Sunday, October 25, 2015

UCHAGUZI WAHAIRISHWA KWA KUKOSA KARATASI ZA UDIWANI


Wakati zoezi la upigaji kura likiendelea nchi nzima wakazi wa kata ya Matongo, jimbo la Bariadi, mkoani Simiyu wameshindwa kupiga kura kwa nafasi ya udiwani kwa kile kinachodaiwa uhaba wa karatasi za kupigia kura.

Akiongea na waandishi wa habari Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo Abdallah Malela amesema kukosekana kwa karatasi ndicho chanzo cha uchaguzi kwa ngazi ya udiwani kusitishwa katika eneo hilo.

Alisema kuwa kata hiyo ina jumla ya wapiga kura 7500, na vituo 17 lakini karatasi ambazo zimetoka Tume ya ucHaguzi zilikuwa 3400 tu, huku zaidi ya wapigakura 4100 wakikosa karatasi hizo za kupigia kura.

RPC ARUSHA AONYA WANAOTAKA KUFANYA VURUGU


Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas .

Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas amesema jeshi hilo limebaini vikundi vilivyojipanga kufanya vurugu na akavitaka kuacha kutekeleza mpango huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda Sabas alisema wamebaini kuwa zaidi ya vijana 100 wamesambazwa mjini Arusha na Arumeru kwa ajili ya kufanya vurugu wakati wa uchaguzi. 

Alisema polisi wamejipanga kukabiliana na uhalifu au vurugu zozote zitakazotokea katika kipindi cha uchaguzi kwa kuwa tayari wamepokea tetesi za kuwapo kwa makundi hayo. “Natoa onyo kwa hayo makundi kuwa kama wanataka usalama waache mara moja kwa kuwa hawatakuwa salama,” alisema Liberatus.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...