Thursday, April 02, 2015

MWIGULU KUFUTA MAADHIMISHO MBALIMBALI YA KITAIFA...!!!

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba juzi alijikuta akitamka kuwa anakusudia kufuta maadhimisho mbalimbali ya kitaifa yanayotumika kama kichaka cha kutafuna fedha za Serikali baada ya wabunge  wa upinzani kuitoa jasho Serikali wakati wa kupitisha Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana wa mwaka 2015.
Mwigulu alitoa kauli hiyo pale alipoingilia kati mjadala huo, akiponda kitendo cha watumishi wa Serikali kutumia magari na fedha lukuki katika wiki za kuadhimisha kumbukumbu mbalimbali za kitaifa.
Kilichoibua mjadala huo ni suala la uanzishwaji wa Mfuko wa Vijana na maadhimisho ya wiki ya vijana ambayo imepangwa Oktoba kila mwaka. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRILI 02, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

TRENI DAR - KIGOMA KAMA NDEGE...!!!

 
 Mwonekano wa ndani ya treni ya kisasa ya abiria ya Kampuni ya TRL iliyozinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shabaan Mwinjaka, Dar es Salaam jana.

Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake ya saa 30 kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.
Kutokana na tofauti hiyo, abiria walioanza safari kwa furaha na matumaini jana saa tano asubuhi wanatarajiwa kufika Kigoma leo saa 11 jioni badala ya saa tano usiku.
Hata hivyo, abiria hao watalazimika kuingiza mikono yao zaidi mifukoni, kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa Sh79,400 badala ya Sh75,700 za awali kwa daraja la kwanza. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

RAIA WA YEMEN WAKIMBILIA SOMALIA

Raia wa Yemen wakikatika Ghuba ya Aden kwa boti ndogo
Mashirika ya umoja wa mataifa yamesema kuwa mamia ya raia wa Yemen wamevuka ghuba ya Aden kwa kutumia boti ndogo na kuingia nchini Somalia, Djibouti na Somaliland wakikimbia mapigano nchini mwao.

Shirika la umoja wa mataifa la UNHCR limesema kuwa linaangalia eneo zuri kwaajili ya kuweka kambi ya wakimbizi kwaajili ya raia hao. Wakati huo huo wakimbizi kutoka nchini Somalia bado wanaendelea kuingia nchini Yemen kuepuka njaa na machafuko nchini mwao.

Shirika hilo la UNHCR linasema kuwa Yemen inawahifadhi wakimbizi wapatao 238,000 kutoka Somalia. Mwandishi wa BBC Africa Mary Harper anasema wazo la Yemen kufikiria kuwa na kambi za wakimbizi nchini Somalia si la kawaida kwa kuwa ni kawaida kwa raia nchini humo kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya mara kwa mara hali ambayo haiwezi kuwa eneo zuri kwa wakimbizi kuhifadhiwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

BUHARI AAHIDI KUTOKOMEZA BOKO HARAM NIGERIA

Muhammadu Buhari, Rais mteule wa Nigeria
Rais mteule wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amezitaja vurugu zinazosababishwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwa ni tatizo kubwa linalokabili nchi.

Katika mahojiano maalumu na BBC, kiongozi huyo mstaafu wa jeshi amesema anatarajia kulishinda kundi hilo baada ya dhamira mpya kutoka jeshini na msaada wa nchi jirani.

 "Kwa ushirikiano na majirani zetu Cameroon, Chad, Niger na jumuia ya kimataifa na dhamira ambayo tutapata kutoka katika jeshi, Nafikiri itachukua muda mfupi zaidi kukabiliana nao."

Jenerali Buhari amesema tayari ameainisha msingi wa tatizo linalokabili nchi ya Nigeria, lakini amewataka raia wa nchi hiyo kuwa wavumilivu.

"Tumebaini matatizo makubwa matatu. Ambayo ni kukosekana kwa usalama nchini, tatizo ambalo kila mmoja analifahamu na lingine ni ukosefu wa ajira, hii ina maana uharibifu wa uchumi ikiwa ni kutokana na vitendo vya rushwa na rushwa yenyewe. 

Matatizo haya matatu makuu, Wanigeria wote wanafahamu na tunaomba ushirikiano wa wananchi wa Nigeria, wasitarajie miujiza kutokea katika kuyapatia ufumbuzi matatizo haya katika kipindi cha miezi michache baada ya kutwaa madaraka kwa sababu uharibifu umechukua miaka mingi, miaka kumi na sita ya utawala wa chama tawala cha nchi hii."

 Anasema rais huyo mteule wa Nigeria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...