Friday, November 21, 2014

MKANYAGANO HATARI WAWAUA 11 ZIMBABWE

Watu 11 wamefariki katika mkanyagano nchini Zimbabwe baada ya ibada ya kidini kufnayika katika uwanja wa soka.
Polisi wanasema kuwa watu wanne walifariki katika uwanja huo ulio mjini Kwekwe wakati wengine saba wakifariki hospitalini.
Mkanyagano huo ulitokea wakati maelfu ya waumini wakikimbilia kuondoka uwanjani humo baada ya ibada iliyoongozwa na mhubiri wa kipentekoste Walter Magaya.
Mhubiri huyo anadai kuwaponya watu kwa kufanya miujiza.
Baadhi ya walioshuhudia mkanyagano huo wanatuhumu polisi kwa kufunga baadhi ya milngo ya kuondokea uwanjani humo, huku watu wakiondoka kupitia mlango mmoja tu.
Hata hivyo polisi wanakana kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.
Bwana Mugaya ambaye ni mkuu wa kanisa la 'Prophetic Healing and Deliverance' aliambia vyombo vya habari kuwa alipopata habari ya kutokea vifo hivyo alihuzunika sana. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...