Friday, November 21, 2014

NDERAKINDO AMKANA SAMUEL SITTA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akitoa ufafanuzi bungeni kuhusu mgogoro wa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, mjini Dodoma jana.

Wakati Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akisema ofisi yake imewakutanisha na kumaliza mgogoro baina ya wabunge wawili wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), mmoja wa wabunge hao, Dk Nderakindo Kessy amesema hakuna kitu kama hicho.

Dk Kessy jana aliripotiwa na vyombo vya habari akidai kupigwa na mbunge mwenzake, Shy-Rose Bhanji, akisema alisababishiwa maumivu makali, lakini likapingwa na Sitta. Jana, sakata hilo lilitinga bungeni na Serikali ikitakiwa kutoa maelezo kwa nini wabunge wa Tanzania wanafanya mambo ya ajabu.

Akijibu swali hilo, Waziri Sitta alisema ilitokea bahati mbaya Bhanji kupitia CCM akamgonga Dk Kessy (NCCR-Mageuzi) na kwa kuwa mbunge huyo wa chama tawala alikuwa na haraka kwenda kuwahi gari, hakusimama, hivyo baadhi ya wabunge wa Uganda wakamshauri Dk Kessy kwenda kuripoti tukio hilo polisi. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 21, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

NAPE: WAPUUZENI WAPINZANI

Wananchi wametakiwa kupuuza kauli alizodai kuwa za wapinzani za kuwataka wasishiriki kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika Desemba, mwaka huu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema hayo juzi alipozungumza na wakazi wa Nchingwea  mkoani Lindi.
Alisema ni marufuku kwa vyama vya upinzani kuzuia wananchi kupiga kura na kumchagua kiongozi wanayempenda
“Tumepata taarifa kuna wapinzani wameanza kuwatisha wananchi wasiende kupiga kura siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,” alidai Nape.
“Hizi ni salamu kwa wapinzani wenye mpango huo kuwa hatutawaacha, lazima tutawashughulikia.”
Alisema kupiga kura ni haki ya kila mwananchi, hivyo kitendo cha kuzuia watu ni sawa na kubaka demokrasia, jambo ambalo CCM haitalivumilia.
Nape alisema CCM imejipanga vizuri na kwamba ina uhakika wa kushinda kwa kishindo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

POLISI WABAKAJI WAONGEZEWA ADHABU

 Baadhi ya wanawake ndio walilalamika kuwa adhabu waliyopewa polisi hao ilikuwa ndogo sana 
 
Polisi wawili nchini Tunisia walioshitakiwa kwa kumbaka mwanamke ndani ya gari la polisi, wameongezewa adhabu katika kesi iliyowashtua wengi.
Maafisa hao walifungwa jela mwezi Machi huku kukiwa na malalamiko kwamba adhabu hiyo haitoshi.
Hukumu hiyo, iliongezwa hadi miaka 15 Alhamisi baada ya rufaa kuwasilishwa mahakamani na mwathiriwa wa kitendo hicho cha unyama Meriem Ben Mohamed.
Wakili wake alitaja hatua ya mahakama kuwoangeza adhabu watuhumiwa kama jambo zuri, na pia kusifu ambavyo kesi za ubakaji zinashughulikiwa nchini Tunisia.
Aliambia shirika la habari la AFP, kwamba ameridhishwa na adhabu hiyo.
"lakini bado haitoshi, kwa maoni yangu kwa tendo la kukera kama hilo,'' aliongeza kusema wakili huyo.
Meriem Ben Mohamed alishambuliwa mwaka 2012 na maafisa wa polisi waliosimamisha gari lake alimokuwa na mpenzi wake mjini Tunis. Alikuwa na umri wa miaka 27.
Polisi wa kupambana na vurugu nchini Tunisia
Watuhumiwa walikanusha mashitaka wakisema kuwa waliwapata wawili hao wakiwa wanashirki tendo la ndoa ndani ya gari lao.
Maafisa wa polisi walijaribu kuwashitaki Meriam na mpenzi wake kwa kosa la kukosa maadili lakini maandamano yalifanywa kupinga hatua kama hiyo huku wengi wakiwatetea wawili hao.
Ilisababisha Rais wa Tunisia kumsamehe Meriam na mpenzi wake.
Afisaa mwingine wa tatu aliyejaribu kuwatoza hongo wawili hao, atatumikia kifungo cha miaka miwili alichokuwa amepewa.
Ripoti iliyotolewa na mtaalamu wa kisaikolojia ilisema kuwa yote yaliyotokea yalimsababisha Meriam kusongwa na mawazo.
Kesi hii inatokea wakati ambapo kumekuwa na shinikizo kali kwa serikali kuzingatia haki za wanawake kufuatia kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali.

