Tuesday, June 25, 2013

KAJALA AKUNUSHA KUHUSU KUGOMBANA NA WEMA SEPETU


Baada ya siku chache za magazeti ya udaku nchini kuripoti kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa karibu sana kati ya mwanadada Wema sepetu na Muigizaji mwenzake Kajala masanja, tuliamua kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wa suala hili ili tusije kuipotosha jamii kwa habari za zisizo na ushahidi wowote.


Katika habari iliyoripotiwa na blogs na magazeti kadhaa ya udaku kuhusu kuvunjika kwa uhusiano huo zilisema kuwa chanzo ni vitendo vya mwanadada wema Sepetu “kumbania” Kajala kwenye dili anzopata za kucheza filamu na hasahasa kumkosesha dili ya kwenda china kufanya filamu aliyoalikwa na watanzania waishio nchini humo.

Bongomovies.com tuliamua kuwatafuta hewani wasanii hawa ili tuweze kupata ukweli wa jambo hili na mwanadada Kajala alikuwa wa kwanza kupokea simu na alikanusha vikali habari hizo na kuwashangaa wanaoziandika wanazipata wapi.

“Unajua mi nashangaa sana watu wanatoa wapi maneno wanayoandika, mimi sina tatizo na Wema, wala siwezi kuwa na tatizo naye, wema amekuwa msaada mkubwa kwangu, sa sijui nitagombana nini na wema, huo ni uzushi tuu jamani, muwe mnatuuliza kabla ya kuandika” Alisema kajala

Alipoulizwa kuhusu ukaribu wake mpya na wolper alisema
“Wolper nimekutana naye kwenye party ndo tukaamua kupiga picha, au siku hizi sitakiwi kupiga picha na mtu mwingine zaidi ya wema? Wolper ni rafiki yangu” Alisisitiza Kajala

 Tulipojaribu kumtafuta wema simu yake ilikuwa haipokelewi na baadaye ilipokelewa na alisema yuko location anatengeneza filamu na mwigizaji Rado hivyo tumtafute baadaye.

MAMA ALIA BAADA YA KUJIFUNGUA MAPACHA WALIOUNGANA KWENYE MAKALIO MBEYA...!!!


MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Kasumuru, Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Grace Joel Lwesha (19), amelia baada ya kujifungua watoto walioungana.Akizungumza na waandishi wetu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jengo la Watoto, Grace alilia kutokana na kile alichodai kujifungua watoto walioungana wakati yeye ni maskini.
Watoto hao mapacha wa kiume, Eliudi na Elikana wameungana sehemu ya makalio hivyo kulazimika kutumia sehemu moja ya haja kubwa.


Grace aliwaambia waandishi wetu kwamba, watoto hao walizaliwa katika Hospitali ya Kyela, Februari 20, mwaka huu wakiwa na miguu miwili na mikono miwili kila mmoja.
“Baada ya kujifungua Machi mosi nilihamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa uchunguzi zaidi ili waweze kujua ni jinsi gani watakavyotenganishwa,” alisema.


Hata hivyo, hospitali hiyo ya mkoa haikufanikiwa badala yake Machi 16, walimhamishia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo kuanzia hapo mpaka sasa anafanyiwa maandalizi kwa ajili ya safari ya kupelekwa nchini India kwa upasuaji.

TUMUOMBEE MZEE MANDELA AFYA YAKE YAZIDI KUDORORA, IKULU KWA ZUMA HAKUKALILIKI...!!!

Nelson Mandela ‘Madiba’.
Habari hizo ambazo awali zilifanywa siri kabla ya kuvuja wikiendi iliyopita, zinasema kuwa Ikulu ya Afrika Kusini ilikosa umakini, hivyo ikaacha gari bovu limbembe Mzee Mandela na matokeo yake lilizimika kwenye barabara kuu (high way).

Kuzimika kwa gari hilo, kulisababisha hekaheka lakini ufumbuzi wa haraka ulikosekana mpaka dakika 40 baadaye ndipo ‘ambulance’ nyingine ilipofika eneo la tukio, ikambeba Mzee Mandela na kumuwahisha hospitali. 

