Tuesday, January 28, 2014

"MBWA MWITU" SASA TISHIO KWA WANANCHI WA TABATA DAR


Dar es Salaam. Wakazi wa Tabata na viunga vyake, sasa wanaishi kwa wasiwasi mkubwa kutokana na kuibuka kwa kundi la vijana, wanaojiita Mbwa Mwitu wakitumia silaha za jadi, kujeruhi watu na kupora mali nyakati za usiku.
Mmoja wa wananchi wa Tabata Matumbi alisema wiki mbili zilizopita, vijana hao walimuua mwanamume mmoja kwenye Daraja la Reli la Matumbi. Kwa mujibu wa mtoa habari huyo ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe, mtu huyo alichinjwa na kichwa chake kutenganishwa na kiwiliwili.
“Watu walipeleka kiwiliwili kituo cha polisi, maana kichwa hakikupatikana na haikufahamika kama alitambuliwa au vipi. Yaani sasa hivi ikifika saa tatu watu inabidi tubaki ndani,” alisema.
 Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

M4C OPERESHENI PAMOJA DAIMA NDANI YA IRINGA


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Iringa, katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa jana.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akihutubia katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa mjini Iringa jana.
Maelefu ya wakazi wa Manispaa ya Iringa na vitongoji vyake wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Operesheni ya M4C Pamoja Daima wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa jana. (PICHA NA CHADEMA)

 Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

KINANA KUPIGA KAMBI Z’BAR KUIMARISHA CCM

kinana_98cb1.jpg
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi
Zanzibar. Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amesema ameamua kuweka kambi Zanzibar, lengo likiwa ni kuimarisha chama hicho na kuhakikisha CCM inarejesha majimbo yake yaliyopotea tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995.
Kinana aliweka msimamo huo kwenye mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa miaka 37 ya kuzaliwa CCM, uliofanyika uwanja wa Soka Kiembesamaki mjini hapa juzi.
Alisema kambi hiyo itaanza kabla ya Aprili mwaka huu, kwa kufanya ziara kuanzia ngazi ya wadi, jimbo, wilaya hadi mikoa kukagua hali ya kisiasa na kuweka mikakati mipya ya chama hicho kisiwani Zanzibar.
"Nitaanza ziara maalumu kabla ya sherehe za Muungano, mengi nitayazungumza wakati huo ukifika, lengo kubwa ni kuangalia uhai wa chama chetu na kuweka mikakati ya kisiasa kabla ya mwaka," alisema Kinana.
Alisema kazi kubwa ya CCM ni kutekekeza sera na ilani yake ya uchaguzi tofauti na vyama vya upinzani, ambavyo ni mahiri na hodari wa kusema bila ya kuonyesha vitendo.
Katibu Mkuu huyo aliviponda vya upinzani nchini na kwamba, CCM imewaachia kazi ya kusema, yenyewe imekijikita kuwatumia wananchi na kutekeleza majukumu yake ya kisera, mipango na mwongozo.
Kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Kinana alisema watu waliobeza Mapinduzi hayo hivi sasa wamefedheheka kwa kushuhudia yakitimiza miaka 50 huku taifa likiwana hali ya amani, umoja na mshikamano.

 Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MTWARA WASHUSHIWA BEI YA KUINGIZA UMEME HADI TSH. 27,000/=

mhongo 67365
Serikali imetangaza neema kwa vijiji vinavyopitiwa na bomba la gesi ambavyo vipo mkoani Mtwara na Lindi, sasa wataunganishiwa kwa Sh27,000. (HM)
Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uzinduzi mradi wa umeme wilayani Nanyumbu na Masasi.
Profesa Muhongo alisema gharama za kuunganisha umeme kwa sasa ni Sh177,000.
Alisema zaidi ya vijiji 50 vimepewa upendeleo huo ili kuwawezesha wananchi kuwa na maisha bora.
Lengo la Serikali ni kufikia asilimia 30 ya wasasatu waliounganishwa na umeme na kwamba, hivi sasa ni asilimia 23 pekee wanaopata umeme nchini wakati Mtwara ni asilimia nne.
 Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

CHADEMA WAANZA KAMPENI ZA URAIS...!!!

