Friday, November 21, 2014

NAPE: WAPUUZENI WAPINZANI

Wananchi wametakiwa kupuuza kauli alizodai kuwa za wapinzani za kuwataka wasishiriki kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika Desemba, mwaka huu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema hayo juzi alipozungumza na wakazi wa Nchingwea  mkoani Lindi.
Alisema ni marufuku kwa vyama vya upinzani kuzuia wananchi kupiga kura na kumchagua kiongozi wanayempenda
“Tumepata taarifa kuna wapinzani wameanza kuwatisha wananchi wasiende kupiga kura siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,” alidai Nape.
“Hizi ni salamu kwa wapinzani wenye mpango huo kuwa hatutawaacha, lazima tutawashughulikia.”
Alisema kupiga kura ni haki ya kila mwananchi, hivyo kitendo cha kuzuia watu ni sawa na kubaka demokrasia, jambo ambalo CCM haitalivumilia.
Nape alisema CCM imejipanga vizuri na kwamba ina uhakika wa kushinda kwa kishindo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...