Friday, October 27, 2017

IDADI YA WALIOPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA MARUDIO NCHINI KENYA UTATA MTUPU

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati amesema wanakadiria kwamba idadi ya waliojitokeza kupiga kura jana kufikia wakati wa kufungwa kwa vituo saa kumi na moja jioni ni asilimia 48.

Akihutubia wanahabari, mwenyekiti huyo amesema vituo 87 kati ya vituo vyote vya kupigia kura vilifunguliwa, ambavyo ni vituo 35,564.

Kati ya vituo hivyo, fomu za matokeo kutoka kwa fomu za matokeo kutoka kwa fomu 27,124 zimepokelewa.

"Vituo 5,389 ambavyo vimetapakaa kote nchini havikufunguliwa. Baadhi vimo katika kaunti nne ambazo nilitangaza awali kwamba uchaguzi umeahirishwa," amesema.

Chebukati amesema vituo kamili vilivyoathiriwa vitatangwa leo katika gazeti rasmi la serikali.

Baadhi ya watu wameshutumu tarehe mpya ya uchaguzi iliyotangazwa na Chebukati wakisema Jumamosi ni siku ya ibada kwa waumini wa kanisa la Kiadventisti ambao ni wengi katika kaunti ambazo uchaguzi umeahirishwa.

Chebukati hata hivyo amesema walizingatia mambo mengi kabla ya kutangaza tarehe mpya.

"Matokeo ya uchaguzi ni lazima yatangazwe katika siku saba. Lazima tujinyime baadhi ya mambo. Wasiotaka kupiga kura hawatalazimishwa," amesema.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...