Ikulu ya Afrika Kusini imelazimika kutoa tamko, baada ya wachambuzi kuelezea tukio hilo kwamba zilikuwa dakika 40 za hatari za Mzee Mandela, kwa maana nusura zichukue uhai wa kiongozi huyo aliyeongoza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, miaka ya 1900 nchini humo.
Tukio lenyewe, lilijiri Juni 8, mwaka huu (zaidi ya wiki mbili zilizopita) lakini ikawa kimya katika vyombo vya habari, japo minong’ono iliendelea kushamiri, kabla ya mambo kuwekwa hadharani wikiendi iliyopita. 

KIVIPI DAKIKA 40 ZA HATARI?
Kwa mujibu wa habari pamoja na makala za wachambuzi mbalimbali wa kisiasa nchini Afrika Kusini, muda mfupi baada ya Mzee Mandela kuondolewa barabarani pale gari lilipomzimikia na kuwahishwa katika Hospitali ya Mediclinic Heart, Pretoria, uvumi ulienea kuwa ameshafariki dunia.

HAWA NDIO AINA YA WANAUME ASIOWAPENDA JACQUELINE WOLPER "GAMBE"


Jacqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai hawapendi  wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni waume za watu na si rahisi kuonyesha mapenzi yao ya dhati kwake, pia hawezi kutembea nao hadharani kwa kuhofia ndoa zao.

“Unajua unapokuwa na mtu mwenye fedha zake halafu mtu mzima hivi unakosa penzi la kweli. Mapenzi yenu yatakuwa ya chumbani tu,” alisema.

“Hamtaweza kutembea pamoja, lakini ukiwa na kijana ambaye ni rafiki hana pesa na wewe una kazi lazima akuonyeshe jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake.

“Wengi wenye fedha zao kuna wakati wananiona nina dharau, lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke, ninahitaji kuwa na mtu anayenijali na kuwa karibu na mimi.

“Kuna watu wanaamini fedha zao ndio kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo ukileta mapenzi hayo lazima unione nina dharau.”
Anasema wengine huwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni malaya, lakini wanasahau kuwa nao ni binadamu.

“Kila binadamu anapenda na kupendwa,” alisema.

WASICHANA HAWA WAGUNDUA GENERATOR LINALOTUMIA MKOJO



WASICHANA wanne kutoka Nigeria wamegundua jinsi ambacyo mkojo unaweza kutumika kama mafuta ya kusukuma jenereta. Wasichana hao, Duro-Aina Adebola,Akindele Abiola, Faleke Oluwatoyin na Bello Eniola, wote wenye umri wa miaka 14 wamefanya maonyesho ya jenereta hilo na limeonekana kufanya kazi.

Genereta hilo linaweza kufanya kazi kwa muda wa saa moja likitumia lita moja tu ya mkojo. Linauwezo wa kuendesha vifaa vinavyotumia umeme wa kati kama vile taa, jokofu, redio, televisheni n.k, Sasa genereta hilo linafanyaje kazi?

Kwanza mkojo huo unawekwa kwenye chombo kiitwacho electolytic cell, ambacho hutenganisha mkojo huo na hydrogen. Kisha hydrogen hiyo huenda moja kwa moja kwenye chujio la maji kwaajili ya kuisafisha na kisha kuisukuma katika gas cylinder.

Hiyo gas cylinder nayo huisukuma hydrogen mpaka katika kitu kinachoitwa, liquid borax ambayo huisukuma hewa hiyo na kuliwezesha jenereta kufanya kazi.

MAREKANI YATOA ONYO KALI KWA MSAFARA WA RAIS OBAMA TANZANIA

Dar es Salaam. Licha ya ujumbe wa Rais wa Marekani, Barrack Obama kutarajiwa kufikia katika hoteli kubwa zenye hadhi wakati kiongozi huyo atakapowasili nchini Julai Mosi mwaka huu, Ikulu ya Marekani imetoa tahadhari ya vyakula ambavyo hawatakiwi kuvigusa wakiwa nchini ikiwa ni pamoja na kutumia maji ya bomba.
Mbali na tahadhari hiyo, ziara hiyo ya Obama itakuwa na ulinzi mkubwa ambao pengine haujawahi kutokea katika historia ya viongozi wa nje wanaotembelea Tanzania kwani utahusisha idadi kubwa ya magari, ndege za kijeshi na meli kubwa ya kivita ambazo zitakuwa zikifanya doria karibu na pwani ya Tanzania.
Tahadhari za matumizi ya chakula, maji na nyinginezo zimetolewa katika nchi zote tatu za Afrika ambazo Obama atatembelea, kila moja kwa jinsi Wamarekani hao wanavyoitathmini.
Rais Obama atatembelea nchi za Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.
Ulinzi
Vyombo vya usalama vya Marekani vimejipanga kuhakikisha ziara ya kiongozi huyo haivurugwi kwa namna yoyote ile. Tayari ndege za jeshi zilizobeba magari ya akiba 56, yakiwemo 14 aina ya ‘Cadillac One’ maalumu kwa ajili ya kiongozi huyo, yamewasili katika nchi hizo tatu za Afrika atakazotembelea.

