Monday, September 22, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 22, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MATOKEO YA LIGI KUU SOKA NCHINI ENGLAND JANA HAYA HAPA

article-2764265-218D921900000578-139_964x386
ENGLAND: Premier League  
05:30 Finished Leicester 5 – 3 Manchester United       
05:30 Finished Tottenham 0 – 1 West Brom      
08:00 Finished Everton 2 – 3 Crystal Palace      
08:00 Finished  Manchester City 1 – 1 Chelsea       

MANCHESTER UNITED YAPIGWA 5-3 BILA HURUMA

1411308209470_wps_84_Esteban_Cambiasso_of_Leic

Cambiasso akishangilia goli alilofunga dhidi ya Manchester United katika uwanja wa The King Power 
MANCHESTER United wakicheza ugenini wametandikwa  mabao 5-3 dhidi ya Leicester.
Magoli ya wenyeji yalifungwa na Ulloa (2), Nugent, Cambiasso na Vardy.
United walijipatia magoli yao kupitia kwa Van Persie, Di Maria na Herrera 
Radamel Falcao shakes hands with Manchester United captain Wayne Rooney and Ander Herrera before kick-off ahead of his first start for the club

Katika mechi nyingine iliyomalizika jana jioni, Tottenham wakiwa nyumbani wamepigwa 1-0 na West Brom.

Muda huu mechi mbili zinaendelea ambapo Everton wapo nyumbani kuivaa Crystal Palace, wakati Man City wanachuana na Chelsea katika uwanja wa Etihad. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SIMBA YABANWA MBAVU NA WAGOSI WA KAYA, YATOKA 2-2…!!!

MESSI1

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba wamelazimisha sare ya mabao 2-2- na Wagosi wa Kaya, Coastal Union katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania bara uliomalizika jana jioni uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Simba chini ya kocha Patrick Phiri walianza mpira wakilishambulia mara kadhaa lango la Coastal na katika dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza Mnyama aliandika bao la kuongoza kupitia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na kiungo mkongwe, Shaaban Kisiga ‘Malone’.
Katika kipindi hicho cha kwanza, Simba waliendelea kucheza vizuri kuanzia safu ya kiungo ambapo Piere Kwizera na Kisiga walionekana kupiga pasi za uhakika, lakini haikuwa rahisi kupasua ngome ya Coastal.
Mara kadhaa Singano na Chanongo walipiga krosi kutoka pande zote za kulia na kushoto, lakini Amissi Tambwe na Okwi walishindwa kukaa maeneo sahihi.
Mnamo dakika ya 36, Tambwe aliandika bao la pili kwa njia ya kichwa akiunganisha krosi iliyochongwa na Okwi kutoka  winga ya kulia na kumuacha kipa wa Coastal Union Shaaban Kado akiokota manyoya.
Dakika ya 56, Uhuru aliingia akitoke benchi kuchukua nafasi ya Haruna Chanongo.
Phiri alifanya mabadiliko ambapo katika dakika ya 64 Tambwe alikwenda benchi na  nafasi yake ilichukuliwa na Paul Kiongera. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...