Monday, April 02, 2018

TAZAMA PICHA ZA NDEGE MPYA YA TATU AINA YA BOMBARDIER Q400 IKIWASILI NCHINI TOKA CANADA



Ndege ya 3 aina ya Bombardier Q400 imewasili leo nchini toka Canada na kupokelewa na kuzinduliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

MKE WA MANDELA AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 81

Winnie Mandela, mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81. Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake.

Winnie alizaliwa Oktoba 26, 1936 ingawa yeye na mumewe  Nelson Mandela walitalikiana mapema miaka ya 1990, Winnie Madikizela Mandela kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Mandela.

Alikuwepo na walishikana mikono alipokuwa akiondoka gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27. Lakini maisha yake pia yalikumbwa na utata. Winnie alikuwa na miaka 20 hivi pale alipojipata katika siasa.

MWIGULU AWAASA MAASKOFU KUHUBIRI INJILI ILI WANANCHI WAWE NA HOFU YA MUNGU KUEPUSHA MATUKIO YA KIKATILI

 Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akionesha albam ya "Usife Moyo" ya Rose Muhando, kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama na Kushoto ni Rose Muhando wakishiriki tukio hilo katika Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana jioni
 Waziri wa Mambo ya Ndani,Dkt Mwigulu Nchemba akipokelewa na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mh. John Mongela mara baada ya kuwasili uwanja wa CCM Kirumba,tayari kwa kuzindua tamasha la pasaka kwa mara ya kwanza chini ya Kampuni ya Msama Promotions Ltd sambamba na uzinduzi wa albamu ya Muimbaji nyota wa muziki wa Injili Rose Muhanda iitwaya 'Usife Moyo' yenye jumla ya nyimbo saba. 
 Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika tamasha la pasaka mapema jana jioni ndani ya uwanja wa CCM 
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Angelina Mabula akimtunza muimbaji wa nyimbo za injili Christopher Mwahangila mapema jana jioni ndani ya tamasha la pasaka.

Waziri Wa mambo ya ndani Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amewasihi viongozi mbalimbali wa dini nchini wakiwemo Maaskofu na Mashekh kutumia muda wao mwingi kwa kutembelea mikoa mbalimbali nchini kunapotokea zaidi matukio ya kikatili ikiwemo mauaji ili kuhubiri injili wananchi wawe na hofu na Mungu jambo litakalopelekea kupunguza ukatili na watu kumjua Mungu.

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA 13 KWA NCHI ZINAZOVUTIA UWEKEZAJI


Shirika la Utafiti la Quantum Global limetoa ripoti ya nchi ambazo zinaongoza kwa kuvutia uwekezaji barani Afrika ambapo nchi ya Morocco imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Misri na Algeria.

Nafasi ya nne imeshikwa na Botswana, Ivory Coast nafasi ya tano, Afrika Kusini nafasi ya sita, Ethiopia nafasi ya saba, Zambia nafasi ya nane, Kenya nafasi ya tisa na Senegal ikishika nafasi ya 10.

Ripoti hiyo imeitaja Tanzania kuwa nchi ya 13 kwa kuwa na kuvutia uwekezaji. Nchi 10 ambazo zimetajwa kuwa hazivutii uwekezaji ni;
1. Afrika ya Kati
2. Liberia  
3. Somalia  
4. Eritrea
5. Equatorial Guinea
6. Gambia
7. Sierra Leone
8. Guinea  
9. São Tomé and Príncipe
10. Zimbabwe

WAZIRI MKUU AZINDUA MBIO ZA MWENGE MKOANI GEITA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwansha Mwenge wa Uhuru kuzindua mbio zake kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018 Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa vijana sita watakaokimbiza Mwenge huo, Charles Kabeho wakati alipozindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU YA PASAKA APRIL 02, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS




Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

MPENZI WA CRISTIANO RONALDO APOST INSTAGRAM KWA KISWAHILI

Lugha ya Kiswahili inazidi kukuwa na kuwavutia watu wengi dunia, jana April 1, 2018 moja kati ya post za mitandao ya kijamii zilizochukua headlines ni post ya mwanamitindo Georgina Rodríguez ambaye ni mpenzi wa staa wa soka wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Georgina Rodríguez ni mwanamitindo na ndio mpenzi wa sasa wa Ronaldo na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Alana Martina, hivyo katika insta story yake amepost picha yake na Ronaldo na kuandika ‘Hakuna Matata’

Msemo wa hakuna matata ni msemo wa Kiswahili ambao umeonekana kupendwa na umekuwa msemo maarufu sana kwa wageni wanaopenda kujua lugha ya Kiswahili, huo huwa ni msemo wao wa kwanza kujifunza lakini haijajulkana bado Georgina Rodríguez ameujulia wapi msemo huo.


Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

AL SHABAAB WAVAMIA KAMBI YA AU NA KUDAI KUUA WANAJESHI 59

Wanamgambo wa kiislamu (Al-Shabaab) wamefanya shambulizi kwenye kambi ya wa jeshi la Muungano wa Afrika AU nchini Somalia.

Wanamgambo hao walilipua mabomu yaliyokuwa yametegwa ndani ya magari mawili nje ya kambi ya jeshi kwenye mji wa Bulamarer, kusini magharibi mwa Mogadishu.

Wenyeji wanasema kuwa walisikia makabiliano makubnwa ya risasi ambayo yalidumu kwa zaidi ya saa tatu.

Msemaji wa Al Shabaab alisema wapiganaji wake 14 waliuawa huku wanajeshi 59 wa AU wakiuawa. Bado madai hayo hayajathitishwa.

Miaka ya hivi karibuni, wanamgambo wa kislamu wamepoteza udhibiti wa miji ya Somalia lakini mara kwa mara hulipua mabomu na kuswashambulia walinda amani.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...