Sunday, July 07, 2013

BABU CHA MIAKA 92 AFUNGA NDOA NA BINTI ALIYEMZIDI MIAKA 70...!!!

 
Musali Mohammed al-Mujamaie (kulia) akiwa na mkewe, Muna Mukhlif al-Juburi.
Mkulima mmoja nchini Irak mwenye miaka 92 amemuoa mwanamke waliyetofautiana miaka 70 katika ndoa tatu kwa mpigo sambamba na wajukuu zake wa kiume wawili.

Musali Mohammed al-Mujamaie alimuoa mke mwenye umri wa miaka 22, Muna Mukhlif al-Juburi katika sherehe iliyodumu kwa masaa manne.

Wajukuu zake wa kiume, wenye umri wa miaka 16 na 17, nao walifunga ndoa kwenye sherehe hiyo iliyofanyika kaskazini mwa Baghdad Alhamisi iliyopita, kwa mujibu wa ripoti.

Mzee Mujamaie alisema kwenye siku hiyo maalum alikuwa akisubiria kwa muda mrefu kutokana na harusi za wajukuu zake kuwa zinaahirishwa mara kadhaa ili aweze kuunganisha na sherehe yake.

TBS YAPIGA MARUFUKU UUZWAJI WA MAFUTA YA KUPIKIA YA 'OKI'.....WADAI YANA MADHARA KIAFYA.

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/OKI.jpg 
Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limebaini kuwa mafuta ya kula aina ya Oki na Viking yaliyoenea sokoni nchini, yamebainika kuwa hayafai kwa matumizi ya binadamu.
Kwa mujibu wa TBS, vipimo vyote vitatu vilivyotumika kuyapima kuonyesha ubora, vimefeli na vimeonyesha mafuta hayo kuharibika kwa haraka tangu yalipotengenezwa na mpaka leo.
Pamoja na Oki, mafuta mengine yenye walakini ni Asma, Vikingi, Partiner na Premier Gold ambayo huuzwa kwa dumu lenye ujazo wa lita 20 kwa bei ya kuanzia Sh 38,000 hadi 45,000, wakati bei ya mafuta ya kula yanayotengenezwa nchini kwa ujazo huo huuzwa kati ya Sh. 52,000 na Sh.55,000.

Baada ya kupimwa, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora TBS, Lazaro Msasalaga, anasema ilithibitika kuwa mafuta ya Oki yanayozalishwa Malaysia na kupakiwa Singapore hayana ubora.
Alisema mafuta hayo yametengenezwa 2011 na kuonyesha mwisho wa kutumika ni Oktoba mwaka huu. Msasalaga alisema walipoyachunguza wamebaini hayana namba ya ufuatiliaji wakati suala hilo ni la muhimu kuwekwa.
Isitoshe, wawalipoyapima kutoka kipimo kimoja kwenda kingine, majibu yake yalishindwa na kuzidi kuonyesha mafuta hayo kuharibika kila walipoyapima.
Alisema kuna vipimo vya maabara ukipima vinaeleza mafuta kama yanafaa kutumika lakini kipimo hicho hakikufanikiwa.NA TALK BONGO

LUCY KOMBA NA IRENE UWOYA NDANI YA BIFU ZITO, KISA NDIKUMANA...!!!

 
MWANAFUNZI na mwalimu wake katika sanaa, Irene Uwoya na Lucy Komba wameingia katika bifu zito chanzo kikidaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumzunguka mwanafunzi wake kwa mumewe, Hamad Ndikumana ‘Katauti’. Lucy ambaye ndiye mwalimu wa Uwoya kisanaa, imedaiwa kuwa amemzunguka Uwoya kwa mumewe, Ndiku kwa kisingizio cha kucheza naye filamu iliyofahamika kwa jina la Kwa nini Nisimuoe?
 
