Saturday, October 28, 2017

TAZAMA PICHA ZA MAFURIKO YALIYOATHIRI MAKAZI YA WATU DAR ES SALAAM

Mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha maeneo mengi pwani ya Tanzania imesababisha mafuriko na uharibifu mkubwa.

Katika eneo la Mji Mpya, Kawe, nyumba zimebomoka na baadhi ya maeneo hayapitiki. Nyumba zaidi ya 20 zimeharibiwa vibaya na mafuriko.

Hizi hapa ni baadhi ya picha za hali ilivyo mtaani humo.

WALIOMUINGIZA MTU MWEUSI KWENYE JENEZA AKIWA HAI WAFUNGWA

Wakulima wawili wa Afrika Kusini waliomlazimisha mtu mweusi kuingia katika jeneza akiwa hai wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.

Theo Martins na Willem Oosthuizen walihukumiwa mnamo mwezi Agosti kwa jaribio la mauaji na utekaji nyara.

Walimtuhumu Victor Mlotshwa kwa kupita katika ardhi, wakamshambulia na kumlazimisha kuingia katika jeneza na kutishia kumchoma akiwa hai.


Kesi hiyo ilizua hisia nchini Afrika Kusini na kuangazia wasiwasi wa ubaguzi wa rangi katika jamii kadhaa za wakulima.

Friday, October 27, 2017

IDADI YA WALIOPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA MARUDIO NCHINI KENYA UTATA MTUPU

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati amesema wanakadiria kwamba idadi ya waliojitokeza kupiga kura jana kufikia wakati wa kufungwa kwa vituo saa kumi na moja jioni ni asilimia 48.

Akihutubia wanahabari, mwenyekiti huyo amesema vituo 87 kati ya vituo vyote vya kupigia kura vilifunguliwa, ambavyo ni vituo 35,564.

Kati ya vituo hivyo, fomu za matokeo kutoka kwa fomu za matokeo kutoka kwa fomu 27,124 zimepokelewa.

"Vituo 5,389 ambavyo vimetapakaa kote nchini havikufunguliwa. Baadhi vimo katika kaunti nne ambazo nilitangaza awali kwamba uchaguzi umeahirishwa," amesema.

VIDEO: RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

Rais John Magufuli amemteua aliyekuwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, huku aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu akiteuliwa kuwa balozi.

Dk. Kashilillah ameteuliwa ikiwa ni takriban wiki tatu kupita tangu alipoondolewa katika wadhifa wa Katibu wa Bunge, nafasi iliyochukuliwa na Stephen Kigaigai.
Rais Magufuli Mei 28,2017 alitengua uteuzi wa IGP Mangu na kumteua Simon Sirro kushika wadhifa huo. Mangu anasubiri kupangiwa kituo cha kazi pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dk Aziz Mlima.

Monday, October 23, 2017

USHAHIDI ALIOUTOA LULU MAHAKAMANI KUHUSU KIFO CHA KANUMBA

Msanii wa filamu, Elizabeth Michael (22) amejitetea katika kesi ya kuuwa bila kukusudia katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Katika utetezi wake, Lulu amesema anakumbuka siku ya tukio ilikuwa Ijumaa ya April 6, 2012 ambapo aliahidiana na rafiki zake kwamba wangetoka usiku.

Amesema kuwa asubuhi ya siku hiyo alienda kuonana na rafiki zake maeneo ya Mikocheni, ambapo pia alikuwa akiwasiliana na Kanumba.

"Marehemu alikuwa ni msanii mwenzangu lakini pia nilikuwa naye na mahusiano naye ya kimapenzi,".

Lulu alisema kuwa marehemu Kanumba alikuwa hapendi kumuona akitoka, hivyo hadi siku ya tukio hakutaka kumwambia kwamba atatoka na rafiki zake.

Sunday, October 08, 2017

KIM JONG-UN AMPANDISHA CHEO DADA YAKE

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amempandisha cheo dada yake mdogo, na kumpa madaraka zaidi katika chama tawala cha wafanyakazi.

