Tuesday, January 28, 2014

MTWARA WASHUSHIWA BEI YA KUINGIZA UMEME HADI TSH. 27,000/=

mhongo 67365
Serikali imetangaza neema kwa vijiji vinavyopitiwa na bomba la gesi ambavyo vipo mkoani Mtwara na Lindi, sasa wataunganishiwa kwa Sh27,000. (HM)
Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uzinduzi mradi wa umeme wilayani Nanyumbu na Masasi.
Profesa Muhongo alisema gharama za kuunganisha umeme kwa sasa ni Sh177,000.
Alisema zaidi ya vijiji 50 vimepewa upendeleo huo ili kuwawezesha wananchi kuwa na maisha bora.
Lengo la Serikali ni kufikia asilimia 30 ya wasasatu waliounganishwa na umeme na kwamba, hivi sasa ni asilimia 23 pekee wanaopata umeme nchini wakati Mtwara ni asilimia nne.
 Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Kuhusu umeme wa gesi, Profesa Muhongo alisema Mtwara wanatarajia kuzalisha megawati 600 ambazo baada ya matumizi nchini, zitauzwa nchi za Malawi, Zambia na Msumbijj.
Awali, akizungumza na mamia ya wakazi wa Mangaka waliofika kushuhudia uzinduzi huo, Pinda alisema mradi huo ni utekelezaji wa azma ya Serikali kuhakikisha kila wilaya inapata umeme.
"Mpango wa kupeleka umeme nchini ni wa miaka mitatu na katika sekta ya nishati chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Sasa (BRN), tumeazimia kwenda kwa awamu," alisema.
ili tuwafikie wananchi wengi zaidi kutoka asilimia 24 ya sasa hadi kufikia asilimia 30 ya watumiaji wa umeme," alisema Waziri Mkuu. 
Chanzo: mwananchi
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...