Friday, November 21, 2014

NDERAKINDO AMKANA SAMUEL SITTA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akitoa ufafanuzi bungeni kuhusu mgogoro wa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, mjini Dodoma jana.

Wakati Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akisema ofisi yake imewakutanisha na kumaliza mgogoro baina ya wabunge wawili wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), mmoja wa wabunge hao, Dk Nderakindo Kessy amesema hakuna kitu kama hicho.

Dk Kessy jana aliripotiwa na vyombo vya habari akidai kupigwa na mbunge mwenzake, Shy-Rose Bhanji, akisema alisababishiwa maumivu makali, lakini likapingwa na Sitta. Jana, sakata hilo lilitinga bungeni na Serikali ikitakiwa kutoa maelezo kwa nini wabunge wa Tanzania wanafanya mambo ya ajabu.

Akijibu swali hilo, Waziri Sitta alisema ilitokea bahati mbaya Bhanji kupitia CCM akamgonga Dk Kessy (NCCR-Mageuzi) na kwa kuwa mbunge huyo wa chama tawala alikuwa na haraka kwenda kuwahi gari, hakusimama, hivyo baadhi ya wabunge wa Uganda wakamshauri Dk Kessy kwenda kuripoti tukio hilo polisi. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Alifafanua kuwa wabunge hao wamekutanishwa pamoja, wamezungumza yameisha.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Kessy alisema tangu tukio hilo lilipotokea hajakutana, kukutanishwa wala kuzungumza na Bhanji, bali mbunge mwenzake huyo amekuwa akimpita bila kumsemesha lolote.

Dk Kessy alisema wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo wamegawanyika na katika baadhi ya vikao wanavyofanya baadhi yao hawaitwi.

Bhanji, ambaye amekuwa katika mgogoro na wabunge wenzake kwa kipindi cha miezi miwili sasa na hadi jana alikuwa hapatikani kwa simu kujibu madai hayo ya kumvamia Dk Kessy na kumpiga mgongoni. Akizungumza kwa simu kutoka Nairobi, Dk Kessy alisema tukio hilo lilitokea bungeni juzi jioni baada ya kikao kuahirishwa.

Kauli ya Sitta

Jana Mbunge wa Konde (CUF), Khatibu Said Haji aliomba mwongozo wa Spika akitaka kujua kwa nini baadhi ya wawakilishi wa nchi katika Bunge la Afrika Mashariki wanafanya mambo ya ajabu hivyo akataka kujua hatua gani zimechukuliwa dhidi ya Bhanji.

Naibu Spika, Job Ndugai ilimpa nafasi Sitta ambaye alisema kilichotokea kinahusiana na mgogoro ulioko kati ya wabunge na Spika wa Eala, Dk Magreth Zziwa.
“Wabunge wamegawanyika pande mbili, kuna wanaotaka Spika abaki na wengine wanataka aondoke na Tanzania ndiyo kikwazo kwa kuwa wanataka abaki,” alisema Sitta.
Alisema kilichotokea juzi siyo kama kinavyoelezwa, kwani Shy-Rose ni mfuasi mkubwa wa Spika hivyo alikuwa anawahi gari akapita katikati ya wabunge na kumgonga Kessy ambaye alihamaki na kwenda polisi kufungua madai ya kushambuliwa.
Sitta alisema askari wa Bunge jijini Nairobi walijaribu kumaliza jambo hilo na kwamba walifanikiwa baada ya kuwaweka Shy-Rose na Kessy pamoja kisha kuzungumza na kuyamaliza wakati huohuo.
Alisema kuhusu madai ya mambo aliyofanya Shy-Rose miezi mitatu iliyopita, Serikali inasubiri Tume ya Eala ieleze nini kilichotokea ili Bunge kama jimbo ichukue uamuzi.
“Kwa sasa hatuwezi kufanya lolote, kuna mambo tunasubiri kwanza ndipo tufanye uamuzi,” alisema Sitta.
Bunge la Eala, tangu mwanzoni mwa mwaka huu, limekuwa likitawaliwa na vioja na mivutano ya hapa na pale na mikakati ya kumng’oa Spika Zziwa kwa madai ya kutofanya kazi kwa weledi ikishindwa kutimia.
Hivi karibuni, Bhanji aliliingiza Bunge hilo katika mvutano baada ya kudaiwa kuliaibisha wakati wa ziara ya nchini Ubelgiji iliyowashirikisha wajumbe wa tume na wenyeviti wa kamati za Bunge akituhumiwa kufanya fujo ndani ya ndege kwa kutoa lugha chafu kwa wabunge wenzake na wahudumu wa ndege.
Baada ya tukio hilo, baadhi ya wabunge walitaka Bhanji achukuliwe hatua za kinidhamu, jambo ambalo halijatekelezwa hadi sasa na kuchochea mgogoro zaidi. Mara zote Bhanji amekuwa akikana tuhuma dhidi yake na kudai zinalenga kumchafulia jina. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...