Sunday, July 07, 2013

MFANYABIAS​HARA MWENYE ASILI YA KIARABU MBARONI KWA KUMBAKA TAHIRA


Na Cresensia Kapinga,Songea.
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamshikiria mfanyabiashara mmoja Jamali Nassoro (67) mwenye asili ya kiarabu mkazi wa eneo la Making'inda katika manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito wa mimba ya miezi 5 msichana mwenye umri wa miaka 27 ambaye anadaiwa kuwa na ugonjwa wa utindio wa ubongo(TAILA) ambaye jina lake tunalo limehifadhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma George Chiposi alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo mwenye asili ya kiarabu limetokea hivi karibuni baada ya wazazi wa msichana kubaini kuwa mtoto wao yupo tofauti kimaumbile na kuchukuwa jukumu la kwenda kumpima ambako vipimo vilionesha kuwa ni mjamzito wa miezi 5.

Chiposi alisema kuwa wazazi wa msichana huyo baada ya kubaini mtoto wao ni mjamzito walimuhoji ili kujuwa ni nani aliyemfanyia unyama huo ambapo licha ya kuwa msichana huyo ni tahira alieleza kwa shida kuwa alikamatwa kwa nguvu na kulazimishwa kutoa nguo yake ya ndani na Nassoro ambaye alimtaka ampelekee maji ya kuoga chumbani kwake.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...