Willibrod-Slaa 9cd30
Viongozi mbalimbali wa Chadema wameanza kupiga kampeni za urais mwaka 2015 kupitia Operesheni Pamoja Daima. (HM)
Akihutubia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Njombe huku mvua kubwa ikinyesha jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa aliwatahadharisha vigogo wa Serikali wanaoiba fedha za umma kuwa, atawashtaki na kuwafilisi iwapo chama hicho kitashinda uchaguzi mwaka 2015.
Alisema chama hicho kikishinda dola, kitaboresha masilahi kwa watumishi waadilifu lakini mafisadi wanaotafuna fedha za Serikali watapata wakati mgumu.
"Tutakuwa wakali kwa walarushwa," alisema Dk Slaa.
Dk Slaa alisema watendaji walarushwa na wezi watashtakiwa ili mali walizowaibia Watanzania zirejeshwa Serikalini.
"Ninawapa miezi 15 kabla ya uchaguzi mkuu, vigogo hao kurudisha mali walizoiba vinginevyo watajuta kwa sababu tutawashtaki tutakapoingia madarakani." alisema.
Naye Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alisema chama hicho kitatumia kila aina ya 'silaha' kilichonayo kuhakikisha majimbo yote ya Mkoa Kilimanjaro yananyakuliwa na chama hicho 2015.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

NYOKA MKUBWA AINA YA COBRA AILAZIMISHA NDEGE KUTUA BILA KUFIKA MWISHO WA SAFARI

NewsImages/6694982.jpgMoja ya ndege zinazo milikiwa na shirika na ndege la Misri.
NYOKA aina ya Cobra amesababisha kizaza kwenye ndege na kuilazimisha kukatisha safari yake na kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Hurghada nchini Misri, auliwa baada ya kumjeruhi abiria .
Nyoka huyo alizua mtafaruku huo baada ya kutoka katika mfuko alipokuwa amehifadhiwa na kumjeruhi abiria mmoja raia wa Jordan aliekuwa amekaa karibu na mfuko uliokuwa amehifadhiwa nyoka huyo.
Abiria walianza kumshambulia wakijaribu kumuua kwa kumpiga na viatu na hatimae kufanikiwa kumuua, abiria aliejeruhiwa alipatiwa huduma ya kwanza, na kuhamishiwa hospitalini kwa matibabu zaidi na kuwekwa chini ya uangalizi kwa masaa 24, hali iliopekea kukatisha safari yake.

Uchunguzi wa awali uliofanywa umebaini kwamba, mmoja wa abiria alimficha nyoka huyo kwenye mkoba na alifanikiwa kupita katika vizuizi na kuingia na nyoka huyo kwenye ndege.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya 
Jambo Tz

MWANAMKE ANASWA NA NGOZI YA CHUI...!!!

Mwanamke anaswa na ngozi za chui
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Mwajuma Hamisi, mkazi wa Yombo Vituka kwa kosa la kukutwa na ngozi mbili za chui kinyume cha sheria, zenye thamani ya sh milioni 11.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema mwanamke huyo alinaswa Januari 18, mwaka huu katika eneo la Yombo Vituka, Wilaya ya Temeke.
Kova alisema mwanamke huyo alinaswa baada ya Ofisa Mhifadhi Wanyamapori mkazi wa Ukonga, kutoa taarifa kituoni hapo kwamba kuna mwananchi anauza ngozi za chui.
Alisema askari walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa na walipompekua chumbani kwake, walimkuta na nyara hizo za serikali.

Wakati huo huo, jeshi hilo limesema limemuua jambazi sugu la uhalifu wa kutumia silaha katika majibizano ya risasi na polisi.
Alisema awali polisi waliweka mtego ili kuyanasa majambazi hayo Januari 22 baada ya kufanya tukio la uporaji wa sh milioni 29 kwa mfanyabiashara wa Mtaa wa Kariakoo, anayejulikana kwa jina la  Shanys Abdalla, mkazi wa Mbezi.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 28.01.2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...