ANGALIA MUME WA JOYCE KIRIA NA VIJANA WENGINE WACHADEMA WAKIWA NA PINGU, KESI YA UGAIDI IGUNGA


Bw.Henry Kilewo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza 

  
Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.


Kamanda Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na watuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 25, 2013

.
.

VIONGOZI WATANO WA CHADEMA WASHITAKIWA KWA UGAIDI .... MAJINA YA VIONGOZI HAO HAYA HAPA



Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es Salaam na vijana wengine leo wameshtakiwa kwa Ugaidi katika mahakama ya Hakimu mkazi Tabora mjini.

Mbali ya Kileo, vijana wengine wa Chadema, ni Evodius Justinian wa Buboka, Oscar Kaijage wa Shinyanga, Seif Magesa Kabuta wa Mwanza, Rajab Daniel Kihawa wa Dodoma, leo wamesomewa shitaka la Ugaidi kwa kumteka na kumwagia tindikali Musa Tesha katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika mwaka 2011.

Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka mawili wote, la kwanza ni la kufanya ugaidi, na la pilini kumwagia tindikali Musa Tesha.

Kesi hiyo ilikuwa ilisikilizwa mbele ya hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, ya Tabora Mjini,Joktani Rushwera, huku upande wa serikali ukiwakilishwa na Wakili Juma Massanja na Ildefons Mukandara Baada ya kusomewa shitaka hilo, Upande wa utetezi wa ukiongozwa na wakili Prof Abdalah Safari, ukiwajumlisha Peter Kibatala na Gasper Mwalyela ulitoa hoja kuiomba mahakama hiyo ifutilie mbali mashtaka hayo kwa sababu, kwanza mashtaka hayakuwa na uhai kwa kuwa yamefunguliwa bila ridhaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.

WABUNGE NA MASHOGA WATETA..... HOFU YA KUWA NA RAIS SHOGA TANZANIA YATANDA....!!!


WABUNGE wanachama wa Chama cha Kupambana na Ukimwi (TAPAC), wiki iliyopita walikutana na kujadiliana mambo mbalimbali na mashoga katika mkutano wa mwaka wa chama hicho uliofanyika kwa muda wa siku tatu mjini  Dodoma. Katika mkutano huo, baadhi ya wabunge walionyesha wasiwasi wa taifa kupata rais shoga katika miaka ijayo kutokana na ongezeko la mashoga hapa nchini.

Mbali na wasiwasi ulioonyeshwa na wabunge, mashoga waliokuwa wakihudhuria mkutano huo, walilalamikia vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa na wanajamii wenzao na kudai watambulike na wapatiwe huduma za msingi za kibinadamu.


Akizungumza katika mkutano huo uliomalizika jana, Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy (CCM), alitahadharisha uwezekano wa nchi kupata rais shoga katika miaka ijayo, iwapo hatua za makusudi za kudhibiti hali hiyo hazitachukuliwa.


“Tabia ya kuwapeleka watoto kwenye shule za mabweni wangali wadogo wa umri wa miaka hadi miwili, itatuletea matatizo baadaye.

“Katika shule nyingi za bweni vitendo vichafu vinafanyika, vikiwamo vya ushoga. Katika vyuo vikuu hivi sasa kuna mashoga wasiopungua 40,000. Hii ni hatari, tusipojihadhari tutakuwa na rais shoga katika miaka ijayo,” alisema Kessy huku akishangiliwa na wabunge.

Mbunge huyo alitaka elimu dhidi ya ushoga na athari zake ienezwe nchini kupitia vyombo vya habari na nyumba za ibada.

MWANAMKE AOLEWA NA WANAUME WAWILI NA KUISHI NAO...!!!

MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.

Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.

Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.

Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...