Tuesday, December 10, 2013

'BABU SEYA, PAPII LAZIMA WATAACHIWA HURU TU'


Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.
NGUZA Mbangu, mtoto mkubwa wa mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya, amesema mzazi wake pamoja na mdogo wake, Papii, ni lazima wataachiwa huru hivi karibuni.

Mbangu, ambaye pia hufahamika kisanii kama Mashine, ambaye hivi sasa ni mwinjilisti, alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipozungumza na gazeti la Uwazi, akisema kuwa kutolewa jela kwa ndugu zake hao, kutawafanya Watanzania kumsujudia Mungu kupitia tukio hilo.

“Amini nakuambia, Mungu amenipa maono, Babu Seya na Papii wako huru, watatoka tu, kinachosubiriwa ni muda tu ambao hauko mbali, ni lazima watatoka kwa sababu hawana hatia,” alisema Mbangu, ambaye pia alihukumiwa kifungo cha maisha jela kama mzazi wake, lakini akaachiwa wakati walipokata rufaa kwa mara ya kwanza mahakamani.

JIONEE PICHA ZAIDI YA 200 ZA IBADA YA KUMUOMBEA MANDELA INAVYOENDELEA IKIWAMO NA MARAIS NA VIONGOZI WALIOWASILI

Sombre occasion: Members of Nelson Mandela's family take their seats amid heavy rain ahead of his memorial service at the FNB Stadium in Soweto, near Johannesburg

Respect: Nelson Mandela is shown on a giant screen inside the stadium as thousands of South Africans and global dignitaries file into the ground

NORA AFUNGUKA KUHUSU RAY ADAI ALIMTONGOZA. MSIKILIZE HAPA..!!!

Muigizaji wa kike aliyefanya vizuri kupitia kundi la Kaole Sanaa Group, Nuru Nassoro aka Nora amedai kuwa amekuwa akifanyiwa fitina na muigizaji mwenzake Vicent Kigosi aka Ray kwa kuwa aliwahi kumtaka kimapenzi akamkataa.
  
Nora amefunguka kupitia kipindi cha Filamonata cha 100.5 Times Fm na kudai kuwa Ray amekuwa akimbania hata kwenye baadhi ya makampuni ambayo anapeleka kazi zake.
 
Mpaka kwenye kampuni ambayo nimepeleka kazi nimeshawahi kusikia wanasema, wakaniahidi sana mpaka nikawakubalia walichokuwa wanataka wao. Lakini yeye (Ray) alitanguliza movies zake, akasema ana movie zake sijui kitu gani..” amelalamika Nora.
 
Ameeleza kuwa Ray amewahi kumbania kufanya kazi na marehemu Kanumba, na hata Mtitu sababu ikiwa ile ile kumkataa kimapenzi.

WINNIE MANDELA NA GRACA MACHEL WAKUTANA MSIBANI, MARAIS ZAIDI YA 90 KUHUDHURIA MAZISHI.... R.I.P MANDELA


Marais zaidi ya 90 wa nchi mbalimbali duniani akiwemo Barack Obama wa Marekani ni miongoni mwa maelfu ya waliojitokeza Johannesburg South Africa kwenye uwanja wa soka wa FNB leo kumuaga Mzee Mandela anaetarajiwa kuzikwa Jumapili ijayo December 15 2013.
madiba 9
Serikali ya Afrika Kusini imeimarisha ulinzi kwa kutumia vikosi vyake vya jeshi vyenye ulinzi wa hali ya juu ambapo sniper team ni miongoni mwa wanaohusika na ulinzi kwenye eneo lote la kiwanja anakoagiwa Mzee Mandela huku helicopter pamoja na ndege za kijeshi zikipita angani mara kwa mara.

ANGALIA PICHA ZA BIRTHDAY PARTY YA NICK MINAJ, BONGE LA KEKI...!!!


First lady wa label ya YMCMB Nicki Minaj amesherehekea birthday yake ya kutimiza miaka 31 na mafanikio ya kujivunia kwenye kazi yake ya muziki ambapo party ilifanyika huko L.A na Restaurant nzima ilibadilika rangi yake na kuwa ya pink maalum kwa ajili ya party ya Minaj ambayo ilihudhuriwa na Lil Twist, Safaree boyfriend wa Nicki Minaj na watu wengine.
nicki-minaj-birthday-5nicki-minaj-birthday-3

YAFAHAMU MAAJABU 10 YA MSIBA WA MANDELA...!!!

RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela, mweusi wa kwanza kushika wadhifa huo katika taifa lenye uwezo mkubwa kiuchumi na kijeshi barani Afrika, alifariki dunia Alhamisi iliyopita akiwa nyumbani kwake jijini Johannesburg.
Kifo chake kimeushtua ulimwengu na kwa mara ya kwanza katika historia, dunia nzima imesimama nyuma ya jemedari huyo, kila mmoja akionesha masikitiko yake. Wakati dunia ikisubiri mazishi yake ambayo pia yatavunja rekodi ya mazishi yote yaliyowahi kufanywa tokea kuumbwa kwa uso wa dunia hapo Desemba 15 mwaka huu, Uwazi limebaini maajabu kumi yanayoambatana na msiba huo.

AIR FORCE ONE KUBEBA MARAIS WATANO WA MAREKANI
AIR Force One ni ndege inayombeba Rais wa Marekani aliye madarakani na kumpeleka popote duniani. Lakini katika hali ya kushangaza, Idara ya Usalama ya Marekani imetoa ruhusa kwa marais wastaafu wakiwa na wake zao, kuandamana na Rais Barak Obama kuhudhuria mazishi ya shujaa huyo wa dunia.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 10, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.


Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...