Audrey amekuwa akitaka baraza la mitihani kubadili jina lake na utambulisho wake wa kijinsia
Mwanamke
aliyebadili jinsia yake ya kiume na kuwa mwanamke na kutaka jina lake
kubadilishwa kwenye cheti chake cha mtihani ameshinda kesi yake dhidi ya
baraza la kitaifa la mitihani nchini Kenya.
Mahakama imelazimisha
baraza hilo kumpa Adrey Mbugua cheti kipya kinachoonyesha hali yake
mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa anapokea matibabu ya kufanikisha jinsia
yake kubadilika kabisa. Bi Mbugua alilishitaki baraza la kitaifa
la mitihani nchini humo kwa kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia
yake kwenye cheti hicho kutoka kwa Mwanamme na kumtambua kama mwanamke
licha ya amri iliyotolewa katika gazeti rasmi la serikali. Jaji
Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku 45 kubadilisha jina la
Adrey katika cheti hicho kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na utambulisho wa
mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la 'Audrey Mbugua' bila ya
kuweka jinsia yoyote. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz