipa vilabu ambapo kwa mechi moja klabu hupata shilingi milioni moja (1,000,000)

Kwa mechi zinazochezwa chamazi, klabu hupata mgao wa kiingilio wa chini ya shilingi laki tatu hivyo nyongeza ya milioni moja kwa mechi kurushwa live ni pesa ya kutosha angalau kwa kuanzia

Dk. Slaa aivuruga CCM


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kauli ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa kwamba kuna baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola wanaripoti kwake, kimesababisha baadhi ya wananchi kukosa imani na vyombo hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkoa Maalum wa CCM Dar es Salaam baada ya kikao chao kutathimini mambo na matukio mbalimbali yanayolitikisa taifa kwa sasa.
Katika taarifa yao iliyosainiwa na Katibu wa Wilaya ya Dar es Salaam (ya kisiasa - CCM), Daniel Zenda ilisema kuwa Dk. Slaa amekuwa akitoa kauli hizo mara kwa mara tangu wakati wa kampeni za urais mwaka 2010, lakini hajaitwa kuulizwa wala kuchukuliwa hatua.
“Lakini pia kauli ya Dk. Slaa imesababisha wananchi wakose imani na Idara ya Usalama na zaidi kupoteza imani juu ya uwezo wa serikali kuwalinda na kuwahakikishia usalama wa maisha yao, ambapo ni jukumu la kikatiba la serikali,” ilisema taarifa hiyo.

Rais Kikwete apokea Ujumbe maalumu toka kwa Rais wa Botswana.


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Botswana uliowasilishwa na  Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo Mhe Pandu Skelemi Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Botswana uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo Mhe. Pandu Skelemi Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Botwana Mhe Pandu Skelemi baada ya kupokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa nchi hiyo jana Ikulu jijini Dar es salaam.(PICHA NA IKULU).

Papa Francis akataa vitu vya kifahari

Siku chache baada ya kuchaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amewashangaza wengi mengi kwa kukataa kuvaa viatu vya kifahari na msimamo wake kuwekwa wazi kuwa hatavumilia makasisi watakaotenda uovu.
 
 Papa Francis 1
Tayari, Papa Francis ameelezwa kuwa kiongozi asiyetaka makuu, mhafidhina na mtu ambaye hataweza kubadili mengi katika kanisa hilo lenye waumini bilioni 1.2 duniani.
Katika siku mbili za uongozi wake, Papa Francis amelithibitisha hilo kwa kutokea hadharani akiwa amevaa viatu rahisi, vyeusi na kuachana na vyekundu vya kifahari vilivyopendelewa na mtangulizi wake, Benedict VXI.
Kutoka Uk 1

Katika uongozi wake, siku zote Papa Benedict, alivaa viatu vyekundu vilivyotengenezwa kwa mkono, jambo ambalo Papa Francis anaonekana kuachana nalo.
Watu walio karibu naye Papa Francis, wanaeleza kuwa kabla ya kuondoka Buenos Aires, Argentina kwenda Rome, Kardinali Jorge Mario Bergoglio, kama alivyojulikana awali, alivaa viatu rahisi vya rangi nyeusi, na kuwafanya marafiki zake, wakiwamo mapadri kutaka kumnunulia viatu vingine vipya.

“Siku ile aliyoondoka mjini Buenos Aires kuelekea Rome kwa ajili ya mkutano wa uchaguzi wa Papa (conclave), marafiki zake walimpa zawadi ya viatu. Yeye, siku zote amekuwa akitokea hadharani akiwa amevaa nguo rahisi, viatu vya kawaida,” walieleza mapadri hao kutoka Amerika Kusini walipozungumza na Kituo cha Redio Vatican.
Mbele ya makardinali 106
Juzi Ijumaa alipokutana na makardinali 106, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 76, licha ya kuonyesha uso wa furaha na kuwatania aliwaonya makardinali hao kuhusu wajibu wao kama viongozi wa kanisa maeneo mbalimbali duniani akiwataka kutosahau kuwa hawarudi kwenye ujana.


Katika ukumbi wa Sala Clementina, ulioko Vatican Papa Francis pia aliwataka makardinali hao wakiwamo waliomchagua kuwategemea zaidi vijana aliosema ndio nguzo kuu muhimu ya ustawi wa Kanisa Katoliki, huku aliwashauri makardinali kusaka njia sahihi ya kueneza Ukristo pande zote za uso wa dunia katika karne ya 21.
Aidha, alimsifu mtangulizi wake, Papa Benedict kwa uamuzi wa kijasiri wa kustaafu, akieleza kuwa ni uamuzi wa busara, wenye kuonyesha ukomavu na kuwataka wasichoke kuiga matendo mema.
Yaliyomo kitabuni mwake

Kupitia kitabu, On Earth and Heaven (Duniani na Mbinguni) alichokiandika akiwa kardinali, Papa Francis alitoa taswira yake kama mtu mwenye dhamira safi hasa katika masuala ya kusaidia jamii, muumini thabiti anayeamini katika majadiliano baina ya makundi ya imani tofauti.

