Tuesday, February 25, 2014

'ANAYEONA POSHO HAITOSHI AFUNGASHE VIRAGO'

bunge_4f64b.jpg
Wizara ya Fedha imepigilia msumari maombi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ya kutaka waongezewe posho na kusema anayeona ameacha kazi inayomlipa zaidi kwenda bungeni afungashe virago na kuondoka.
Msimamo huo umekuja siku moja tu baada ya gazeti hili kudokeza kuwa madai ya wajumbe wa bunge hilo kutaka waongezewe posho kutoka Sh300,000 za sasa kwa siku, yamegonga mwamba baada ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza uhalali wake kusema kiwango hicho kinatosha.
Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Kificho alisema jana bila kutaja viwango, kuwa ripoti ya kamati hiyo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi.
Madai ya wajumbe kutaka waongezewe posho, yamechafua hali ya hewa ndani na nje ya Bunge, huku baadhi ya wananchi wakipaza sauti zao na kumsihi Rais Kikwete alivunje bunge hilo iwapo wajumbe watashikilia msimamo wa kutaka nyongeza ya posho.
Jana, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema wanaoshiriki kutunga Katiba ni Watanzania na siyo wataalamu washauri waliokodiwa kutoka nje.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

NYALANDU APANGUA WAKURUGENZI MALIASILI


nyalandupx_745e8.jpg
Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amewaondoa katika nyadhifa zao, Wakurugenzi mbalimbali kwa sababu zilizoelezwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.
Hatua ya Nyalandu imekuja ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Bunge la Desemba 22, 2013 lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza.
Nyalandu alisema: "Namwondoa Prof Alexander Songorwa (Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori) na kumteua Paul Sarakikya kukaimu nafasi hiyo."


Alisema pia kuwa amemwondoa Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Profesa Jafari Kidegesho kwenye nafasi hiyo na Dk Charles Mulokozi ameteuliwa kushika wadhifa huo.
Mwingine aliyeteuliwa ni Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji-Ujangili, nafasi iliyoachwa wazi na Sarakikya wakati Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu, Nebbo Mwina anabaki kwenye nafasi yake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARI 25, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

. 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

KUANGALIA MECHI YA TWIGA STARS, ZAMBIA BURE

twiga star by mafoto1 97507
Washabiki wa mpira wa miguu nchini watashuhudia bure mechi ya timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) dhidi ya Zambia (Shepolopolo).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itachezwa Ijumaa (Februari 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili alasiri.
Twiga Stars ambayo ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Lusaka, Februari 14 mwaka huu kwa mabao 2-1 iko kambini chini ya Kocha Rogasian Kaijage na msaidizi wake Nasra Juma ikijiwinda kuwakabili Wazambia wanaotarajiwa kutua nchini Alhamisi (Februari 26 mwaka huu).
Waamuzi wa mechi hiyo Ines Niyonsaba, Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana na Suavis Iratunga kutoka Burundi kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa (Februari 26 mwaka huu). Kamishna Fran Hilton Smith kutoka Afrika Kusini yeye atatua nchini Februari 27 mwaka huu kwa ndege ya South Africa Airways. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 
 Chanzo: TFF

MILIPUKO YA MABOMU YARINDIMA Z'BAR

bomu_b1855.png
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi
Zanzibar. Watu wanne wamejeruhiwa baada ya milipuko minne inayoaminika kuwa ni mabomu kutokea katika maeneo matatu tofauti Zanzibar.
Katika moja ya matukio hayo, watu wanne walijeruhiwa, mmoja akikatika mguu, katika eneo la Unguja Ukuu, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Majeruhi wawili wamelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja.
Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Mkoa wa Kusini Unguja, Hamad Said Masoud alisema mlipuko wa kwanza ulitokea juzi katika eneo la Fuaoni Maili Nne wakati watu wasiojulikana waliporusha kitu kinachoaminika kuwa ni bomu wakati waumini wa Kanisa la Evangelist wakiendelea na ibada ya Jumapili.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame alisema tukio la juzi, kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kilirushwa wakati waumini wa kanisa hilo wakiendelea na ibada na kutoa mlipuko na kishindo kikubwa. Alisema wakati wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo, milipuko mingine mitatu ilitokea jana.
Katika mlipuko wa kwanza kwa jana uliotokea saa 6.30 mchana katika kituo kimoja cha fundi vyuma aliyetambulika kwa jina la Juma Abdallah huko Unguja Ukuu ndiko kulikokuwa na watu waliojeruhiwa.
Waliojeruhiwa katika tukio hilo ni Pandu Haji Pandu aliyekatika mguu na Shaaban Khamis Ibrahim ambaye aliumia sehemu za kiuno.
Hamad alisema mtu mmoja aliokota chuma kizito na kukipeleka kwa fundi akitaka atengenezewe nanga kwa ajili ya uvuvi.
Alisema mhunzi huyo alipokea kazi hiyo na alipokuwa akijiandaa kwa matengenezo ndipo mlipuko huo ulipotokea. Mlipuko huo ulitokea sambamba na mwingine katika Mgahawa wa Mercury's uliopo Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi na kusababisha huduma za chakula kusitishwa kwa muda.
Tukio la mwisho lilikuwa saa 7:15 mchana katika Kanisa la Anglikana, Mkunazini. Katibu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Zanzibar, Nuhu Saranya alisema: "Nilisikia kishindo cha mlipuko, wakati nikitafakari ni kitu gani hicho, nikasikia mlipuko wa pili nje ya kanisa letu," alisema.
Mmoja wa majeruhi, Mohamed Ibrahim alisema hakujua kilichotokea huku akilalamika kuwa masikio yake hayasikii vizuri kutokana na kishindo hicho.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...