Kim Yo-jong, anayeaminika kuwa na umri wa zaidi ya miaka 26 amekuwa mjumbe katika kamati kuu ya chama, ambalo ni baraza kuu la uamuzi linalojulikana kama politburo.

Bi Kim Yo-jong alipewa kwanza wadhifa wa kuwa afisa wa wa cheo cha juu wa chama, miaka mitatu iliyopita.

Familia ya Kim, imeongoza Korea Kaskazini, tangu nchi hiyo ilipoundwa, mwaka wa 1948.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 08, 2017 YA MICHEZO, DINI NA HARDNEWS





POLISI YADAI PANYA NDIO WALIOKULA MADAWA YA KULEVYA YALIYOKAMATWA

Police katika mji wa Mumbai nchini India wanawalaumu panya kwa kutoweka kwa kilo 34 za dawa za kulevya kwa jina Ketamine.

Wanasema wanawatuhumu panya hao kwamba ndio wa kulaumiwa baada ya kupata mabagi hayo yalitobolewa kwa chini.

Uchunguzi wa miaka mitatu umekamilika kwamba iwapo ingekuwa binadamu wangechukua mabagi yote.

Dawa hizo zilizohifadhiwa katika ghala moja la serikali zilikuwa miongoni mwa kilo 200 za mihadarati zilizopatikana na walanguzi wa mihadarati 2011.

Hii sio mara ya kwanza kwa maafisa wa polisi nchini India kuwalaumu panya kwa kutoweka kwa mihadarati iliokamatwa.

Saturday, October 07, 2017

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI





'KUNA UWEZEKANO WA KUFANYIKA MAPINDUZI NCHINI ZIMBABWE' GRACE MUGABE

Mke wa rais Robert Mugabe, Grace Mugabe ameonya kwamba kuna uwezekano wa kufanyika kwa mapinduzi huku kukiwa kuna wasiwasi mkubwa nchini humo kuhusu harakati za kumrithi rais Mugabe.

Anasema kuwa washirika wa makamu wa rais Emmerson Mnangangwa wanatishia maisha ya wale ambao hawamuungi mkono kumrithi rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93.

Bi Mugabe yeye binafsi na bwana Mnangagwa wako kifua mbele na uadui wao umekigawanya chama tawala cha Zanu PF .

Mgogoro huo unajiri baada ya bwana Mgangagwa kudai kwamba aliwekewa sumu katika chakula chake mwezi Agosti.

Wafuasi wake wamesema kuwa wapinzani wake ndani ya Zanu PF ndio wakulaumiwa, ijapokuwa bwana Mnangagwa amejitenga na madai kama hayo.

Alikiambia chombo cha habari cha taifa hilo anasalia kuwa mtiifu kwa rais Mugabe.

Bi Grace Mugabe aliyekasirika alimshutumu bwana Mnangagwa katika hafla moja mjini Harare.

''Tunatishiwa usiku na mchana kwamba iwapo mtu fulani hatokuwa rais , tutauawa'', alisema.

MAREKANI YAIONDOLEA VIKWAZO SUDAN

Marekani imeiondolea vikwazo Sudan ikisema taifa hilo la Afrika lilikuwa limeanza kuangazia maswala kuhusu kukabiliana na ugaidi pamoja na ukiukeaji wa haki za kibinaadamu dhidi ya raia wanaoishi katika jimbo la Darfur.

Uamuzi wa kuiondolea vikwazo na kusitisha vikwazo vya kiuchumi wa taifa hilo unajiri baada ya utawala wa Trump mwezi uliopita kuliondoa taifa hilo katika mataifa ambayo raia wake wamewekwa vikwazo vya kusafiri.

Sudan ndio taifa la pekee ambalo liliondolewa katika orodha hiyo. Lakini uamuzi huo unaviacha vikwazo vingine kuendelea kwa sasa ikiwemo vile dhidi ya watu binafsi walio na agizo la kukamtwa kufuatia unyanyasaji uliofanyika katika eneo la Darfur.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...