Sunday, July 07, 2013

BABU CHA MIAKA 92 AFUNGA NDOA NA BINTI ALIYEMZIDI MIAKA 70...!!!

 
Musali Mohammed al-Mujamaie (kulia) akiwa na mkewe, Muna Mukhlif al-Juburi.
Mkulima mmoja nchini Irak mwenye miaka 92 amemuoa mwanamke waliyetofautiana miaka 70 katika ndoa tatu kwa mpigo sambamba na wajukuu zake wa kiume wawili.

Musali Mohammed al-Mujamaie alimuoa mke mwenye umri wa miaka 22, Muna Mukhlif al-Juburi katika sherehe iliyodumu kwa masaa manne.

Wajukuu zake wa kiume, wenye umri wa miaka 16 na 17, nao walifunga ndoa kwenye sherehe hiyo iliyofanyika kaskazini mwa Baghdad Alhamisi iliyopita, kwa mujibu wa ripoti.

Mzee Mujamaie alisema kwenye siku hiyo maalum alikuwa akisubiria kwa muda mrefu kutokana na harusi za wajukuu zake kuwa zinaahirishwa mara kadhaa ili aweze kuunganisha na sherehe yake.


Alieleza: "Nina furaha sana kuoa pamoja na wajukuu zangu," Mzee Mujamaie alisema baada ya sherehe hiyo ya masaa manne. "Najihisi kama mwenye umri wa miaka 20!"
Mzee Mujamaie aliwalea watoto wake 16 kwenye nyumba yake iliyoko kijiji cha Gubban akiwa na mke wake wa kwanza, ambaye amezikwa kusini mwa mji wa Samarra ulioko katikati ya Irak.

Ndoa yake ya pili imekuja miaka mitatu baada ya mkewe kufariki.

Sherehe hiyo ya masaa manne ilijumuisha muziki na usakataji dansi na upigaji bunduki za kusherehekea.
Viongozi wa kijadi na kidini walihudhuria sherehe hizo tatu.
 
NA ZIRRO BLOG

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...