“Kimenuka! Lucy Komba amemhadaa Ndiku, akazuga kuigiza naye filamu moja ndipo walipozama kwenye ukaribu kwelikweli.
“Mbaya zaidi filamu yenyewe wameigiza wahusika wawili tu (Lucy na Ndiku) mwanzo mwisho kule Tegeta. Sasa wewe unafikiri kuna nini hapo kama siyo mapenzi?’’ kilihoji chanzo hicho makini.
Baada ya paparazi wetu kuyanasa madai hayo, Jumatano iliyopita alimtafuta Uwoya kwa njia ya simu ambapo alipopewa taarifa hizo, alionesha kushtuka na kuchanganyikiwa mumewe kuigiza filamu moja na Lucy, alikata simu kisha baadaye akampigia paparazi yeye.
“Kuna wakati nilikuwa namtafuta Ndiku sijui alipo kumbe alikuwa na Lucy, sawa lakini kama Lucy ameamua kunifundisha mimi na sasa amemfundisha mume wangu sawa, tupo hapa!”
Paparazi wetu alihamishia majeshi kwa kumtwangia ‘mtuhumiwa’, Lucy ambaye alitiririka kama ifuatavyo:
 
“Nilijua Uwoya akisikia itakuwa ni balaa maana siku za nyuma niliwahi kumshutumu kutoka na mzazi mwenzangu (Patrick Mbasha) lakini mimi nipo tayari kwa lolote!”
Lucy Komba ndiye aliyemuingiza Uwoya kwenye sanaa baada ya kumchezesha Filamu ya Yolanda ambayo ndiyo iliyomtambulisha vyema staa huyo kisha kuliteka soko la sinema Bongo.

SERIKALI YA AFRIKA YA KUSINI YAKANA MZEE NELSON MANDELA KUWA HANA FAHAMU

Former South Africa's President Nelson Mandela is pictured during an interview with the media at is house in Qunu, South Africa,18 July 2008. Mandela, the anti-apartheid icon spend his 90th birthday at home in Qunu with his family, and the whole village is celebrating EPA/THEMBA HADEBE

SERIKALI ya Afrika Kusini imekanusha taarifa kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela, hana fahamu zake tena kama inavyoelezwa katika nyaraka za mahakama zilizowasilishwa mnamo 26.06.2013. 

Kifungu kinachoelezea hali mbaya ya Mandela kilitumika katika nyaraka za mahakama zilizowasilishwa na jamaa wa familia ya Mandela, kwa mujibu wa wakili aliyenukuliwa na vyombo vya habari. Ofisi ya rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ilisema madaktari wanakana rais huyo wa zamani amepoteza kabisa fahamu na hali hiyo haitabadilika. 
Zuma alisema jana mchana baada ya kumtembelea hospitalini kuwa Madiba anapewa matibabu ya hali ya juu na timu ya madaktari bingwa waliobobea katika taaluma ya utabibu, ambao wako kando ya kitanda chake hospitalini kila wakati.
Nyaraka za mahakama zilizopatikana na shirika la habari la AFP zinaonyesha madaktari wanaomtibu Mandela walisema hana fahamu na kuishauri familia wiki moja iliyopita iruhusu mashine zinazomsaidia kuishi zizimwe ili apumzike.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 7, 2013

.



.
.

MFANYABIAS​HARA MWENYE ASILI YA KIARABU MBARONI KWA KUMBAKA TAHIRA


Na Cresensia Kapinga,Songea.
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamshikiria mfanyabiashara mmoja Jamali Nassoro (67) mwenye asili ya kiarabu mkazi wa eneo la Making'inda katika manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito wa mimba ya miezi 5 msichana mwenye umri wa miaka 27 ambaye anadaiwa kuwa na ugonjwa wa utindio wa ubongo(TAILA) ambaye jina lake tunalo limehifadhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma George Chiposi alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo mwenye asili ya kiarabu limetokea hivi karibuni baada ya wazazi wa msichana kubaini kuwa mtoto wao yupo tofauti kimaumbile na kuchukuwa jukumu la kwenda kumpima ambako vipimo vilionesha kuwa ni mjamzito wa miezi 5.

Chiposi alisema kuwa wazazi wa msichana huyo baada ya kubaini mtoto wao ni mjamzito walimuhoji ili kujuwa ni nani aliyemfanyia unyama huo ambapo licha ya kuwa msichana huyo ni tahira alieleza kwa shida kuwa alikamatwa kwa nguvu na kulazimishwa kutoa nguo yake ya ndani na Nassoro ambaye alimtaka ampelekee maji ya kuoga chumbani kwake.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...