Friday, May 02, 2014

JK: MISHAHARA ITAPANDA NA KUPUNGUZWA KODI


Rais Jakaya Kikwete akiangua kicheko wakati walimu (juu), walipokuwa wakipita kwa maandamano, huku wakiimba ‘Shemeji mshahara bado’ wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) zilizofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana. Walimu walimwita shemeji kwa kuwa mkewe, Salma ni mwalimu kitaaluma. Picha na Silvan Kiwale. 
Dar/mikoani. Rais Jakaya Kikwete ametoa ahadi mbili za kuwafurahisha wafanyakazi. Kwanza ametangaza nia ya kuongeza mishahara yao na pili, kupunguza kodi inayokatwa kwenye mishahara hiyo mambo ambayo ameahidi kutekelezwa katika Bajeti ya mwaka 2014/2015 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema anatambua kuwa wafanyakazi wana hamu ya kujua Serikali itasema nini kuhusu masilahi yao.
Alisema malalamiko ya wafanyakazi wengi ni kutaka kuona kima cha chini cha mshahara kinaongezwa huku kodi kwenye mishahara (Paye), ikipungua.
“Mimi na wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira ya kufanya hivyo, tumethibitisha miaka iliyopita na tutaendelea kuwa hivyo,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Huku akishangiliwa na wafanyakazi waliofurika katika Uwanja wa Uhuru, Rais Kikwete alisema: “Najua kuwa nyongeza tuliyotoa mwaka jana si kubwa kama wafanyakazi walivyotaka iwe... hata mimi nisingependa iwe hivyo.”

HII NDIO TAARIFA RASMI YA YANGA KUHUSU USAJILI WA DOMAYO NA KAVUMBAGU

Didier-Kavumbagu-na-Frank-Domayo-wakisaini-kuichezea-klabu-ya-Azam-FCUongozi wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha wanachama wake, wapenzi wa soka na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa wachezai wake Didier Kavumbagu na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani walishakubaliana na uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba ramba.
Yanga tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba inayoendelea na kama kanuni za VPL kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu zitatumika wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi ndio watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba mwongozo kwa TFF juu ya taratibu zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya kuwasainisha Kavumbagu na Twite.
Awali uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji hao tangu mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014 juu ya kuongezewa muda wa mikataba yao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga kwa ajili msimu mpya ujao 2014/2015.
Didier Kavumbagu na Mbuyu Twite ambao mikataba yao ilikuwa mwishoni waliongea na uongozi tangu mapema mwaka jana mwezi wa Septemba juu ya kuweka sahihi zao na kuendelea kuitumikia Yanga na kukubaliana mambo yote ya msingi kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya usajili wa wachezaji wa kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la Bagamoyo linapaswa kuanza kutekelezwa msimu huu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 02, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

HAMAD RASHID KUGOMBEA URAIS 2015

Hamad_Rashid6_3bea3.jpg
Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed amesema anapanga kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha urais katika Uchaguzi Mkuu mwakani.
Akizungumza katika mahojiano maalumu hivi karibuni mjini Dodoma, Hamad Rashid alisema: “Kama Mwenyezi Mungu akinijalia uhai na uzima mwakani, ninatarajia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais ama wa Muungano au wa Zanzibar.

“Ila sijaamua kama ni Bara au Zanzibar; kama ni chama cha CUF au kingine, hayo yote yatakuja baadaye,” alisema Hamad Rashid.
Mohamed ambaye ana mgogoro mahakamani na chama chake cha CUF, ametoa kauli hiyo wakati tayari viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), CUF kikiwamo wanajipanga kusimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi ujao.
Mbali na CUF, vyama vingine vinavyounda Ukawa ni NCCR-Mageuzi na Chadema ambavyo pia vinakusudia kusimamisha mgombea mmoja kwa nafasi za ubunge na udiwani, lengo likiwa kukabiliana na nguvu ya chama tawala, CCM.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WATU 19 WAUAWA KATIKA MLIPUKO NIGERIA

Waliojeruhiwa walikimbizwa hosipitalini
Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa watu 19 wameuawa baada ya mlipuko kutokea katika kituo cha basi katika mji mkuu wa taifa hilo Abuja.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya kushughulikia mikasa na hali ya dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60 walijeruhiwa vibaya lakini sitaka kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Amesema kuwa magari sita yameharibiwa katika mlipuko huo.
Mlipuko huo umetokea katika eneo la Nyanya, karibu na kituo cha basi ambako zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi Aprili.
Ripoti za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari. Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa. Hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini Abuja
Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Lakini shambulizi la bomu la tarehe 14 Aprili lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...