Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akionesha
albam ya "Usife Moyo" ya Rose Muhando, kulia ni Mkurugenzi wa Msama
Promotion Alex Msama na Kushoto ni Rose Muhando wakishiriki tukio hilo
katika Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza jana jioni
Waziri wa Mambo ya Ndani,Dkt Mwigulu Nchemba akipokelewa na
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mh. John Mongela mara baada ya kuwasili uwanja wa
CCM Kirumba,tayari kwa kuzindua tamasha la pasaka kwa mara ya kwanza
chini ya Kampuni ya Msama Promotions Ltd sambamba na uzinduzi wa albamu
ya Muimbaji nyota wa muziki wa Injili Rose Muhanda iitwaya 'Usife Moyo'
yenye jumla ya nyimbo saba.
Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakifuatilia yaliyokuwa
yakijiri katika tamasha la pasaka mapema jana jioni ndani ya uwanja wa
CCM
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Angelina Mabula
akimtunza muimbaji wa nyimbo za injili Christopher Mwahangila mapema
jana jioni ndani ya tamasha la pasaka.
Waziri Wa mambo ya ndani Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba
amewasihi viongozi mbalimbali wa dini nchini wakiwemo Maaskofu na
Mashekh kutumia muda wao mwingi kwa kutembelea mikoa mbalimbali nchini
kunapotokea zaidi matukio ya kikatili ikiwemo mauaji ili kuhubiri injili
wananchi wawe na hofu na Mungu jambo litakalopelekea kupunguza ukatili
na watu kumjua Mungu.
Dkt Nchemba ameyasema hayo Wakati akimuwakilisha Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu alipokuwa
akihutubia mamia ya waumini kwenye Tamasha La muziki Wa Injili
lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ambayo huratibu matamasha
hayo kila mwaka.
Dkt Mwigulu aliwasihi wananchi kwa mshikamano na wingi wao
Kuendelea kumuombea Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Dkt
John Pombe Magufuli kwani anafanya kazi kubwa katika kuwatumikia
watanzania ikiwa ni pamoja na usimamizi mzuri Wa Rasilimali za Taifa
ambazo amekusudia kuwanufaisha watanzania wote kupitia uchumi
fungamanishi.
Alisema nia na Dira ya Rais Magufuli ni msisitizo mkubwa Wa
umuhimu Wa maslahi kwa watanzania huku akiwasihi maaskofu Wa makanisa
yote nchini kuendelea kueneza neno la Mungu kwani matukio yanayotokea ya
mauaji yanasababishwa na wananchi kutomjua Mungu kwa kufanya imani za
kishirikiana na ukatili kwa watoto, ubakaji wa wanawake, ulawiti,
unyanyasaji wa wazee na wananchi wengi kwa ujumla wake.
Katika tamasha hilo Dkt Mwigulu pia Amezindua albamu ya
Msanii nguli Wa nyimbo za injili nchini Tanzania Bi Rose Muhando
ijulikanayo kama USIVUNJIKE MOYO na kununua albamu hiyo kwa Shilingi
500,000 huku tamasha hilo likichagizwa na waimbaji 17 Wa ndani na nje ya
nchi.
Akijibu risala ya Kampuni ya Msama Promotion kuhusu wizi Wa
kazi za wasanii, Mhe Mwigulu alisema kuwa serikali inatambua kadhia hiyo
inayowakumba wasanii Wa dini nchini hivyo atawasiliana na Wizara ya
Habari, sanaa, utamaduni na Michezo ili kuweka msisitizo katika kuratibu
shughuli ya kuepusha wizi Wa wasanii.
Awali akisoma risala ya kampuni ya Msama Promotion Askofu
Zenobiasi Sisaya Wa kanisa la Filadephia, alisema kuwa Watanzania kwa
umoja wao wanapaswa kudumisha amani na mshikamano ambapo pia amesisitiza
serikali kupigia chepuo kwa kuzitambua kazi za wasanii na kuwatia
nguvuni wale wote wanaochakachua kazi za wasanii.
Alisema kuwa hali hiyo inawafanya wasanii wanaotumia kazi
kubwa kiakili na kimwili kutengeneza kazi hizo lakini pasina kuwa na
faida kwao kwani wezi hao wanazalisha kazi nyingi ambazo zipo chini ya
kiwango na hatimaye kulikosesha faida Taifa kwa kutolipa kodi.
Aliiomba serikali kupitia Wizara ya mambo ya ndani ya nchi
na Wizara ya Habari, sanaa, utamaduni na Michezo kuwachukulia hatua za
haraka wezi Wa kazi hizo za wasanii kupitia wakuu Wa wilaya na mikoa
kufanya msako endelevu kwa wote wanaofanya jukumu hilo.
Dhifa hiyo ya Tamasha la Pasaka imehudhuriwa pia na Mkuu Wa
Mkoa Wa Mwanza Mhe John Mongela, Naibu waziri Wa Wizara ya ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula ambaye pia ni Mbunge Wa
Jimbo la Ilemela, Maaskofu Wa makanisa mbalimbali nchini sambamba na
Mbunge Wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu.
Mgeni Rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba na
Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion wakizindua albam ya mwimbaji
Rose Muhando inayojulikana kwa jina la “Usife Moyo” kwenye Tamasha la
Pasaka lililofanyika jana jioni kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza ambapo waimbaji mbalimbali wa injili wameshiriki katika tamasha
hilo.
Dk Mwigulu akimpongeza Rose Muhando mara baada ya kuizindua
albamu yake iliyosheni nyimbo kazi nzuri alioifanya ya utunzi wa nyimbo
zenye kuielimisha jamii katika nyanja.
Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili Rose Muhanda akiimba moja
ya wimbo wake mpya uliomo kwenye albamu yake mpya ya 'Usife Moyo'
uitwao 'lazima wakae 'mbele ya umati wa wakazi wa jiji la Mwanza
waliojitokeza kwa wingi, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Mambo ya
Ndani Dkt Mwigulu Nchemba.
No comments:
Post a Comment