Msimamo kuhusu makasisi
Papa Francis ameonyesha wazi kuchukizwa na matendo ya makasisi (mapadri) wasio waadilifu, ambao kwa miaka mingi wamelifedhehesha kanisa na kwamba yeye hakubaliani na wanaoficha maovu ya baadhi ya mapadri ukiwamo ulawiti.
“Suala la useja (mapadri kutokuoa) kwamba ndicho chanzo cha ulawiti linaweza kusahaulika,” anaeleza katika kitabu hicho. “Endapo padri ni mlawiti, alikuwa hivyo hata kabla ya ukasisi wake. Lakini, hili linapotokea, lisiangaliwe kwa mtazamo tofauti, lisifichwe. 

Kama kiongozi, hutakiwi kutumia madaraka yako kuangamiza maisha ya mwingine.”
Kuhusu hatua gani atachukua, wakati akiwa Kardinali Bergoglio, alijibu kuwa hawezi kukubaliana na waovu, lakini alipoulizwa kama askofu angechukua hatua gani dhidi ya mapadri wa aina hiyo, alijibu,” Nitamfukuza kazi, kisha kumshtaki, jukumu langu ni kuweka usafi wa kanisa mbele.
“Hili ni suluhisho kwa matukio kama hayo kama jinsi ilivyopendekezwa Marekani; lakini si kuwahamisha wakosaji kutoka parokia moja kwenda nyingine.
“Huu ni upuuzi, kwani hata huko wataendeleza tatizo hilo. Jibu sahihi kwa tatizo hili ni kutowavumilia.”

Katika kitabu hicho, Papa Francis anazungumzia maisha ya utauwa (usafi wa moyo), uadilifu na maovu akiweka wazi msimamo wake usio wa mzaha na kuruhusu mijadala baina ya makundi ya imani tofauti, msimamo ambao unaweza kupingwa na baadhi ya Wakatoliki wenye msimamo mkali.Kwa maneno yake, Papa Francis anaonyesha kuwa mtu mwenye akili, anayefikiri haraka, mjuzi wa mambo, anayechanganya uhafidhina wa kijamii na akiwa mwenye msimamo mkali wala kutokukubali upuuzi kwa mambo asiyoyapenda au kuyakubali.

Kiongozi huyo ameahidi kutumia Jumamosi ya Machi 23 kumtembelea mtangulizi wake, Papa Benedict katika jumba analoishi huko Castel Gandolf, kusini mwa Rome na anaeleza kuwa kanisa limepitia nyakati ngumu. “Kumekuwa na vipindi vingi, majaribu mengi. Kumekuwa na vipindi vigumu, lakini, kanisa limesimama imara.”
Hata hivyo, katika misa yake ya kwanza, Alhamisi, Papa Francis alieleza kuwa kanisa hilo halina budi kwenda na wakati, kukubali mabadiliko.

“Ni dhahiri kuwa katika historia yake, kanisa limebadilika mno, sioni sababu za kwa nini tusikubali mabadiliko na kuwa utamaduni wetu wa sasa,” anaeleza.
Alieleza kuwa mafundisho ya msimu ya Kikatoliki, msimamo kuhusu mashoga, ndoa za jinsia moja, hayawezi kubadilika.
Pia, anaeleza kuwa utoaji mimba ni tatizo la kisayansi zaidi, lakini ambalo haliwezi kukubaliwa na kanisa.
Kuhusu utandawazi, Papa Francis alieleza kwamba hakubaliani nao kwa kuwa mfumo huo hauheshimu tamaduni. “Aina ya utandawazi unaofanya vitu vyote kuwa sawa ni aina ya unyama,” anaeleza akiongeza kwamba tofauti za kitamaduni hazina budi kudumishwa.
“Hatimaye, utandawazi unageuka njia ya kuwatumikisha wengine,” alisema.

BALOZI KAMALA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO UHOLANZI

IMG_1539Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania waishio Uholanzi (TANE), Bw. Musuto wa Chirangi  (aliyesimama) akizungumza wakati wa kumkaribisha Balozi Kamala.IMG_1548Mwenyekiti wa TANE, Bw. Kweba Bulemo (aliyesimama Kulia), akisema machache kabla ya kumkaribisha Mhe. Balozi.

Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe Atua Shinyanga, tayari kuzindua Kanda ya Ziwa Mashariki

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kakola, mahali ambapo mgodi wa dhahabu wa Buzwagi unapatikana, Emmanuel Bombeda anayetokana na chama hicho, wakati kiongozi huyo mkuu wa CHADEMA alipokuwa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama hicho, baada ya kuwasili mkoani Shinyanga, kwenye kikao cha Baraza la Uongozi Kanda ya Ziwa Mashariki (Mara, Shinyanga na Simiyu). Mbowe anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara Mjini Shinyanga, kufanya uzinduzi wa kanda hiyo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...