Mwanariadha bingwa wa mbio kwa walemavu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya mpenzi wake kwa kumpiga risasi Oscar Pistorius amekubaliwa kupewa dhamana.
Wakati wa kusikiliza maombi ya awali ya dhamana hiyo hapo jana, Hakimu wa mahakama ya Pretoria ameweka wazi kuwa hakuna aliyemtilia shaka kuwa atakimbia wala kuwa ana tabia hatarishi.
Pistorius amekana mashitaka ya mauji, akisema alimpiga risasi Reeva Steenkamp akidhani ni mvamizi aliyeingia katika nyumba yake.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena tarehe 4 mwezi wa 6 mwaka hu.
Pistorius amekaa katika sero ya polisi mjini Pretoria tangu alipokamatwa mnamo February 14, 2013.