Na BBC

MKANYAGANO HATARI WAWAUA 11 ZIMBABWE

Watu 11 wamefariki katika mkanyagano nchini Zimbabwe baada ya ibada ya kidini kufnayika katika uwanja wa soka.
Polisi wanasema kuwa watu wanne walifariki katika uwanja huo ulio mjini Kwekwe wakati wengine saba wakifariki hospitalini.
Mkanyagano huo ulitokea wakati maelfu ya waumini wakikimbilia kuondoka uwanjani humo baada ya ibada iliyoongozwa na mhubiri wa kipentekoste Walter Magaya.
Mhubiri huyo anadai kuwaponya watu kwa kufanya miujiza.
Baadhi ya walioshuhudia mkanyagano huo wanatuhumu polisi kwa kufunga baadhi ya milngo ya kuondokea uwanjani humo, huku watu wakiondoka kupitia mlango mmoja tu.
Hata hivyo polisi wanakana kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.
Bwana Mugaya ambaye ni mkuu wa kanisa la 'Prophetic Healing and Deliverance' aliambia vyombo vya habari kuwa alipopata habari ya kutokea vifo hivyo alihuzunika sana. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RONALDO AOSHA VYOMBO BAADA YA KUSHINDWA

Ronaldo aosha vyombo baada ya kushindwa katika karata na mchezaji wa Tenisi Rafa Nadal 

Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Brazil Ronaldo alilazimika kuosha vyombo baada ya kushindwa katika mchezo wa karata na mchezaji wa tennisi Rafa Nadal,
na kumfanya mchezaji huyo wa tenisi kupokea dola 50,000 za hazina yake ya kutoa msaada huku Ronaldo akiosha vyombo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 alikabiliana vilivyo na mwana tenisi huyo kutoka uhispania katika mechi kati ya wawili hao katika meza ya pokerstar, Casino ya Hippodrome mjini London ambapo Nadal alishinda fedha hizo.
Duru ziliarifu kwamba kiini cha nyota hao wawili kukutana katika chumba kimoja ni chakula kilichoandaliwa katika hafla hiyo.
Hatahivyo kitu kilichowafurahisha wengi kulingana na wageni ni hatua ya Ronaldo kukubali kushindwa na kupewa kazi ya kuviosha vyombo vya Nadal alivyotumia kula. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ADEBAYOR ADAI MAMAAKE NI MCHAWI


Mchezaji huyu wa kilabu ya Totenham amedai kuwa mamaake amekuwa akitumia uchawi kujaribu kumuharibia kazi yake. 
 
Mshambuliaji wa kilabu ya Totenham nchini Uingereza Emmanuel Adebayor amekosana na mamaake kwa madai kwamba anatumia uchawi kumharibia kazi yake.
Duru zimearifu kuwa mama huyo tayari ameondoka katika nyumba ya familia huku dadaake Adebayor akiambia radio moja ya mjini Accra kwamba Adebayor ndiye aliyemfukuza.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Arsenal anadai kwamba mamaake aliondoka mwenyewe na kwamba hawana mawasiliano yoyote kati yao kwa kuwa amekuwa akitumia uchawi kutaka kumuharibia kazi yake.

Adebayo aliwahi kuchezea Arsenal
'' Ninawezaje kuzungumza na mama ambaye yeye na dadaangu wamekuwa wakijaribu kuniroga''aliwauliza maripota.Mchezo wa Adebayor katika kilabu ya Tottenham umeathirika katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita huku Tottenham ikidaiwa kujaribu kumuuza kwa mkopo mchezaji huyo katika dirisha la uhamisho mnamo mwezi January kufuatia kushuka kwa mchezo wake.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...